#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 226
Anaendelea Mhe. Lissu.
Waheshimiwa Majaji uamuzi uliotolewa na Mahakama ya rufani katika kesi ya Katibu Mkuu wa CHADEMA na bodi ya wadhamini wa CHADEMA vs Saidi Issa Mohammed na wenzake inasema kwamba kama mdaawa (Mleta maombi) analeta maombi mwenyewe ni yale yaliyoko kifungu cha 6 kifungu kidogo cha e, maombi mengine ni Mahakama yenyewe ndiyo inaamua bila kusukumwa na yeyote au kuletewa maombi yenye hati ya kiapo.
Waheshimiwa Majaji kwa vyovyote vile maombi hayo hayako halali mbele ya mahakama hii kwani hayakuletwa katika utaratibu wa kisheria kwani Mahakama hii haijaamua maombi haya yaje yenyewe Suo moto kwa hiyo Mahakama isikubali kusikiliza maombi hayo kwasababu ambazo nimezisema.
Anaendelea Mhe. Lissu
Sasa waheshimiwa Majaji sijui kama mnaniruhusi niendelee au wajibu kwanza.
Jaji anasema Jamhuri wajibu kwanza PO kisha tutaendelea.
Anasimama Wakili Katuga anasema Waheshimiwa Majaji tukirejea mapingamizi yake ya awali yameletwa chini ya kifunga cha 8.2.d hiki ni kifungu mahususi kwa mashauri ya madai.
kifungu hiki kilikopwa kikatumika kwenye madai kwenye mashauri ya rufaa, hata kama Mahakama yenu tukufu kwa rejea hizo za Mahakama hii ikakikopa kitumike kwenye maombi yetu haya bado tunasema kwamba maombi yetu yako sahihi mbele ya mahakama hii tukufu tofauti na kile ambacho mjibu maombi amekileta kama pingamizi la awali.
Maombi yetu yameletwa chini ya kifungu cha 6 specifically kifungu kidogo cha 3 cha Sheria ya mamlaka ya Mahakama. Kanuni ya 65 na kanuni ya 45 ya kanuni za Mahakama ya Rufani inasuport maombi yetu.
Anaendelea Wakili wa Serikali Katuga
Waheshimiwa Majaji ukiyasoma maombi yetu kwenye notice of motion hakuna sehemu yeyote tunayoiomba Mahakama hii tukufu ipitie order ya Mahakama au uamuzi wa Mahakama, pale mwisho tunasema Mahakama idiscuss kukataa ushahidi hatujazungumzia kukataa notice, sisi tunazungumzia kuuchambua na kuukataa ushahidi.
Hakuna sehemu kwenye maombi haya tunalalamikia order, Mahakama yenu itaona kwamba pingamizi la mjibu maombi limekuwa mislead hakuconsue sawasawa maombi yetu.
Pale ambapo neno or litatumika kwenye Sheria yeyote maana yake maneno haya hayako similar yanatumika tofauti, Waheshimiwa Majaji nimewarejesha humu muweze kukitafsiri kifungu cha sita. Haya maneno yanatakiwa yatafisiriwe tofauti hayaendi pamoja ama hayategemeani, inaweza kuwa kimoja wapo kati ya haya.
Kama mahakama yenu imekikopa kifungu cha 8.2.d kinazungumzia katazo la decision or order ndo hauwezi kuziombea appeal or revision.
Sasa tunapata wapi nguvu za kuleta pingamizi kwa tafsiri hiyo tunaiomba Mahakama hii ikaangalie maana ya maneno haya.
Waheshimiwa nawarejesha kwenye kamusi kwa sababu nayo ni kati ya vitu vinavyopaswa kutumika kutafsiri Sheria. Katika ukurasa wa 129 kamusi inadefine order ni nini?
Kwenye application yetu hakuna sehemu tumeombea decision or order, kwenye kifungu cha 8 hata kama kimekopwa hakiwezi kucocer maombi yetu.
Mahakama yenu ilishawahi kuiamulia hili kwenye kifungu 394 cha CPA, katika kesi ya Peter Michael Madeleka dhidi ya jamhuri.
Kutaja kitu fulani means exclusion ya kitu kingine, kitendo cha kifungu cha 8 kutaja findings and order means haijatuzuia kwa maana hiyo findings hapa haijazuiwa kwa maana hiyo tunachotaka kuiambia Mahakama yako ni kwamba ule ushahidi ulikataliwa kabla ya wakati wake.
