“If you’ve ever felt ‘not yourself’ — this is for you.
DID isn’t rare. It’s hidden in plain sight.
Share if you know someone who needs this. ”
#DIDAwareness
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 283
Wote wameongeza mambo kwa mdomo ambayo kwenye maandishi hayapo kabisa. Wameongeza yasiyokuwemo kwenye maelezo yao.
Ni ushahidi wangu kwamba ushahidi wa maneno unaotofautiana na ushahidi wa maandishi kwenye jambo hilo hilo ni ushahidi usioaminika.
Ndio kusema ushahidi wote wa mashahidi wote wa upande wa mashitaka hauaminiki.
PW1,2,3,6,9,12 and 16 hawa wote ni mapolisi na waliandika maelezo polisi wenyewe na wakajikanya wenyewe na kujishuhudia wenyewe. Niliwauliza ni sheria gani iliwaruhusu wafanye hivi wakadai ndivyo huwa wanafanya mapolisi.
Sasa ni ushahidi wangu kuwa Mapolisi wanafanya mambo kienyeji na vielelezo D1,2,5,8,12 wote walijaindika ni polisi mmoja tu ndio aliandikwa na polisi mwenzake kwa mashahidi wote walioletwa na Jamhuri.
Waheshimiwa Majaji wale Mapolisi wa Ruvuma waliandikwa na mapolisi wengine lakini hawakuletwa. Wangewaleta njngewathibitishia kuwa maelezo yao yaliandikwa kwa usahihi.
Kwahiyo ushahidi wangu ni huo. Nimemaliza ingawa nimevuta vuta kidogo. Majaji wanaandika.
Jaji Ndunguru: Sasa hawa ambao hawajaletwa mahakamani unasemaje sasa?
Mhe. Lissu : Wangeletwa tungethibitisha taratibu za kuandika maelezo huwa ukoje. Kwahiyo ni ushahidi unreliable huu unatakiwa kwa kesi kubwa kama hii.
Ajuaye Wakili wa Serikali anasema tunaomba health break kabla ya kuanza cross exanination.
Naomba repost yako.
Mwenyekiti Lissu ameniambia leo, Siasa za Udalali zinapaswa kupingwa sirini na hadharani. Anasema yeyote anayezifanya hawezi kuwa rafiki yake. Amenionya mimi na Vijana wote wa CHADEMA kuwa tusiwe Madalali kwenye Siasa. Nimemuelewa na BAVICHA tutasimama hilo kwa wivu Mkubwa.
#Tanzania activist @mangekimambi is suing @Meta over claims it silenced her US accounts at Dodoma's request. As I tell @Sheriffb, a win in court would prove 'the government made us do it' isn't a shield, it's an admission that platforms cave to autocrats.
https://t.co/SSB8tzBoFB
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 282
Mhe. anaendelea hapa.
Anasema hawa PW1, 2 na 16 niliwaonesha vifungu vya kanuni ya adhabu na sheria ya vyombo vya habari kuhusu sio uchochezi wala sio kosa kuonesha mapungufu ya serikali na kuipinga serikali na wao walikiri na kusema ndio sio makosa. Nilifanya kazi hiyo na wao walikiri kuwa sio makosa.
Nikwaambia ni wapi walizingatia vifungu hivyo wakati wa upelelezi wao wakasema hawana na lakusema kuhusu mambo hayo.
PGO 1(24) nguzo kuu ni presumption of inocence niliwauliza walinitreat wapi kwamba sina hatia wakati wote waliokaa na mimi? Hakuna walipozingatia hilo kabisa. Walikuwa wanajiendea tu. Walishaniona nina tuhuma tayari na muhaini.
Tar. 04/04 ndio waliona video yaani PW1 na PW 2 yaani PW 1 alimpelekea PW 2akamuonesha vipande vipande. Na siku hiyo hiyo akaamuru kuonesha jalada lifunguliwe. Akaaamuru jalada lifunguliwe.
Kwahiyo hakukuwa na presumption of innocence kwamba Lissu ametenda uhaini siku hiyo hiyo waliamua hivyo.
PW 16 Amin Mahamba anasema na yeye alipotizama akaona uhaini hakukuwa na presumption of innocence ndio maana hawakutaka kupata ushauri wa DPP wala washauri wa kisheria wa Serikali.
Na kwa vile walikuwa na Majibu tayari ndio maana waliulizwa mliwatafuta Viongozi wa Chadema muwaulize? Wakajibu HAPANA.
Je mlinitafuta Mimi Lissu mwenyewe mniulize nilikuwa na maana gani? Wakasema HAPANA.
Kwahiyo nasema kwamba hawakunitafuta kwasababu walishaona tayari wana mkosaji.
Ndio maana hata walipoletewa na ushahidi wa PW 17 yule wa JAMBO. Yeye anasema ndie aliyechapisha na kusambaza na hakuona uhaini. Maelezo ya P hayakuwa na maana tena kwao.
Wao majibu yao walikuwa nayo kabisa.
