Leo, Ikulu jijini Dar es Salaam, nimempokea Rais wa Jamhuri ya Rwanda, Mheshimiwa Paul Kagame, aliyewasili nchini kwa ziara ya kikazi ya siku moja.
Tanzania na Rwanda si tu ndugu na majirani, bali pia ni washirika wa kimkakati wenye uhusiano unaoendelea kukua kwa kasi. Takribani asilimia 70 ya shehena ya Rwanda inapitia katika bandari za Tanzania. Biashara kati ya nchi zetu mbili imefikia shilingi bilioni 644 mwaka 2025, na uwekezaji kutoka pande zote mbili unaendelea kuchochea ajira na ukuaji wa uchumi kwa wananchi wetu.
Katika mazungumzo yetu, tumekubaliana kuongeza kasi ya ushirikiano kwa kuondoa vikwazo visivyo vya kikodi, kuimarisha biashara na uwekezaji, na kuwekeza zaidi katika miundombinu ya usafiri na usafirishaji, mawasiliano, pamoja na nishati ya uhakika. Aidha, tutaimarisha ushirikiano katika masuala ya ulinzi, usalama na ajenda za kikanda na kimataifa.
Karibu tena Tanzania, Mheshimiwa Rais.
Not every strong feeling is the Holy Spirit. God’s Spirit doesn’t confuse you, and doesn't contradict His Word. He brings peace, clarity, and truth. If you’re unsure about a decision right now, slow down and pray. Open Scripture. Ask God to lead you, and trust that He will.
Shukrani kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu na mwingi wa rehema kwa kunijalia kuifikia siku nyingine ya kumbukizi ya kuzaliwa na umri wa miaka 66. Kwa moyo wa dhati, nimepokea na ninawashukuru nyote kwa salamu zenu za upendo.
Nimesherehekea siku hii kwa kupanda miti. Wito wangu kwenu, tujenge na tuendeleze utamaduni wa kupanda miti na kutunza mazingira ili nayo yaendelee kututunza sisi na vizazi vijavyo.
Ninawatakia nyote kheri katika maadhimisho ya Miaka 62 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar. Kwa miaka 62 tumeendeleza dhamira ya msingi ya Mapinduzi ya kujenga jamii ya watu huru, yenye utu, yenye maendeleo, umoja, haki, amani na mshikamano.
Sote tunao wajibu wa kuendelea kuzilinda tunu hizi na kuzirithisha kwa vizazi vijavyo, kama tulivyorithi toka kwa waasisi wetu.
Wataalam wa Sheria kutoka Wizara ya Katiba na Sheria wakiendelea kutoa huduma ya elimu ya Sheria kupitia Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia (MSLAC) kwa wananchi wa Kijiji Cha Ngadinda, Halmashauri ya Madaba leo Mei 12, 2025
Dear Heavenly Father,
No matter the enemy's plan this Tuesday, help us rise above it. Forgive us for the ways we complain about life circumstances, take away what weighs heavy on our hearts and help us overcome every storm with confidence. Guide and bless us now and always. We pray this In Jesus' Name. Amen! 🙏
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Jaji Joseph Sinde Warioba mara baada ya mazungumzo yao, Ikulu Jijini Dar es Salaam, tarehe 17 Desemba, 2025.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wakuu wa Kamandi, Wakuu wa Matawi na Makamanda wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kabla ya kufungua mkutano wa 9 wa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Makamanda uliofanyika katika Shule ya Kijeshi ya Ulinzi wa Anga (SKUA) mkoani Tanga tarehe 15 Desemba 2025.
Matukio mbalimbali wakati wa mkutano wa 9 wa CDF na Makamanda uliofanyika katika Shule ya Kijeshi ya Ulinzi wa Anga (SKUA) mkoani Tanga. Mkutano huo wa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Makamanda ulifunguliwa na rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, tarehe 15 Desemba 2025.