Salamu za mwaka mpya wa 2024, toka kwa Mwl Christopher Mwakasege.
Na Malengo 5 ya kuwa nayo katika Mwaka 2024
Nilipokuwa ninaiombea tarehe 1 Januari 2024, hasa juu ya watu wa Mungu kuweka malengo ya mwaka. Kuna ujumbe ambao Mungu aliniwekea moyoni, ambao nataka nikushirikishe hapa kwa muhtasari tu.
Ujumbe huo ulihusu aina ya malengo, ambayo watu wake wengi, wanasahau kuyaweka kama malengo.
Wengi wao huwa wanaweka kama ajenda za maombi, lakini si kama malengo ya kuyaombea na kuyatekeleza, ili Mungu awasaidie katika kuyatekeleza.
Malengo yoyote yasiyo na mikakati ya kuyatekeleza, hata ukiyaombea, inakuwa vigumu kuyatekeleza, na kuyafuatilia kiutekelezaji.
Ndio maana Mungu akikupa “wazo” la kufanya, ujue anao mkakati anaotaka uutumie kulitekeleza wazo hilo. Neno linalotumika zaidi kibiblia kuhusu mkakati, ni neno “njia”.
Mungu anasema katika Isaya 55:8, 9; juu ya utofauti uliopo juu ya mawazo yake juu yetu, na utofauti wa njia zake au mikakati yake ya kutekelezea mawazo aliyonayo juu yetu.
Kila wazo lina mkakati wake wa kulitekeleza. Vivyo hivyo na malengo. Kila lengo lina mkakati wake wa kulitekeleza. Kwa hiyo, wazo la Mungu lina malengo na mikakati ndani yake.
Ukijiwekea malengo ambayo hayaendani na mawazo ya Mungu, na mikakati ya Mungu kwa ajili yako, inakuwa si vyepesi kupata msaada stahiki toka kwa Mungu, kwa ajili ya kuyafanikisha.
Ndani ya ujumbe niliowekewa moyoni mwangu, ni kukuwekea msisitizo ya kuwa, katika malengo yako ya mwaka 2024, usiyasahau malengo mkakati yafuatayo:
LENGO MKAKATI LA 1:
Upate kumjua Mungu zaidi, sawasawa na Ayubu 22:21.
Mstari huu wa Biblia unasema hivi: “Mjue sana Mungu, ili uwe na amani; ndivyo mema yatakavyokujia”. Ukitaka kuona mema aliyokupangia (Yeremia 29:11), kwa mwaka 2024 yanakujia, basi weka lengo hili na mikakati yake husika, kuhusu kumjua Mungu zaidi, ili uwe na amani.
LENGO MKAKATI LA 2:
Umzalie Mungu matunda, ambayo atayatumia kuwagusa wasiomjua, ili wapate kumjua, sawasawa na Ufunuo wa Yohana 22:2.
Mstari huu unazungumzia juu ya “Mti wa uzima, uzaao matunda, aina kumi na mbili,wenye kutoa matunda yake kila mwezi; na majani ya mti huo ni ya kuwaponya mataifa”. Hii ina maana tuwe na lengo la kumzalia matunda kimkakati!
Yesu anapokuwa “mti” wa uzima, tuliookoka tunakuwa “tawi” lake la uzima! Tunatakiwa tumzalie matunda, kwa msaada wa uzima wake, aliouweka ndani yetu.
Leo, Yesu anatukumbusha ya kwamba hatukujichagua kuingia mwaka 2024, bali ni yeye aliyetuchagua sisi. Na lengo mojawapo la kutuingiza mwaka 2024, ni ili tumzalie matunda, na matunda hayo yapate kukaa (Yohana 15:16).
LENGO MKAKATI LA 3:
Uweze kuomba kwa mfululizo kwa lisaa limoja, angalau mara moja au zaidi kwa wiki, sawasawa na Mathayo 26:40, 41.
Yesu anauliza kwenye mstari huu swali hili: “Je! Hamkuweza kukesha pamoja nami hata saa moja? Kesheni, muombe, msije mkaingia majaribuni; roho i radhi, lakini mwili ni dhaifu.”
Yesu anataka tujue, msaada tunaoupata tunapoomba kwa muda mrefu kwa mfululizo, wa kutusaidia kushinda upinzani dhidi ya mwombaji kutengenezewa mazingira ya kukishinda, kile kinachomzuia asiyafanye mapenzi ya Mungu.
Soma na kutafakari habari hii ya Mathayo 26:36 – 46, inayotujulisha jinsi maombi ya muda mrefu yalivyomsaidia Yesu, kuivunja nguvu ya mwili iliyokuwa inafanya roho yake iombe kikombe kimwepuke.