Nilimuuliza Amin Mahamba kuwa Insp. Andrew Churu ulisoma maelezo yake aliyosema kuwa ni P ndio alichapisha na kusambaza? Huyu Amin Mahamba hakuna na lakusema kwasababu walifanya kazi hii wakiamini mimi ni muhaini kabla ya lolote.
Pia, niliwauliza juu ya matakwa ya PGO No. 1(25) inayowaambia kuwa makosa ni yale yaliyopo kwenye sheria na sio vinginevyo.
Wakajibu ni kweli. Nikawauliza someni kifungu nilichoshitakiwa nacho kuhusu kosa nikiloshtakiwa nalo kama kwenye hicho kifungu kuna habari ya kuzuia uchaguzi, kuhamasisha watu kuzuia uchaguzi nayo? Ibara ya 151(1) kuhusu serikali kwamba niliitishia serikali kweli?
Yote hayo wakasema hawajui na hakuna kosa nimelifanya kwenye hayo. Wakasema hakuna nilichofanya kuitishia serikali.
Yuko speed majaji wanasema unaenda kasi sana tunashindwa kuandika.
Ni ushahidi wangu kwamba hiyo Executive wanayosema niliitishia yaani serikali maana yake nilimtishia Rais, Vice President, Ministers na Deputy Ministers, Inaweza kuwa RC na Ma DC hao wote ni Executive. Wakurugenzi wa Wilaya na manispaa wanaitwa District Executive Directors (DED) hata majina yao wanaitwa Executive.
Exevutive of the United Republic wanaweza kuwa ma VEO au WEO yaani Village Executive officer na Ward Executive Officer wote hao ni Executive.
Na Executive wanaweza kuwa watu wowote waajiriwa wa serikali isipokuwa Mahakama na Bunge. Kwahiyo kifungu cha 39(2) cha Penal Code hakitekelezeki hakuna atakayepona na hawawezi kuithibitisha.
Kwamba hawajasema kati ya hao kuanzia Rais hadi mtendaji wa kijiji na mtaaa ambao wote ni Serikali nilimtisha nani kati yao? Kifungu hicho kilichotungwa wakati wa Grey Likungu Mataka wakati wa utawala wa Chama kimoja hakifai tena kuwa sehemu ya sheria zetu.
Naona Katuga anahangaika kwenye kiti kuwa Mhe. Lissu anafanya nini? Hii ni Mahakama ya Kikatiba kweli hadi aseme kifungu hakifai kuwepo? 😂 haelewi mchezo uliopo hapa.
Waheshimiwa majaji hakuna shahidi hata mmoja amesema nia yangu ya kuitishia serikali ilitekelezeka hata mmoja.
Hakuna aliyesema kuwa serikali iliogopa sana siku hiyo. Hakuna aliyesema IKULU HAKUKUKALIKA siku hiyo.
Part 283 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Leo Agosti 26, 2026
Last time tuliishia part 276 so leo tunaendelea na -;
Part 277
Mwenyekiti ameingia tayari Mahakamani akiwa vibe.
Amesema naona wameanza kunyoana wenyewe.
Watu 😂😂😂
Amewaona akina Mzee Lwaitama na Jenerali Ulimwengu anasema nyie Wazee hamjakata moto kama wale wazee wengine.
Amemuona Makamu Mwenyekiti Heche anasema Makamu ongeza kupeleka moto.
Tunawaona mashahidi watatu wa Mh. Lissu wapo hapa Mahakamani, John Heche, John Mnyika na Amani Golugwa.
Majaji wameingia tayari muda huu. Na wakati anaingia watu walikuwa wanaimba mtetezi wa wanyonge kwa sauti na kwa vibe.
Nimemuona anaongea na Mwenyekiti wa Bavicha Taifa Wakilli Mahinyila anamuuliza mmeshaandaa mashahidi tayari. Anamjibu kitu anasema haya leo tutamaliza hakuna shida.
Inapigwa high court
Wanaingia Majaji na kukaa sehemu yao.
Anasimama karani Criminal session No. 19605 Jamhuri dhidi ya Lissu.
Anasimama Ajuaye Zengeli wakili wa serikali yupo na Katuga, Job Mrema, Ignas Mwinuka, Thawabu Issa, Cathbert Mbiringe na Winiwa Kasawa kikundi chote kinaiwakilisha Jamhuri na Lissu yupo anajiwakilisha mwenyewe.
Waheshimiwa majaji na mimi niko tayari anajibu Lissu. Na mashahidi wangu wako humu naomba watoke ila wasikae mbali.
Majaji wanateta na kucheka kidogo. Makamu Heche, Mnyika, Golugwa na Brenda wanatoka zao nje.
Watu wanajiset kwenye viti vyao hapo wanakaaa.
Majaji wanateta kidogo kisha wanasema tuendeleee.
Mhe. Lissu anasema haitakuwa vibaya mkinikumbusha nilipoishia.
Jaji Ndunguru pale ulipomtaja Askofu Pissa.
