#Habari:Tanzania imeungana na mataifa mengine Duniani kuadhimisha siku ya Malaria huku takwimu zikionesha kiwango cha maambukizi kupungua kutoka asilimia 14.4 mwaka 2015 hadi asilimia 7.3 mwaka 2017 huku mkoa wa Kigoma ukiongoza kwa maambukizi kwa kiwango cha asilimia 24.4.
#Habari:Wanafunzi 30 wa kike wa kidato cha tatu katika shule ya Sekondari Islamic iliyopo wilayani Sengerema mkoani Mwanza, wamenusurika kifo baada ya Bweni lao kuteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo.
#Habari:Makamu wa rais Mama Samia Suluhu Hassan amezindua mradi mkubwa wa ujenzi wa kiwanda cha Kemikali cha Msufini kitakachotengeneza Dawa za kusafisha maji utakaogharimu zaidi ya shilingi bilioni 200 na kuwataka watanzania kushiriki na kuthubutu katika uwekezaji wa viwanda.
#Habari:Wananchi wanaotumia Daraja linalounganisha kata za Tungi na Mkundi manispaa ya Morogoro wameiomba serikali kuchukua hatua za haraka kurekebisha eneo hilo baada ya mvua zinazonyesha kusababisha mafuriko katika Mto Ngerengere na maji kuvunja kingo za daraja lililopo
#Habari:Jeshi la Polisi mkoani Kagera limemfikisha Mahakamani Bw. Respicius Rugakingira anayekabiliwa na tuhuma ya kuwaua kikatili watoto wake Mapacha siku chache zilizopita mkoani Kagera.
#Habari:Serikali imesema kwa mwaka ujao wa fedha 2018/19 imejipanga kutekeleza ujenzi na ukarabati wa miradi mbalimbali ya Barabara ambapo bodi ya mfuko wa Barabara imetengewa zaidi ya bilioni 636 huku TARURA nayo ikitengewa zaidi ya Bilioni 272.
#Habari:Mvua zinazoendelea kunyesha zimeharibu miundombinu ya barabara ya Kangaye-Mecco wilayani Nyamagana pamoja na kukata mawasiliano ya Daraja kati ya Buhongwa na Kijiji cha Mwasonge wilayani Misungwi na kusababisha wakazi wa maeneo hayo kuvuka kwa kutumia usafiri wa Mitumbwi
#Habari:Idara ya uhamiaji mkoa wa Mara imekamata wahamiaji haramu sita raia wa Ethiopia baada ya kuingia nchini kupitia mpaka wa Sirari wilayani Tarime wakitokea Kenya katika Oparesheni inayoendelea mkoani humo .
#Habari:Madereva wanaondesha Magari yanayokusanya taka ngumu katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam wamelalamikia kukwama kushusha taka kwa siku tatu wakiwa wamepanga foleni katika eneo la Pugu Kinyamwezi kutokana na ubovu wa barabara.
#Habari:Wataalam kutoka kituo cha Taifa cha utafiti wa Miwa cha Kibaha kwa kushirikiana na bodi ya Sukari na kiwanda cha Sukari Kilombero wanaendesha tathimini ya athari za aina mpya ya wadudu wanaoshambulia Miwa katika bonde la Kilombero ili wasiendelee kuathiri zao hilo
#Habari:Waziri wa Kilimo Dkt. Charles Tizeba amesitisha mkataba wa Mkurugenzi Mkuu wa bodi ya Korosho nchini kwa kile alichokisema haridhishwi na mwenendo na utendaji kazi wa Mkurugenzi Mkuu huyo na kusema muda wowote atatangazwa atakaye kaimu nafasi hiyo.
#Habari:Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa mkoa wa Mwanza, imewafikisha Mahakamani waliokuwa viongozi wa Chama Kikuu cha Ushirika mkoani humo, Nyanza kwa tuhuma za kukisababishia chama hicho hasara ya zaidi ya shilingi Milioni 400.
#Habari:Polisi mkoani Pwani limewaua watu wanne wanaosadikiwa kuwa ni Majambazi na kumjeruhi mmoja ambaye alifanikiwa kukimbia katika mapambano ya kurushiana risasi baada ya kuwadhibiti katika tukio la uvamizi wa nyumba ya Mhasibu wa kikundi cha akinamama cha VICOBA Ushelisheli.
#Habari:Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa amewataka wanasiasa wajiepusha na tabia ya kuingiza siasa katika suala la kuwaondoa wananchi waishio mabondeni kwa kuwa jambo hilo linafanywa kwa maslahi ya wananchi wenyewe
#Habari:Zaidi ya watu 200 wamekwama kwa siku 4 baada ya Magari waliokuwa wakisafiria yakiwemo ya abiria na ya mizigo yanayotoka mkoani Mbeya kuelekea Tabora kukwama katika eneo la Msuwa wilayani Sikonge mkoani Tabora kutokana na Daraja kusombwa na maji ya mvua zinazonyesha.
#Habari:Askari na maofisa wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wanaoshiriki ulinzi wa amani nchini Sudan wametunukiwa nishani ya umoja wa mataifa na kutakiwa kulinda heshima na sifa nzuri ya jeshi hilo kitaifa na kimataifa .