🚨INFANTINO KWANINI YUPO KIMYA?? @FIFAcom NA AFRICA INANYANYASIKA
Gianni Infantino alimchagua Omar Abdulkadir Artan kama mwamuzi bora wa Afrika na Msomali wa kwanza kuwahi kuchezesha Kombe la Dunia kisha anashuhudia mamlaka za Marekani zikimnyima kuingia nchini licha ya kuwa na pasipoti ya kidiplomasia na visa halali
Alirejeshwa mpakani kana kwamba hana thamani yoyote, Hakukuwa na maelezo, hakukuwa na utetezi na wala hakukuwa na msimamo kutoka FIFA
INFANTINO Unahubiri kuhusu "umoja wa soka duniani" na "football for all", lakini wakati maafisa wa Afrika wanapodhalilishwa kwa sababu za kisiasa za mipakani, unakaa kimya🚮🗑️
Huu si uongozi, huu ni woga na usaliti kwa mchezo wenyewe
RAISI WA HOVYO ZAIDI KUWAHI KUTOKEA (Afrika haitaisahau fedheha hii)
Stand up or step down.