Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) liliingia mkataba wa miaka mitano wenye thamani ya Shilingi Bilioni 3 na Kampuni ya Sandaland Fashion Wear Limited (@sandaland_theonlyonetz ), kwa ajili ya kuzalisha na kuzivalisha jezi timu za Taifa za Tanzania. Mkataba huo ulisainiwa Septemba 2023.
Wakati wa kusainiwa kwa mkataba huo, Sandaland ilikubaliana kuipatia TFF jezi pamoja na fedha taslimu kila mwaka kwa kipindi cha mkataba.
Aidha, Rais wa TFF, Wallace Karia, alisema mkataba huo ungepunguza gharama ambazo TFF ilikuwa ikitumia kununua jezi za timu za Taifa.
Mkataba huo ulihusisha timu za Taifa za Tanzania, zikiwemo Taifa Stars na timu nyingine za Taifa za wanaume na wanawake, huku Sandaland ikiwa na jukumu la kutengeneza na kusambaza jezi hizo.
#KitengeSports
Wataalamu wa michezo mtusaidie, nini kimemkuta kocha wetu mwanzoni mwa tulikua na timu ambayo tunashinda kwa goli nyingi mpaka tukawa tunatamba tutakuja kumfunga mtu 7, sasa imekuaje mbona now tunapata ushindi kiduchu hata kwa timu za kawaida NINI SHIDA au tuwaheshimu WAPINZANI
Nachukua fursa hii kuwashukuru na kuwaombea baraka with a special shoutout keyboard na microphone warriors wote mliokuwa mnahudhuria kesi ya Tundu Lissu kimyakimya kila siku ✊🏽
Mnatu represent vyema na Mungu awalinde! Maana mmeacha shughuli zenu kuwa hapo Mahakamani- come rain or shine! Na hamtambi wala hamna kitu mta gain zaidi ya thawabu!
Ndo maana tunasema kuwa Tundu Lissu ni icon wa Taifa tutamlinda kwa wivu mkubwa
#FreeTunduLissu
SHERIA SIYO MITULINGA😂:
Ule muda wa mimi KUFUNDISHA SHERIA umewadia. Kuanzia tarehe 5 Oktoba 2026 👇 nitakuwa MAHAKAMA YA RUFANI pale ARUSHA ili KUTUNGA SHERIA MPYA (Precedent) ya “PLEA BARGAIN”. Kutakua HAKUNA KIINGILIO. Wote MNAKARIBISHWA.
Hakuna wa kuja kutuokoa! Tujiandae kabisa kisaikolojia! Lissu hatupambanii bali anatuonyesha njia
Sisi ndo tunatakiwa kumpambania na kujipambania
Waovu hawaendi kumwachia labda akubali masharti yao
Tundu Lissu is human - he needs our support! Nobody is coming to save us!
#FreeTunduLissu
.... Leo nimepata bahati kuongoza maombi kabla ya kunaza kwa Kesi ya uongo inayomkabili Mwenyekiti Tundu Lissu.
Nimerejea kitabu cha Issaya 33:22, nakuukumbusha umma kuwa Bwana ndie Mfalme, Mwamuzi na Mtunga sheria wa Haki.
Wamtumainiao hawataachwaa.
Nilipokutana na Mchungaji PETER MSIGWA katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Dar es Salaam kwenye Kesi ya UHAINI inayomkabili TUNDU LISSU, leo tarehe 18 Septemba 2026
Tundu Lissu ameeleza Mahakama Kuu kwamba, ameelezwa na DCI Ramadhan Kingai, hata CDF Jacob Mkunda na IGP Cammilius Wambura pia hawapo tayari kutoa ushahidi upande wa utetezi, kwa sababu ile ile wapo upande wa watu watakaoshangilia TAL akipatikana na hatia ya kunyongwa hadi kufa.
BREAKING NEWS : Mmiliki wa Kampuni ya SANDALAND amesema atamshtaki BWANA CHUGA kwa kudai Kampuni yake imedhalilishwa kwa kuambiwa jezi hazina QUALITY
Sandaland amedai anamkataba halali na TFF nayeye kauli ya BWANA CHUGA imeishushia hadhi kampuni na imemuharibia
✍️ : Kitenge TV
Kampuni ya Sandaland Fashion Wear Limited imetangaza kuchukua hatua za kisheria dhidi ya kauli iliyotolewa hadharani na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, kuhusu jezi za Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars.
Hatua hiyo imetangazwa kupitia tamko rasmi la kampuni hiyo, iliyosema kauli ya Makonda iliyotolewa Septemba 16, 2026 kupitia akaunti yake ya Instagram imeathiri jina, chapa, hadhi na uhalali wa bidhaa za Sandaland katika soko.
Katika ujumbe huo, Makonda alinukuliwa akisema: “Hii sio jezi ya Taifa Stars, Taifa Stars kwa ubora wake hatuwezi kuwa na jezi za kiwango chini hivi. Acheni kutumia picha za Naibu wangu huku ofisi yangu haina taarifa.” Ujumbe huo uliambatana na picha ya Naibu Waziri Hamis Mwinjuma, maarufu Mwana FA, akiwa amevalia jezi yenye mchanganyiko wa rangi ya njano, bluu, nyeusi iliyochanganyika na kijani.
Sandaland imesema kauli hiyo imezua taharuki na sintofahamu, huku ikidai kuwa tayari imesababisha madhara ya kiuchumi na kwa hadhi ya kampuni. Kampuni hiyo imeeleza kuwa ina mkataba halali na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) wa kutengeneza na kusambaza jezi za Taifa Stars, ambazo zimekwishatumika katika mashindano mbalimbali ya timu za taifa za wanaume na wanawake.
Kutokana na hali hiyo, Sandaland imesema haitanyamaza na inakusudia kuchukua hatua za kisheria dhidi ya kauli hiyo, ikidai kuwa ilitolewa kwa namna inayoweza kuichafua chapa yake. Kampuni hiyo pia imesisitiza kuwa imejenga jina na heshima yake kwa muda mrefu na ilipewa dhamana kimkataba ya kushughulikia jezi za Taifa Stars.
#KitengeSports
SC Tundu Lissu amefunga utetezi wake baada ya Samia, Majaliwa, Mpango, DGIS, IGP, CDF & DCI kuingia mitini.
Kesi nzima imekuwa ni darasa huru la ubovu wa mfumo wetu uchaguzi, haki jinai na utawala.
We thank God & looking forward to his RELEASE!
Free Tundu Lissu!
Tundu Lissu amepanda kizimbani na kuieleza Mahakama Kuu ya Tanzania kwamba DCI Ramadhan Kingai amesema hayupo tayari kutoa ushahidi upande wa utetezi na amemueleza (yeye) yupo upande wa wale watu ambao watashangilia na kufurahi Mahakama ikimkuta na hatia ya kunyongwa hadi kufa.
Jamaa ana akili sana imenikumbusha 2020 akichukua form wakiwa CHADEMA wagombea zaidi ya 200 wamewekewa mapingamizi kugombea nafasi mbali mbali! Ye alipiga Utosini akamwekea Magufuli pingamizi la kugombea kwa makosa Yale Yale kwa wanayotuhumiwa nayo wa CHADEMA, ikabidi TUME Kesho yake waondoe mapingamizi yote! Jamaa ana akili sana yan
Video ya kwanza ikionesha Mangi aliyepigwa mkwara na kumuacha Mwenyekiti BAVICHA akidharirishwa.
Video ya pili ni mama mmoja aliyejitosa kwenda kumtoa kijana aliyeluwa akipigwa na polisi.