Kwa ndugu zangu, Watanzania ๐น๐ฟ
Kuna nyakati giza linapotanda, sauti za haki zinaponyamazishwa, na mioyo ya watu wema inapokata tamaa. Lakini hata katika kimya hicho, bado kuna tumaini. Tumaini kwamba kila kizazi huamka, huuliza maswali, na huchagua kusimama upande wa kweli.
Wise men speak because they have something to say; fools because they have to say something.
Wenye hekima husema kwa sababu wana cha kusema; wapumbavu kwa sababu wanapaswa tu kusema kitu.
"Mimi kama kaka, kama mshika dau wa sanaa ninawaombea radhi [wasanii] kwa niaba yao ili kiwanda kiendelee kusonga mbele." - Francis Ciza (Majizzo), Mmiliki wa E-FM Company Limited
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imesema uzalishaji wa maji kwenye mtambo wa Ruvu Chini umeshuka kutoka lita milioni 270 hadi lita milioni 50 kwa siku, na kusababisha tatizo la maji mkoani humo.
Afisa Mtendaji Mkuu DAWASA, Mkama Bwire amesema sababu hizo zimetokana na mvua za masika kunyesha chini ya wastani, kuchelewa kwa mvua za vuli zilizotarajiwa kunyesha mwezi Oktoba, kuongezeka kwa joto na kuongezeka kwa shughuli za kibinadamu ndani ya Bonde la Mto Ruvu.
Wise men speak because they have something to say; fools because they have to say something.โ
Wenye hekima husema kwa sababu wana cha kusema; wapumbavu kwa sababu wanapaswa tu kusema kitu.
Cc: @godbless_lema@mj0058@MiriamMkanaka
Uamuzi wa kusema au kunyamaza hauhitaji akili nyingi, unahitaji utulivu na kusudi sahihi. Kati ya maneno na ukimya, chagua kile kinachojenga, kinacholinda, na kinachotenda haki.
Kwa hiyo, wacha tusinyamaze tena.
Wacha tuwe kizazi kinachoamua kulipa gharama ya kusema kweli kwa upendo.
Kwa ajili ya watoto wetu, nchi yetu, na heshima ya mwanadamu. Tumaini bado lipo. Na kila mmoja wetu ana nafasi ya kulihuisha kwa sauti, kwa kalamu, na kwa matendo.
Najua kuna uchungu mwingi, lakini pia kuna nguvu nyingi ndani yetu.
Ukombozi wa kweli hauanzi kwa risasi, bali kwa sauti, sauti inayosema, โInatosha.โ
Sauti inayotetea uhai, haki, na utu.
Nchi yetu imepitia mengi, huzuni, hasara, na maumivu. Lakini bado tuna nafasi ya kuandika simulizi jipya; simulizi la ujasiri, upendo, na uwajibikaji. Wakati wema wanaponyamaza, uovu hushamiri; lakini wakati watu wa Mungu wanapoinua sauti zao, milango ya mabadiliko hufunguka.
Kukata tamaa ktk kuutafuta wema wa watu ni dhambi mbaya sana ktk maisha ya Binadamu. Kuutafuta wema na haki inapaswa kuwa kusudi la kila mmoja ktk maisha. Matatizo mengi duniani yanasababishwa na watu wema kukaa kimya wakati uovu unashamiri. Mateso kwa ajili ya haki ni Faraja kubwa sana ya moyo. Hata wanaofikiri sisi ni maadui zao wanapaswa kujua kuwa sisi ni marafiki zao na jitihada zetu ni kwa ajili ya watoto na wajukuu zao pia. Tuko nje kwa dhamana.