Anaendelea Wakili wa Serikali Katuga
Waheshimiwa naomba niishie hapo kwenye hilo ili tusiende mbali kwa kuyasema hayo mtaona kwamba kesi ambazo mshitakiwa amewapitisha ni distinguishable kwenye mazingira yetu.
Hii kauli ya kwamba hatuna mamlaka ya kuomba Mahakama iitishe ‘Suo moto’ sisi tunasema mamlaka tunayo.
Katiba anasema naomba Mrema anisaidie anayo nyongeza.
Anasimama Wakili wa Serikali huyu anaitwa Job Mrema anakipara kama Mrema wa ubwabwani, sijui na yeye huwa anakunywa visungura kama mwenzake, anyway
Part 227 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Leo July 3, 2026
Last time kwenye ya Uhaini dhidi ya Mhe. Lissu tuliishia part 224 so leo tunaendelea na -;
Part 225
Mheshimiwa Tundu Lissu anaingia ndani ya chumba cha mahakama, ukumbi namba 01 wa Mahakama Kuu.
Anaonekana mwenye tabasamu na furaha usoni kwake kama ilivyo siku zote.
Upande wa Jamhuri wapo kama kawaida yao
Inapigwa Court…..
Jopo la Majaji watatu wanaingia,
Kesi inatajwa
Anasimama Wakili wa Serikali anajitambulisha jina lake Ajuaye kisha anatambulisha Mawakili wenzake.
Jaji anaamuliza Mhe. Lissu kama yupo tayari
Mhe. Lissu anasema yuko tayari kuendelea.
Kama kawaida yao anasimama Wakili wa Serikali Katuga kuweka pingamizi.
Mhe. Lissu anapendekeza maombi yake ya sikilizwe kwanza ndo pingamizi lao lijibiwe.
Majaji wanasema tuanze kwanza kusikiliza PO, kisha taratibu nyingine zitafuata.
Anaanza Mhe. Lissu Waheshimiwa Majaji kesi hii inatokana na maombi namba 19065 ya mwaka 2025, Juu ya maombi ya kuongeza ushahidi katika muendelezo wa kesi, uamuzi wa tarehe 24 February 2026 wa Mahakama Kuu wa kukataa kuingizwa kwa ushahidi mpya.
Waheshimiwa Majaji uamuzi wa February 24, 2026 ni uamuzi mdogo, uamuzi ambao haujamaliza shauri na kwa mantiki hiyo kisheria kabisa haupaswi kukatiwa rufaa au pingamizi.
Waheshimiwa Majaji wa rufaa, Mahakama hii katika kesi ya Mkurugenzi wa Mashitaka dhidi ya Mohammed Mussa Ussi criminal appeal namba 521 ya mwaka 2023 Mahakama ikiwa imeketi Zanzibar ilisema msingi wa kukataza rufaa ama mrejesho (revision) ya jinai msingi wa hiyo hoja ni kifungu cha 8.2.d kutokana na marejeo ya mwaka 2023 mahakama hii ilisema uamuzi huo hauwezi kukatiwa rufaa kwani ni uamuzi usiomaliza shauri.
Anaendelea Mhe.Lissu
Kesi ambazo nimeziwasilisha mbele yenu waheshimiwa Majaji zinazungumzia uamuzi mdogo ni wa aina gani na uamuzi unaoweza kutolewa kama uamuzi wa mwisho unaoweza kuombewa revision ni wa aina gani.
Uamuzi unaomaliza kesi na kunyima haki za wadaawa ndiyo unaopaswa kukatiwa rufaa, uamuzi unaokuwa treated as the final order ndiyo unaomaliza haki za msingi za wadaawa lakini kama uamuzi haufanyi hivyo hauwezi kukatiwa rufaa.
Sasa waheshimiwa Majaji baada ya kuwapitisha kwenye kesi hizo nirudi kwenye hoja yangu ya msingi je uamuzi wa February 24 mwaka huu ulimaliza kesi hii?
Kama ni hivo ulimaliza kesi hii na kwamba Sasa hivi sina kesi ya uhaini basi hoja yangu haina msingi na maombi haya hayawezi kusikilizwa.
Hoja yangu waheshimiwa Majaji ni kwamba uamuzi wa Mahakama Kuu wa February 24, 2026 haukumaliza kesi namba 19065/2025 na kwasababu haukumaliza maombi haya ya revision yanakatazwa kuletwa Mahakama ya Rufaa.