LENGO MKAKATI LA 4:
Jiwekee lengo kimkakati la kuweka akiba ya kutosha, uweze kupambana na upungufu wa pesa, katika eneo ambalo mwaka 2023, lilikusumbua kwa upungufu wa pesa za matumizi, sawasawa na Mithali 6:6 – 11.
Mistari hii ya Mithali 6:1 – 11, inaweka msisitizo wa mtu kushinda uzito moyoni, ambao watu wengi wanakuwa nao, wa kushindwa kuweka mikakati endelevu ya kuweka akiba.
Kumbuka ya kuwa, akiba ni jambo mojawapo muhimu linalokusaidia kuweka akiba ya kukidhi mahitaji yako ya wakati ujao.
LENGO MKAKATI LA 5:
Jiwekee lengo mkakati la kuilinda imani ndani yako, inayobeba amana uliyokabidhiwa na Mungu kwa njia ya Roho Mtakatifu, sawasawa na 2 Timotheo 1: 14.
Soma hii kama Unataka Kubadili Maisha yako 🧠
Kila mtu anatamani maisha mazuri,
Shida inakuja kwenye kulipa gharama.
Repost Iwafikie Wana!
Wengi wanakosa nidhamu na kujiheshimu.
Wakitumwa wanafanya, Wakijituma hawafanyi.
Ziko njia nyingi za kufikia maisha unayoyataka.
Unaweza kurithi, wachache wana bahati.
Unaweza kufanya biashara haramu. Utafungwa
Pia unaweza kubaki ukiomba Mungu.
Ama ukaamua kuchukua sheria mkononi na kutengeneza maisha yako, na mwenyezi Mungu atakujaalia.
Njia sahihi ya kuyafikia maisha unayotaka ni:
Kuwekeza kwako na kuwa bora zaidi ya jana.
Jifunze ujuzi mpya utakaokusaidia kuingiza kipato.
Simaanishi Learning a skill,
Namaanisha Acquiring a skill,
Kuna utofauti mkubwa hapa...
Acquiring is more than Learning a skill.
Tatizo kubwa la mfumo wa elimu ni kuwafunza watu bila ku-acquire skills.
Yaani mtu anasoma Comp. Sc lakini hawezi kutengeneneza hata landing page.
Mtu anasoma lugha mpya lakini hawezi kuongea fluently hata kwa dakika moja tu.
Hii ni Learning na sio Skill Acquisition.
Skill Acquisition inahitaji:
Mazoezi . Mazoezi. Mazoezi.
Tena kwenye mazingira halisi.
Kama unajifunza Kichina hakikisha unapata sehemu za kuongea na Wchina wenyewe.
Kufanya mazoezi kwenye mazingira halisi until autonomous stage - Hapo uta-acquire skill.
Tutoke huko.
Jifunze tabia mpya zitakazokusaidia kuweza kuwa mtu bora:
Kuamka mapema.
.
Kuishi kwa malengo.
.
Acha kuamua kwa kutumia hisia.
.
Wajibika kwenye maisha yako.
.
Anzisha biashara mpya. Ingiza kipato.
.
Wekeza. Nunua hisa. Nunua vipande.
Nunua ardhi. Wekeza kwenye real estate.
.
Usikae tu kulalamika, do something.
.
Unapoweka malengo, jiheshimu na uyafate kikamilifu.
.
Kuwa na mwendelezo kwenye kile unafanya.
.
Sow-up kila siku. Italipa in the long run.
Acha tabia zinazokurudisha nyuma:
-Acha porn
-Acha betting
-Acha masturbation
-Acha kufanya fanya ngono
- Live more mindfully...
Kataa kuwa normal💪
Dunia sio ya watu wa kawaida.
Duniani ili uweze kufanikiwa lazima kufanya mambo yasiyo ya kawaida kwako.
-Lazima uanze kuwaza tofauti,
-uanze kuishi kwa kusudi,
-uanze kufuata njia yenye tumaini mbele yako.
Inawezekana.
Wewe ni #JeshiLAM2M1
Bookmark & Repost!
Ili kujifunza zaidi kwenye Bio Hacking, Personal Development na Expert Business:
FOLLOW ME: @millambo_
Join our Telegram Channel:
https://t.co/mB5Pj1PSsG
Subscribe to our YouTube:
https://t.co/RGJ3g44UFP
Kama Unafanya kazi SOMA hii⁉️
Utaokoa Maisha yako...🫡
Siku hizi kumekuwa na ongezeko la vifo vya ghafla kya vijana wengi (24-45).
Kwanini?
