Mtoto wa Mungu jidhabihu kwenye maombi, mwanzoni itakuwa mahangaiko kweli [real struggles] lakini mwili na nafsi vikishaanza kuzama hutoki. Uzuri wake huwezi kuuhadithia kwa lugha ya kutosha.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Leo November 6, 2026
Last time tuliishia part 493 so leo tunaendelea na -;
Part 494.
Karani amewasha kipaza sauti kutoa Tangazo kuwa watu wakae kwenye viti vyao na simu zao wahakikishe zinatolewa sauti na milio ya aina yote.
Waandishi wa Habari na wao wako wakutosha sijawahi kuwaona Mahakamani kwenye kesi yoyote wakiwa wa idadi hii ni wengi sana sana.
Hata waandishi ambao huwa hawajagi kabisa naona wamekuja, namuona yule Charles William wa Wasafi nae leo yupo kuna mtiti hapa unataka kutokea, wanataka kumnyayua Mzee Mpoki alienda kukaa viti vya Mawakili wa Serikali 😂😂😂
Wale watoto wa serikali ambao huwa wanakaa kwenye benchi la nyuma ya akina Katuga, leo wamekaa mawakili wa Mhe. wabishi hatari wamegoma kusimama.
Ameingia Mheshimiwa Lissu akiwa na vibe na kusema TUTAFIKA! TUTAFIKA! TUTAFIKA!
Wameingia Mawakili wa Serikali.
MAJAJI walikwisha ingia hata kabla Mawakili wa Serikali hawajaingia.
Muda huu wanawasha zile mic zao ili tuendelee.
Jaji Ndunguru anasema karani tuendeleeee.
Jamhuri dhidi ya Lissu. Anasoma namba ya shauri karani.
Anasimama Katuga anajitambulisha niko na wenzangu Job Mrema, Cathbert mbiringe ba Winniwa Kasala
Tunaiwakilisha Jamhuri na Mshitakiwa yupo.
Shauri linakuja kwa ajili ya uamuzi na upande wa Jamhuri tuko tayari.
Mshitakiwa vipi wewe?
Mheshimiwa Lissu anasema niko tayari pia.
Majaji Wanateta pale kabla hawajaanza kuusoma huo uamuzi.
Jaji Ndunguru anasoma, naomba tusikilize Hukumu.
Katika shauri hili Mshitakiwa Tundu Lissu anashitakiwa kwa kosa la uhaini kinyume na kifungu cha 39(2)d kanuni ya Adhabu 2023.
Maelezo yanasema kwamba Tarehe 03/04/2025 Wilaya ya Kinondoni Dar es salaam mshitakiwa alitengeneza nia ya kuzuia uchaguzi wa 2025 kwa lengo la kuitishia Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Kudhihirisha nia hiyo kwa kitendo cha kutamka maneno ya wanasema kitu kimoja sahihi kwamba msimamo huu unaashiria uasi na tutahamasisha uasi na hiyo ndio namna ya kuleta mabadiliko na huu uchaguzi tutauvuruga.
Mshitakiwa alikana hati ya mashitaka na shauri likaanza kusikilizwa.
Kama ilivyo kawaida upande wa Mashitaka waliongozwa na Wakili Renatus Mkude na Ajuaye Zengeli na Nasoro Katuga na anawataja Mawakili wote wa Serikali.
Upande wa Mashitaka walileta mashahidi 17 na ambao kati yao 17 walikuwa ni mashahidi wanaolindwa.
Na mshitakiwa alijiwakilisha Mwenyewe na alileta Mashahidi wanne na yeye alikuwa watano na pia utetezi walitoa vielelezo anbavyo ni 16.
Baada ya upande wa mashitaka kutoa ushahidi na mshitakiwa alijitetea na walileta hoja za majumuisho walileta hoja hizo.
Mahakama hii iliongozwa na kanuni mbalimbali ni
1. Katika Mashauri ya Jinai mwenye jukumu la kuthibitisha ni Upande wa Mashitaka.
2. Kutiwa hatiani kwa mshitakiwa hakutazingatia udhaifu wa mshitakiwa.
3. Ushahidi utatazamwa kwa ujumla wake na sio vipande.
4. Mashaka yoyote hata kama yana uzito kiasi gani hayabadilishi burden ya kuthibitisha shitaka.
Mahakama hii imechunguza kwa umakini hati ya mashtaka, ushahidi na mawasilisho ya pande zote mbili na kuja viini vitatu vya kuthibitisha
Moja: Iwapo Mshtakiwa alikuwa chini ya utii wa JMT
Mbili: Iwapo Mshtakiwa alitengeneza nia ya kuzuia uchaguzi mkuu wa 2025 kwa lengo la kuitishia serikali.
Tatu: Iwapo mshtakiwa alidhihirisha nia hiyo kwa kutamka na kusambaza maneno hayo.
Mahakama imeona ni vyema ifafanue kwanza katika hoja ambazo zinaonekana kama mapingamizi wakati wa hoja za majumuisho ya mshtakiwa.
Kwa kuwa hati ya mashtaka ndio inayoanzisha shauri la jinai ni vyema tuamue kwanza kuhusu uhalali wa hati ya mashtaka. Mshtakiwa alisema hati ya mashtaka ina mapungufu katika maeneo matatu moja kuwa kwa mujibu wa kifungu cha 39(2)(d) kinazungumzia kuhamasisha kikundi cha watu, pili hati ya mashtaka haikutoa taarifa muhimu ambazo zilipelekea ashindwe kutoa utetezi kamili na tatu hakuna lengo lilioonyeshwa katika hati ya mashtaka.
Part 495 itaendele kwenye post inayofuata
Naomba Repost yako.
Katika katiba hii haki za binadamu, maadili ya viongozi na uwajibikaji ni dhaifu n hii ni kutokana na kuwepo na mianya Katika katiba hii. Matukio ya 2025 yamethibitisha hilo.
#KatibaMpya
@stevenBrain360 Hapo mzee kacheza karata mbili kwa ufasaha mkubwa, kwanza kafikisha ujumbe wenyw funzo kwa mke wake, pili ameliorate biashara ya mke wake maana angepanik angeuwa biashara mazima