Anaendelea Mhe.Lissu
Waheshimiwa Majaji uamuzi huo unasema nini, ili tujue kama ulimaliza kesi lazima tuusome huo uamuzi unasema nini.?
Rulling yenyewe iko ukurasa wa 405-432, kwenye ukurasa wa 431 paragraph ya mwisho waheshimiwa Majaji mtaona Mahakama ilichokiamua.
Kilichokataliwa kupokelewa na Mahakama ni notice of additional substance of evidence, Mahakama Kuu haikusema kesi haitaendelea. Mahakama kuu ilitoa Mwongozo haikutoa uamuzi wa mwisho wa kesi, uamuzi wao ulikataa subodinate issue.
Waheshimiwa Majaji ushaidi mwingine huko kwenye maombi yenyewe yaliyoletwa. Mahakama inasema ilijadili na kukataa notice yao ya kuongeza ushahidi haisemi kesi ilifia hapo kutokana na uamuzi huo.
Mahakama imekata notice of additional substance of evidence, kwahiyo wanalalamikia uamuzi wa notice kukataliwa.
Jambo la pili ni Je mleta maombi anayo mamlaka ya kuiambia Mahakama itumie mamlaka yake ya kupitia kumbukumbu ili kuridhisha matakwa yake mwenyewe?
Jibu ni hapana hiyo siyo haki yao kisheria kwani wajibu wa kuangalia record ni wa mamlaka yenyewe.
Part 226 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba repost yako.
TAARIFA KWA UMMA
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinasikitika kuwatangazia kifo cha Suez Dani Maradifu ambaye ni dereva wa Makamu Mwenyekiti Bara, Mheshimiwa John Heche.
Suez amekutwa amefariki leo asubuhi Jumatano, Julai 01, 2026 chumbani kwenye nyumba ya wageni aliyofikia, mjini Kigoma.
Mwili umechukuliwa na Polisi kuupeleka hospitali ya mkoa wa Kigoma kwa ajili ya taratibu nyingine za uchunguzi.
Chama kinatoa pole kwa familia ya marehemu, wanachama, ndugu jamaa na marafiki kwenye msiba huu mzito.
Taarifa zaidi tutaendelea kuzitoa.
Bwana alitoa. Bwana ametwaa. Jina lake lihimidiwe. Amina
Hii tuliifahamu, mbogamboga lazima muogope. Hatimaye mmekimbia magetoni baada ya kupigwa paipu mfululu. Tumewatandika spakoo za kutosha sana. Pumzi ndogo, hamuwezi kufanya siasa za kujibu hoja, mmeomba msaada wa bunduki. Mbogamboga mnachokishuhudia sasa sivyo mlivyotarajia. Kila CHADEMA inapokanyaga ni mtiti, mafuriko. Wananchi wanapambana kwa nguvu kuchangia harakati za chama kupitia TONE TONE. Tunajua ile inawauma sana. MaCCM, mlifikiri kwa kupora uchaguzi, kujitangazia ushindi wa 98% na kujipachikia kura milioni 32, mngetawala bila upinzani na kuizika CHADEMA kisiasa? Uhalali haujengwi kwa kupora uchaguzi, unatokana na ridhaa ya wananchi. Mkaenda kufadhili mashoga zenu (ACT na CHAUMMA) ili washiriki uigizaji wenu wa demokrasia bandia. Baada ya kupora uchaguzi wameshindwa kufanya mikutano ya hadhara. Mbogamboga, hamtaweza kuwanyamazisha watu wote. Sisi siyo mazombi. #KatibaMpya #FreeTunduLissu
Zile NYOMI za CHADEMA ilikuwa lazima tuu wasenge warudishe nchi GIZANI.
CHADEMA ilikuwa inapiga PAIPU back-to-back sio poa. Sasa vilaza hawana majibu ya hoja zetu wanaamua kurudisha nchi GIZANI.
Huu ni ushahidi mwigine kuiambia DUNIA Tanzania tupo UTUMWANI tunahitaji msaada.
Leo tarehe 25 Juni 2026 nimemaliza ZIARA yangu ya kikazi katika nchi za Ujerumani, Uholanzi, Ufaransa, Ubelgiji na Uswisi. Ninamshukuru MUNGU kwa MAFANIKIO MAKUBWA yaliyopatikana kwenye ZIARA hiyo. 👇