Kuna sababu nyingi lakini jambo la msingi tumepoteza dira ya maisha,
Focus kubwa ya vijana imekuwa kwenye mambo 2 makubwa:
1. Kusaka noti
2. Kuponda maisha
Zamani wazee wetu walidumu sana kutokana na lifestyle yao:
i. Kutafuta chakula kwa nguvu kubwa
ii. Kutembea na kukimbia umbali mrefu wakitafuta chakula (Mazoezi)
iii. Kula vyakula vya asili
iv. Kutokula kabisa bidhaa
➡️SASA SISI TUMEGHUBIKWA NA AINA MPYA YA MAISHA:
1. Kutafuta na Kusahau Afya
Watu wamewekeza nguvu kubwa kwenye kutafuta maisha kuliko kawaida.
Sio kitu kibaya kufanya kazi kwa bidii.
Mimi mwenyewe nafanya kazi kwa muda mrefu sana.
Suala la msingi, unatunzaje afya yako?
Mind you, unaweza kutafuta sana pesa ukiwa kijana na kuja kuitafuta sana afya ukiwa mzee.
Mimi ninaamini kwenye yote 2.
TUTAFUTE PESA NA HUKU TUKITUNZA AFYA ZETU.
2. Kula Hovyo bila Kujali Afya
Watu wengi hasa wanaofanya kazi za maofisini,
Hawali kwa makusudi,
Wamejaza sukari, milo, maziwa feki, jam, mayonnaise, margarine na bidhaa zingine ofisini mwao.
Mikate ndio vyakula visivyokatika ofisini.
Wakitoka kwenda kula: wanakula kuku wa kisasa, soda, energy, na junk food kama zote.
Kwa kifupi kula kwa afya sio kipaumbele kabisa.
Ni huzuni sana.
3. Kutokufanya Mazoezi
Kufanya mazoezi peke yake kuna kuepusha na magonjwa mengi sana.
Sasa watu wanatumia magari kwenda kazini,
Wanaamka na kwenda job bila kufanya mazoezi,
Wakitaka kwenda lunch wanatumia usafiri,
Wakiwa ofisni wanatumia lift kupanda juu,
Kwa kifupi miili imelemewa na mafuta na nyama uzembe.
Kwa namna hii utapata kila aina na madhara na udhaifu.
Miili haitumikishwi kabisa na,
Mwanadamu anakuwa imara anapokuwa na rapsha rapsha na mambo yanayofanya mwili usikae kizembe.
4. Kukaa kwa Muda Mrefu
Mwili wa mwanadamu kimuundo unatakiwa kuwa umesimama zaidi kuliko kukaa.
Ndo maana kuna changamoto nyingi sana za magonjwa zitokanazo na kukaa kwa muda mrefu.
Mwili wa mwanadamu unatakiwa kuwa na balance nzuri ya kukaa na kusimama.
Sasa unakaa kwenye usafiri kwenda kazini,
Kazini muda wote umekaa,
Ukienda lunch umekaa,
Ukirudi nyumbani kwenye usafiri umekaa,
Nyumbani unakaa.
Unadhani bawasiri utaikwepaje hapa?
Unadhani low back pain utaikosaje hapa?
Lazima tu utawindwa na magonjwa kadha wa kadha.
5. Kutokuwa na Vifaa Bora vya Kufanyia Kazi
Kwa watu wanaokaa kwa muda mrefu wanatakiwa
kuwa na viti maalum na meza za kufanyia kazi.
Unatakiwa kuwa na adjustable table,
Meza unayoweza kuitumia ukiwa umekaa na
ukichoka ukabadilisha ikawa ndefu ukasimama.
Na ukafanya kazi ukiwa umesimama.
Wapo wengi wana meza hizi lakini hawazitumii kikamilifu.
Kaka yangu @MalemboLE anayo hii meza na huwa anajitahidi kuitumia kikamilifu. Tujifunze.
Haya je tunatumia viti gani?
Watu wengi hawatumii vitu bora,
Vinavyoruhusu kukaa kwa muda mrefu ukiwa kwenye pozi sahihi.
Hivi ni baadhi tu ya vifaa vya muhimu zaidi kwa,
Utendaji kazi bora na kulinda afya zetu.
6. Stress za Mapenzi
Kumekuwa na chipuko kubwa la soy boys na simps kwa vijana wengi.
Wenye pesa na wasio na pesa. Mapenzi yanawanyanyasa.
Wenye pesa wanadhani wanastaihili kupendwa kwa sababu wanazo, huzuni!
Wasionazo wanadhani wanastahili kupendwa kwa sababu wanajipendekeza kupitiliza. Dah!
Wote ni maumivu tu.
Ku-survive mapenzi kwa dhama hizi unakuwa ujuzi adimu.
