Tuliwashauri kesi ni ya kisiasa, tulizeni mafuvu yenu kesi iishe kisiasa, lakini Lissu na kagenge kake kwa ujinga wao wakadanganyana ati yeye sio FAM, ili baada ya kesi aibuke kama shujaa wa Dunia. Walichosahau ni kwamba, hakunaga shujaa mwenye UHAI. Mashujaa wote walisha kufa.🤣
MAJUKUMU YA CHAMA CHA WANASHERIA TANGANYIKA #TLS @TanganyikaLawSociety
Kifungu cha 4 cha Tanganyika Law Society Act kinaeleza madhumuni ya kuanzishwa kwa TLS. Haya ndiyo majukumu yake na mantiki ya kila jukumu:
1. Kifungu cha 4(a): Kulinda na kuboresha viwango vya maadili na elimu ya taaluma ya sheria.
Mantiki: Kuhakikisha mawakili wanazingatia maadili ya taaluma, wanaongeza ujuzi na kutoa huduma za kisheria zenye ubora.
2. Kifungu cha 4(b): Kuwezesha upatikanaji wa maarifa ya kisheria kwa wanataaluma ya sheria na watu wengine.
Mantiki: Kuendeleza elimu ya sheria, mafunzo na uelewa wa sheria ili wanataaluma na wananchi waweze kuitumia sheria kwa usahihi.
3. Kifungu cha 4(c): Kusaidia Serikali, Bunge na Mahakama katika masuala yanayohusu utungaji wa sheria, usimamizi wa sheria na utekelezaji wa sheria nchini.
Mantiki: Kutoa mchango wa kitaalamu katika maboresho ya sheria na mifumo ya utoaji haki ili sheria ziwe bora na utekelezaji wake uimarishwe.
4. Kifungu cha 4(d): Kuwakilisha, kulinda na kusaidia wanataaluma ya sheria kuhusu mazingira ya utendaji wao wa kazi na masuala mengine yanayowahusu.
Mantiki: Kulinda maslahi halali ya mawakili na kuwezesha wafanye kazi zao bila vikwazo visivyo halali, vitisho au kuingiliwa isivyofaa.
5. Kifungu cha 4(e): Kulinda na kusaidia umma katika masuala yote yanayohusu sheria au yanayohusiana nayo.
Mantiki: Kuhakikisha wananchi wanapata msaada wa kisheria, wanalindwa dhidi ya ukiukwaji wa haki na wanapata fursa ya kudai haki zao kwa mujibu wa sheria.
6. Kifungu cha 4(f): Kupata, kumiliki, kuendeleza au kuuza mali za aina mbalimbali, zinazohamishika au zisizohamishika, na kupata mtaji au mapato kutokana na mali hizo kwa ajili ya kutekeleza madhumuni ya TLS.
Mantiki: Kuiwezesha TLS kuwa na rasilimali na mali zinazosaidia kutekeleza majukumu yake na kuimarisha uwezo wake wa kifedha.
7. Kifungu cha 4(g): Kukusanya au kukopa fedha kwa ajili ya kutekeleza madhumuni ya TLS, kwa njia na kwa dhamana zitakazoamuliwa na Chama.
Mantiki: Kuiwezesha TLS kupata fedha za kuendesha shughuli zake na kutekeleza mipango yake kwa kuzingatia taratibu husika.
8. Kifungu cha 4(h): Kuwekeza na kusimamia fedha za TLS ambazo hazihitajiki kutumika mara moja, kwa namna itakayoamuliwa na Chama.
Mantiki: Kuhakikisha fedha za TLS zinatumika kwa busara, zinalindwa na zinaweza kuleta manufaa ya kifedha kwa taasisi.
9. Kifungu cha 4(i): Kufanya mambo mengine yote yanayohusiana na au yanayochangia kufikiwa kwa madhumuni yaliyotajwa hapo juu.
Mantiki: Kuiwezesha TLS kutekeleza shughuli nyingine halali zinazohitajika ili kufanikisha majukumu yake ya msingi.
Kifungu cha 4 kinaweka msingi wa uwepo na wajibu wa TLS. Kinaonyesha kuwa TLS si taasisi ya maslahi ya mawakili pekee, bali pia ina wajibu kwa taaluma ya sheria, Serikali, Bunge, Mahakama na wananchi kwa ujumla.
Utekelezaji wa majukumu haya unapaswa kuongozwa na sheria, weledi, uwajibikaji na maslahi ya umma.
