Habari kaka? Tunaomba utusaidie kufikisha kwa ndugu zetu Watanzania wenzetu watusaidie mchango wa matibabu ya mtoto wetu Savio Salvatory Tarimo (07) mwenye tatizo la saratani ya misuli ya jicho, iliyosababisha kupoteza jicho moja. Savio amefanyiwa matibabu kwenye hospitali za KCMC, BUGANDO, MUHIMBILI na OCEAN ROAD na kutokana na hali ya mtoto madaktari wamependekeza apelekwe India kwa matibabu ya juu zaidi.
Savio anatakiwa kupelekwa India haraka iwezekanavyo, hivyo tunaomba kuisaidia familia kwenye michango kwa ajili ya matibabu na safari. Gharama ni TZS 120,000,000/= na kutokana na ukubwa wa gharama hizo, familia hatuwezi kumudu peke yetu, hivyo tunaomba watanzania watusaidie kutushika mkono ili kuokoa maisha ya mtoto wetu Savio.
Yeyote atakayeguswa anaweza kutuma mchango wake kupitia Yas/Tigopesa 0712707714 Prisca Tarimo, NMB BANK - 22202400365 Salvatory Tarimo, MPesa - 0767308110 Salvatory Tarimo, CRDB BANK - 0112009368200 Salvatory Tarimo. Tunatanguliza shukrani 🙏🏽
Naitwa Vumilia Mariki, mkazi wa Uru, Moshi, mkoani K'njaro. Naomba msaada wa matibabu kwa mwanangu Levina John (06) mwenye tatizo la miguu kupinda kiasi cha kushindwa kutembea.
Levina alizaliwa mzima kabisa na alipofikisha umri wa kutambaa alitambaa, baadaye akasimama na kisha kutembea. Lakini alipofikisha umri wa miaka minne miguu yake ilianza kupinda na ilizidi kupinda hadi akashindwa kutembea kabisa.
Kutokana na changamoto za kiuchumi nilishindwa kumpeleka hospitali hivyo nikawa nampeleka kwenye maombezi. Baadhi ya ndugu na marafiki walinishauri nimpeleke kwa waganga lakini nilikataa.
Nilimtumainia Mungu na kuamini kwamba ataniinulia watu wa kumsaidia mwanangu kusimama tena. Mimi ni single mother na kutokana na changamoto za kimaisha nilirudi kwa wazazi wangu Uru, japo hawana uwezo wa kunisaidia lakini walinitia moyo na kuniombea.
Nilihangaika maeneo mbalimbali kuomba msaada bila mafanikio. Nilikaribia kukata tamaa kuona mwanangu anakua mlemavu nami sina jinsi ya kumsaidia. Lakini nikapata msaada wa TZS 600,000/= kupitia kikundi cha “Sadaka Yetu” nikampeleka mtoto hospitali ya Mawenzi.
Baada ya vipimo aligundulika kuwa na tatizo liitwalo Tibia vara (Blount’s disease) yaani ukuaji usio wa kawaida wa sahani ya tibia inayosababisha mfupa kupinda kwa ndani.
Walinipa rufaa kwenda CCBRT kwa matibabu zaidi. Akajitokeza msamaria mwema mmoja ambaye alinichukua mimi na mtoto kwenda CCBRT Dar.
Madaktari walishauri ili mwanangu aweze kusimama tena anahitaji operesheni 4 yaani mbili kila mguu. Kila operesheni itagharimu kiasi cha TZS 1.2M hivyo jumla ni 4.8M.
Namshukuru msamaria aliyenitoa Moshi alilipia gharama za operesheni moja. Sasa imesalia operesheni moja kwenye mguu aliofanyiwa, na operesheni mbili kwa mguu mwingine.
Jumla ya gharama zinazohitajika ni 3.6M. Naomba Watanzania wanisaidie ili kumuokoa mwanangu na ulemavu. Nimeambiwa akikamilisha operesheni hizi atakuwa na uwezo wa kutembea tena. Mungu awabariki.