Unahitaji kujifunza kubalance shobo za mapenzi.
Lazima ujifunze kutokuwa simp na soy boy.
➡️Wanawake watakupenda na kukuheshimu ukionesha:
..Unayejali, linda, fikisha kunako, tunza, ongoza.
LAKINI, lazima uwe na:
..Sauti
..Mamlaka
..Uongozi
..Usiyetabirika
..Usiyekubali ujinga
HAYA YOTE UNATAKIWA KUBALANCE SHOBO.
7. Kutokufanya Kazi Unayopenda
Watu wengi wamekuwa na kawaida ya kufanya kazi zinazowaingizia pesa,
Bila kujali wanapenda au la.
Sibishi, kwa mazingira yetu wengi wanakuwa hawana uchaguzi na kuishia,
Kufanya kazi wasizozipenda ili tu mkono uende kinywani.
Tatizo ni kuwa haya maisha yana stress nyingi sana kuliko furaha ukiwa kazini.
Hawa ndio watu wanachukia zaidi Jumatatu na kufurahisi kila Ijumaa.
Maisha yao yote wanawaza kumaliza kazi na kuanza wikendi.
Ikifika Jumapili wanaanza mawazo kuwaza blue Monday.
Tofauti ni kuwa ukifanya kazi unayoipenda sana,
Unakuwa hujui tofauti ya kazi na kupumzika.
Unatamani kufanya kazi muda wote maana ni sehemu ya maisha yako.
Ukiweza, jitafute, wafanyie kazi kwa muda ukijitafuta - Siku moja amka ukiwa unaenda kufanya kazi unayopenda kutoka moyoni.
Na sio kukaa kwenye kazi unalaani kila siku,
Na maisha ya kazi yanachukua muda wetu mwingi wa hapa duniani.
Furaha yako imebaki kwenye kupokea mshahara tu.
You can do better.
Work on yourself more than you work on your job,
...Jim Rohn.
Bonus:
8. Kukosa balance ya maisha
9. Kunywa pombe na kupati kupitiliza
➡️MADHARA YA LIFESTYLE HII:
i. Kuugua mara kwa mara
ii. Kuwa umechoka muda wote
iii. Kukosa hamu ya chakula
iv. Kunenepa bila mpango
v. Kuotesha vitambi uchwara
vi. Bawasiri kushamiri
vii. Low back pain kuzidi
viii. Magonjwa ya moyo
ix. Kuongezeka kwa pressure na kisukari
x. Upungufu wa nguvu za kiume
xi. Kukosa furaha na maisha
xii. Stress zisizoisha
xiii. Na mengine mengi
➡️ NINI KIFANYIKE?
✅FIX maisha yako:
1. Kula vizuri
2. Fanya mazoezi (3-7 kwa wiki)
3. Kuwa mtu wa movements – Tumikisha mwili
4. Tumia vifaa bora kazini
5. Ondoa sukari, jam, margarine, mikate na bidhaa zote ofisini
6. Ongeza muda wa kutembea kwa miguu
7. Jifunze ku-survive mapenzi
8. Fanya unachopenda au penda unachofanya
9. Paki gari mbali na utembee
10. Ukiwa karibu na kazini nenda kwa miguu
11. Usitumie lift kupanda majengo
12. Ukiwa karibu na kazini nenda kwa miguu
13. Punguza kupati i.e pombe
Nakuamini sana kuliko unavyojiamini,
You brother
Millambo, R.
15-09-2023
Kimara Baruti, DSM.
#Tutoboewote
#Jeshilam2m1
Watu Wengi Hawajui Namna ya Kuweka MALENGO na Kufikia Ndoto zao.
Miaka 5 iliyopita, nilifanya maamuzi magumu ya KUJIKOMBOA.
Na huu ndio MSINGI Uliobadili maisha yangu.
Hii ni RATIBA YANGU YA SIKU, ukiweza kuifata Utajikomboa pia.
Retweet Wengi Wajifunze 🙏
🧵
JE UNAZITAMBUA HIZI USSD CODE NA KAZI ZAKE KWENYE SIMU YAKO
Kupitia Dial jaribu.
*31# (ondoa Caller ID)
Mtu unaempigai atoweza kukutambua kurudisha piga*31#
*#06# (Check the Device's IMEI)
Angalia IMEI number ya simu yako
*#67# (angalia Call Forwarding)
...🔄👇
Kwa miaka takribani 5 nimesoma na kujifunza mengi juu ya mafanikio na umasikini.
Nimebaini SABABU 10 zinazowafanya wachache kufanikiwa na wengi kuzidi kuwa masikini.
🧵
Repost Wengi Wajifunze!