Ukitaka kufanya mabadiliko kwenye Dunia fanya hivyo wakati huna familia maana ukishapata familia hutaweza kubadilisha hata Chaneli ya Runinga (TV) 😂.
Haka kamsemo ni kama cha masikhara ila kana maana.
#Thread
Kupata mteja mpya ni kazi rahisi kuliko kumfanya aendelee kuwa mteja wako milele.
Anachohitaji mteja mpya ni Matangazo na ushawishi kwenye watu wanaomzunguka.
Lakini kumfanya abaki na endelee kuwa mteja, kunahitaji umtengenezee imani iliyotukuka zaidi ya matangazo.
Sio kila mvumilivu hula mbivu, wengine wamevumilia mpaka maisha yao yakaharibika, wengine ikafika mahali wakapata maradhi au kujitoa uhai, kuna visivyo vumilika angalia unaweza jitoa kishujaa kumbe unajitoa kitoweo, kisicho kuuwa kinaweza kika kuvunja na sio kukukomaza kiaskari