Ukiwa huna shughuli ya kufanya na muda wako, ni rahisi mno kutaka kuutumia muda huo kwenye maisha ya wenzako, ambao nao wanaweza kuwa na muda na mambo yao mengine. Usiwalaumu kuwa wanajitia wako bize, ni kwamba muda wao wa kutumia na wewe unapishana na wako. Tuwe tunaomba miadi!
Kila mtoto ana Baba yake, awe mzuri au mbaya, mwema ama katili, tajiri ama maskini. Hatupewi fursa ya kufanya usaili wa baba na kumchagua tunayemtaka. Baba uliyepewa ndio Baba uliyepimiwa na uliyetunukiwa. Baba yako ni mtihani wako. Inategemea tu na unaupokeaje! #FathersDay2021
Polisi nchini wamefanya operesheni maalum ijulikanayo kwa jina 'Operesheni Wami' ikishirikisha Mikoa minne ya Tanga, Pwani, Morogoro na Mkoa wa Kipolisi Kinondoni kwa muda wa siku 45, wamekamata malighafi za kutengeneza pesa bandia, magari 4 na pikipiki 7, silaha, ngโombe 132 n.k