Ningekuwa rais aisee watoto wa kike wasinge enda shule hasa elimu ya juu🙌 uhuru wa kuke chuoni na kuishi mbali na wazazi, na njaa unawafanya wanapotea sana
@SuluhuSamia Mhe Rais naendelea kushauri kwa dhati Tundu Lissu aachiwe huru kwani kesi haikamiliki. Hekima na busara iliyokufanya kutangaza sera ya 4Rs mara ulipoingia madarakani ikuongoze tena katika jambo hili. Simulizi hizi za kutisha za vyombo vya habari vya kimataifa, zinaibua hisia kali hasa kwa vijana, hata wazee tumekumbushwa kadhia ya operation Sogeza iliyounda vijiji vya ujamaa 1974 -1976. Taarifa hizi zinaathiri kikubwa taswira ya taifa letu na maslahi yake. Athari ni kubwa. Tutafute muafaka kupitia uwajibikaji na maridhiano. Tuwe na hofu ya Mungu na kutambua miujiza yake mfano wa risasi 16 kushindwa kukomesha uhai ingawa maumivu ni makubwa. Tutubu na kusali kuliombea taifa letu kila mtu kwa imani yake.
Nilichelewa sana kujua namna ya kula "healthy"
Nawatamania sana waliojua ishu za diet kitambo na wanaziishi kama sehemu ya maisha yao.
Huu mwaka nimewekeza kwenye AFYA yangu-moja ya kitu nilianza nacho ni DIET yangu izingatie Heathy na kupiga tizi back to back.
KILO 11 zimepotea mpaka sasa. Hii ni challenge ya mwaka mzima MUNGU akinipa kibari. 🙏
#HABARI Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa kushirikiana na kikosi kazi maalum cha kuzuia na kupambana na matumizi ya makosa ya kimtandao limewakamata Claudian Makaranga (28) mkazi Kawe na Hongliang Yang (35) Mchina, mkazi wa Kigamboni, kwa tuhuma za kuingiza vifaa vya mawasiliano ya intaneti nchini bila kufuata utaratibu wa kisheria vyenye jina la STARLINK KIT/DEVICE.
Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda maalum SACP Jumanne Muliro anasema Watuhumiwa hao wamekuwa wakijitangaza kuuza vifaa na kutoa huduma ya internet nchini kupitia mtandao ya kijamii wa Instagram kwa akaunti yenye jina la STARLINK.
Baadhi ya vifaa vilivyoingizwa nchini imebanika vilishauzwa na kutumika katika baadhi ya maeneo ya Dar es Salaam kitendo ambacho ni kosa na kinyume na sheria kwani havijaidhinishwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).
#EastAfricaTV
Kilichobaki nitafute hela niende vijijini huko ninunue eneo la ekari 3, niweke banda la kuishi, ninunue ng'ombe wa maziwa nianze ufugaji na kilimo.
Naona shule nilipoteza muda wangu.