UKWELI,HAKI NA UWAJIBIKAJI VITALIPONYA
#UKWELI#HAKI#UWAJIBIKAJI#
@mangekimambi@TunduALissu Asante sana sister umeeleza vyema
Kwa kweli mi niko overwhelmed hata kueleza natoa highlights tu!
Umesema vyema tumemwangusha Lissu na kwa sasa tusipopambana nchi imekwenda hii!
We need to fight like HELL!
KIMENUKAAAAAAAAA, naomba mniruhusu nilale, nikiamka na drop watoto shule then drop 💣 .
Video itakuwa hewani saa 1 usiku ya Tanzania. Yani saa 1 usiku fanyeni ku refresh page…..
ISHU NI DIPU!!!!!
MUSIOGOPE!
Yesu ninayemwamini ndiye Njia, Kweli na Uzima. Taifa letu linahitaji UKWELI, HAKI NA UWAJIBIKAJI.
Amani ya kweli haipatikani kwa kuua, kutisha au kutumia vibaya mamlaka ili kumnyamazisha Boniface Mwabukusi. Amani ya kweli hujengwa kwa kutenda haki, kuheshimu utu na kuwajibika kwa matendo yetu.
Kwangu mimi, kuishi ni Kristo, na kufa ni faida. Ni bora nikose vyote, lakini nibaki upande wa wanyonge wanaonyanyaswa, wanaodhulumiwa na kupuuzwa katika harakati za kutafuta haki.
Mungu ninayemtumikia ni Mungu wa haki. Hata tukipita tena na tena katika bonde la uvuli wa mauti, sitaogopa mabaya, kwa maana najua kuwa makusudi ya Mungu yatasimama.
MUSIOGOPE! Ukweli unaweza kucheleweshwa, haki inaweza kuzuiwa, na sauti ya mtu inaweza kutaka kunyamazishwa, lakini hakuna mamlaka ya mwanadamu inayoweza kuishinda kweli ya Mungu.
Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.” — Mathayo 6:33
UKWELI. HAKI. UWAJIBIKAJI.
Mungu mbele, hofu nyuma, na haki daima!
HAKI ITASHINDA.
BAK MWABUKUSI .
Kama baada ya serikali haram kuwekeza mabilioni ya fedha na kushirikiana na ma influencer wa instagram wameshindwa kukusanya hata Watanzania elfu 5 siku ya leo basi naomba niseme hivi,
HONGERENI WATANZANIA, LEO MMETUTIA MOYO…..
VIDEO:
Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu akiingia mahakamani kwa ajili ya kusikiliza hukumu ya kesi ya kikatiba juu ya haki za Mawakili wake kumuona na kuzungumza nae kwa usiri akiwa Gerezani.
Hukumu hiyo itatoelewa katika Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo ya Dar es Salaam na Jopo la Majaji watatu wakiongozwa Jaji Amir Mruma.
Ni aibu kiasi gani kuwa wakili kwenye nchi ambayo Jaji ambaye ni M/kiti wa Kamati ya Maadili ya Mawakili, Naibu Mwanasheria Mkuu na Mwanasheria Mkuu wanakuwa wa kwanza kudharau amri za Mahakama?
Hii ni Kamati ya maadili isiyo na maadili?
Yote ni kumvua Mwabukusi Urais wa TLS!
Hii nchi haiji kutulia kamwe. Na haya mambo ya KUTISHANA hayaturudishi nyuma kamwe.
Asanteni TLS kusimama bila woga kupambana n WAKOLONI WEUSI. Ushindi unakuja.🙏
KIMENUKAAAAAAAAA, naomba niingie kulala, ila nikiamka na ku-drop watoto shule na drop 💣 moja kali.
Video itakuwa hewani saa 1 usiku ya Tanzania.
ISSUE NI DIPU!!!!!
Jamani eh! Huko ndani si kwamba sijaona message zenu kuwa hamjalipwa - ni kwamba #MO29 msiwe sehemu ya dhulma!
Nyie msiandamane kama waoga ila msikubali kutumika kutisha wananchi au kutuumiza!
Mgomo baridi pia ni sehemu ya harakati
Nadhani mmenielewa
Sasa tupambane let’s make this happen 👊🏽
Huko ndani wamevurugana!
Achaneni na mambo ya nani ana influence na mazagazaga - wanataka tuwape nafasi ya kupumua!
Hawa bado kidogo wanaanguka hawa 👏🏽😂
#TutaelewanaTu mwaka huu!