Mhe. Lissu sasa leo nataka nijikite kwenye kesi kama ilivyowasilishwa kwenu na Upande wa Mashitaka. Ushahidi wao walivyouleta, Waheshimiwa Majaji naomba niseme utangulizi ufuatao:
1. Mashahidi walioletwa mbele yenu ni mashahidi wa aina gani na ushahidi wao unapaswa upewe uzito wa aina gani?
2. La pili nitazungumzia ushahidi wenyewe. Ushahidi uliotolewa na mashahidi hawa. Na nitaonesha hakuna kosa la Uhaini na hakuna kosa lolote la jinai kwahiyo hayo ndo mawili ya utangulizi.
Sasa nianze na la kwanza kuhusu hao mashahidi.
Wakati wa Preliminary hearing upande wa mashitaka ulileta orodha ya mashahidi 30. Ambao walisema hao ndio wataleta ushahidi wa kuthibitisha tuhuma za uhaini dhidi yangu.
Upande wa mashitaka haukuleta mashahidi wote hao 30 badala yake walileta mashahidi 17 peke yake.
Hao 13 ambao hawakuletwa, hawakuletwa kwasababu muhimu fulani na nitazisema.
Hiyo ommission ya hao mashahidi 13 is neither insignificant nore without importance.
Sio kwasababu hawana maana na sio kwasababu hawana umuhimu.
Nianze na ambao waliletwa.
Katika mashahidi 17 walioletwa. Mashahidi 8 ni askari Polisi.
Mashahidi 9 waliobaki ni mashahidi wa kificho.
Mahakama haiwafahamu majina yao. Haiwafahamu kabisa, haifahamu wanaishi wapi? Haifahamu wanafanya kazi gani na haifahamu chochote zaidi ya majina ya P, P1, P2 P nini huko.
Inaweza kuwa tumekuwa nao throughout hapa kesi ikiwa inaendelea kwasababu Mahakama haiwajui na upande wa utetezi hauwajui hata kidogo.
Kwahiyo ushahidi wa hao mashahidi 9 ni ushahidi wa watu wasiojulikana na Mahakama wala utetezi, Watu pekeee wanaowajua ni waendesha mashitaka waliowaleta.
Part 278 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
Hati ya mashtaka imetaja Lissu alitaka KUZUIA UCHAGUZI & KUKINUKISHA. Haya maneno ni (subject to interpretation) yanaweza kuwa na maana yoyote ile kutokana na mtu anavyoelewa. Lissu amewaambia majaji kuwa, aliletwa tu mahakamani pasipo wao (polisi) kumuuliza maana ya maneno hayo. Kwahiyo, Lissu yuko gerezani kwa sababu ya TAFSIRI binafsi ya Jeshi la Polisi.
Kupitia Katiba ya nchi, Sheria ya Uchaguzi, PENAL CODE & Kamusi ya Kiswahili, Lissu tayari ameshathibitisha mbele ya mahakama kuwa haya maneno yanayoitwa makosa ya jinai, hayajaandikwa kwenye kitabu au sheria zote hizi tajwa & pia hayapo kwenye sheria zote za Tanzania.
DPP kwa upande wake, ameshindwa kuleta ushahidi wa TAFSIRI ya maneno hayo kuthibitisha tuhuma dhidi ya Lissu. Hii hati ya mashtaka ina nguvu kubwa kuamua kesi hii.
The principle of legality ile Kanuni ya No crime without law (nullum crimen sine lege), yaani ili kitendo kiwe kosa ni lazima kitendo hiko kitajwe kwenye sheria kuwa ni kosa la jinai. Sula hili liwe ni muhimu kuzingatiwa na mahakama.
Limitations of common law crimes inakataza majaji kutengeneza kosa isipokuwa Bunge. Hili nalo lizingatiwe.
Tuendelee kujifunza...
Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam.
Tupo tayari kuendelea na usikilizaji wa utetezi wa Mwenyekiti wetu, Tundu A.M. Lissu. Baada ya kukamilisha msingi wa ushahidi wa tabia yake njema (good character), Tundu Lissu ataelekeza hoja zake kwenye hati ya mashtaka ili kuonyesha kutokuwepo kwa kosa lolote la jinai linalokidhi vigezo vya uhaini. #FreeTunduLissu
Leo nchi ITAFURAHI kutokana na kitakachotokea MAHAKAMANI. Hata kama FURAHA itakuja kwa KUCHELEWA, ni MUHIMU SANA kutambua kwamba; FURAHA hiyo ITAIPONYA nchi kwa wakati huu.
Nchimbi hakuomba radhi na/au kuwapa pole Watanzania kwa serikali yao kuuwa maelfu, kutesa, kupoteza na kuwapa kesi za uongo.
Mamlaka ilikuwa muhimu kwake vs our collective good.
Leo ni victim wa mfumo alioulea, hana hakika na usalama wake.
A good road is good for all of us!
Tz mainstream media so afraid of reporting news of Nchimbi's resignation even as speculation.
Yet another reminder that Tz mainstream media are a bunch of cowards and self-censoring pimbiz hiding under 'ethical guidelines & maadili' .
Basically too scared