USIOMBE kudaiwa na serikali; huwa wanataka chao leo leo kama siyo kesho. Sasa, wewe uwe ndo unaidai serikal; hakuna ofisi utaacha kuijua. Utazunguka hadi uzeeke au ufe na hutakaa upewe chako. Kwa ufupi, omba usidaiwe wala kuidai serikali.
Ukiuelewa uwezo uliomo ndani yako na ukaweza kuuachilia uonekane, wewe unajiamini.
Ukiutambua ukomo wa uwezo ulionao, wewe ni mnyenyekevu.
Ukijiamini kiasi cha kuanza kufikiri uwezo wako hauna ukomo, wewe unasumbuliwa na kiburi. Usipochukua hatua mazingira yatakunyenyekeza.