Wanamuziki wa Hip Hop Tanzania, Fid Q na Lord Eyes usiku wa kuamkia November 02 2024 kwa pamoja wametambulisha vionjo kadhaa vilivyomo kwenye album yao ya kwanza iitwayo ‘Neno’ ambayo inatarajiwa kutoka hivi karibuni na moja ya mambo yaliyogusa hisia za wengi ni perfomance ya Mzee Zahiri Zoro ambaye baada ya kukaa ndani kwa zaidi ya mwaka mmoja na miezi minne, Mzee Zoro ameibuka na Wheel Chair kwenye show hiyo.
Vionjo hivyo ni baadhi ya vitu vinavyopatikana kwenye album yao ya NENO yenye nyimbo 15 na vionjo vilivyotolewa ni nyimbo 7 tu kwa ajili ya Wadau wachache walioalikwa kusikiliza wakiwemo Viongozi wa Serikali, Mabalozi mbalimbali, Wasanii na Waandishi wa habari.
Akiongea na Waandishi wa Habari, Rappa Fid Q amesema “Leo tumewaonjesha Wadau nyimbo 7 kutoka kwenye album yetu yenye nyimbo 15 na baada ya hapa, Mashabiki wa muziki wategemee kuona tour ya Fid Q na Lord Eyes tukiwafata hukohuko waliko”
Upande wa Lord Eyes amesema ‘Huu ni mradi mkubwa, ndani ya albamu hii kuna albamu 3 ndani yake, itakuja na Filamu fupi, nia yetu kufanya mapinduzi ya muziki wa hip hop Tanzania, Neno the Album inakuja hivi karibuni’
Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma akiwasilisha salaam za Rais Samia amesema ‘Rais anafurahia kuona Watanzania wanafurahi kupitia Sanaa ya Nchi yao na sisi kama Wizara tutahakikisha hivi vitu havikwami sehemu yoyote na tutaunga mkono kwa asilimia mia”
Nyimbo zilizotambulishwa kwenye usiku wa Neno Experience iliyoandaliwa na Wanene Entertainment ni pamoja na Glory RMX, Cheupe, Okey na Dunia na baadhi ya Wasanii walioshirikishwa kwenye album hiyo ni pamoja na Damian Soul, Zahir Ally Zoro na Melissa John.
#MillardAyoUPDATES
Fortunate for my team & super grateful for having Mzee Zorro @ZahirAlly on stage with us. It doesn’t get more HIP HOP than that! One NENO, one EXPERIENCE
BTW; hip hop kama hip hop has always been a competitive field, with everyone claiming to be the best..But it takes more than just being a skilled MC to dominate, succeed, or create art that appeals to a larger audience.
One of my fave female activists once gave me some much-needed wisdom after I was snubbed at an awards show. She said to me, ‘Your talent cannot be tarnished by the lack of accolades. We know who you are—you’re destined for greatness’
Lord is nowhere near being considered a weak MC. In fact, if comments count in this debate…we should also look at how well-received his verse was during its release —-> https://t.co/bpWAaaHdeH