#MyTake:
Mimi na wewe tuna nafasi ya kumsaidia mtoto Levina kusimama tena. Tuma sadaka yako kupitia M-PESA #0752581983, Tigopesa #0719744954, CRDB #0150633516500, NMB #24110012109 Gifted Hearts Foundation. RudishaTabasamu, LetLoveLead.
Hiyo ni jana nikiwa hospitalini mloganzila ndugu zangu nilienda kwajili ya vipimo vikubwa vya xrei tumboni niomeona utumbo ulivyo jaa kinyesi, tatizo lingine linakuja dakitari alipo jaribu kunafanyia kipimo Cha haja kubwa akuta chembechembe ya kinyesi kinatoka akasema.
Assallam Alleykum Warahmatullah Wabarakatuh.!
Lile zoezi letu tunalofanyaga la kukusanya michango kwaajili ya Juzuu, In shaa Allah tutalifanya ndani ya mwezi huu wa Ramadhan na makadirio ni juzuu 2000 ambapo kila juzuu ni Tsh 400 🙏🏻
Na tutayatoa sadaka humu kwa wenye uhitaji 🙏🏻
Naumia kuona mwanangu akipoteza maisha nami sina namna ya kumsaidia. Nikiwa kama mzazi naandika kwa uchungu kutokana na kupata baraka ya mtoto ambayo imeambatana maumivu.
Naitwa Dismas Kweka, mkazi wa Hai, ni mzazi wa mtoto Ebenezer Kweka (miezi 9) mkazi wa Kata ya Narumu–Wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro.
Mwanangu alizaliwa na tatizo la kichwa kikubwa (hydrocephalus). Tulihangaika na matibabu yake mpaka akiba yetu ya mwisho. Tuliomba msaada kwa ndugu, jamaa na marafiki na mtoto akafanyiwa upasuaji hospitali ya KCMC Moshi kuwekewa mpira (ventricular shunt) wa kuondoa maji kichwani.
Tulimshukuru Mungu kwamba baada ya mahangaiko yote hatimaye mtoto wetu amepona. Licha ya kwamba nilifilisika kabisa hadi kutumia mtaji wangu wa biashara, lakini nilipata faraja kuona mwanangu amepona.
Lakini ni kama shetani alikuwa ananiwinda. Baada tu ya kutibiwa tatizo la kichwa, alianza kupata changamoto ya upumuaji, kutoka jasho kwa wingi, kushindwa kunyonya na kutetemeka kama ana degedege. Tulipomrudisha hospitali aligundulika kuwa na tundu kwenye moyo (VSD). Alipewa rufaa ya haraka kwenda JKCI kwa ajili ya upasuaji.
Baada ya kupata rufaa hiyo nilimshirikisha mke wangu na wote tukajikuta tunalia. Tulijiuliza kwa nini Mungu ameruhusu tukapita kwenye majaribu makubwa hivi? Hata hivyo tuliamini hakuna jaribu lisilo na mlango wa kutokea. Yeye aliyeruhusu jaribu hili litupate anajua namna ya kututoa hapa.
Kwa msaada wa ndugu na marafiki tulifanikiwa kumleta Ebwnezer taasisi ya moyo ya JKCI ambako alifanyiwa vipimo, na sasa anatakiwa kufanyiwa upasuaji ambao gharama yake ni zaidi ya 7M. Hata hivyo baada ya kuomba na kueleza hali yetu walitupunguzia hadi 4M ambayo hata hivyo hatuna uwezo wa kuipata. Nimebaki tu nikiangalia mwanangu nisijue cha kufanya.
Mimi na mke wangu kwa unyenyekevu mkubwa, tunaomba Watanzania watusaidie kuokoa maisha ya kijana wetu Ebenezer, mzaliwa wetu wa kwanza. Hatuna cha kuwalipa zaidi ya kuwaombea baraka kwa Mungu.
#MyTake:
Ukiguswa kuokoa maisha ya mtoto Ebenezer, tuma sadaka yako kupitia: M-PESA: #0752581983 Tigopesa: #0719744954 CRDB: #0150633516500 NMB: #24110012109 Gifted Hearts Foundation #RudishaTabasamu #LetLoveLead