Karibu sanaa mkoani Singida, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, hakika umetupa heshima kubwa Wananchi wa Singida katika maadhimisho haya ya Siku ya Wafanyakazi duniani (MEI MOSI).
Maandalizi ya kuelekea kwenye maadhimisho ya siku ya Wafanyakazi duniani (Mei Mosi) kwa mwaka huu 2025 yatafanyikia katiika uwanja wa Bombadia mkoani Singida, ambapo mgeni rasmi anatarajia kuwa Rais wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
πΈ @DalidaliR (@CloudsMediaLive)
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema ameridhishwa na Maandalizi kuelekea sherehe za siku ya wafanyakazi duniani zitakazofanyika kesho Mei mosi, 2025 kitaifa Mkoani Singida katika Uwanja wa Bombadia
Mahojiano na kipindi cha #Clouds360 (@CloudsMediaLive) kuelekea kwenye Siku ya Wafanyakazi duniani (Mei Mosi) ambayo kitaifa inafanyika mkoani kwetu Singida.
Karibuni sana SINGIDA
#kaziinaendelea
Nawashukuru nyote kwa salamu nyingi za kheri na upendo katika kumbukizi ya miaka minne ya Kiapo cha kuitumikia nchi yetu katika nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Tuungane pamoja kumuomba Mwenyezi Mungu aendelee kuibariki nchi yetu, tudumu katika umoja, amani na utulivu. Tumuombe pia Mwenyezi Mungu aendelee kutuongoza katika utu na weledi kwenye utekelezaji wa majukumu yetu, na kuzibariki kazi tunazozifanya katika kuleta ustawi wa nchi yetu na Wananchi wote.
Kazi na Utu, Tunasonga Mbele.
Shughuli hiyo itafanyika uwanja wa Liti uliopo Manispaa ya Singida, ambayo itatanguliwa na shughuli mbalimbali ,huku Β jumla ya watu 2,500 wakitarajiwa kushiriki kwenye michezo hiyo itakayohusisha watumishi kutoka katika wizara tofauti,taasisi binafsi na za umma,
SINGIDA MWENYEJI MEI MOSI 2025
Kuelekea katika maadhimisho ya siku ya Wafanyakazi Duniani (maarufu kama Mei Mosi),Mkoa wa Singida unatarajiwa kuwa mwenyeji wa maadhimisho hayo nchini Tanzania yatakayofanyika Tarehe Mosi mwezi Mei 2025.
WAZIRI SILAA AANZA ZIARA MANYONI-SINGIDA
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Jerry William Silaa, amewasili Mkoa wa Singida, na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa Mhe. Halima Dendego na viongozi wa wilaya ya Manyoni leo Oktoba 22, 2024.
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Jerry William Silaa (Mb.) akikagua kituo cha kuongeza usikivu cha Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kilichopo Mwanzi Wilayani Manyoni - Singida leo Oktoba 22, 2024.
#ZiarayaWaziriSilaaSingida#KaziIendelee
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Jerry William Silaa (Mb.) akikagua mradi wa maji wa miji 28 wa miji 28 wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo katika wilaya ya Manyoni - Singida leo Oktoba 22, 2024.
#ZiarayaWaziriSilaaSingida
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Jerry William Silaa, amezindua mnara wa mawasiliano ya simu katika Kijiji cha Hika, Wilaya ya Manyoni, Singida, leo Oktoba 22, 2024.
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Jerry William Silaa (Mb.) akikagua mradi wa ujenzi Shule ya Msingi Mlowa wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo katika wilaya ya Itigi mkoani Singida leo Oktoba 22, 2024.
#ZiarayaWaziriSilaaSingida
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Jerry William Silaa (Mb.) akikagua kituo cha Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano wilayani Itigi - Singida leo Oktoba 22, 2024.
#ZiarayaWaziriSilaaSingida#KaziIendelee
Nikiwa na Viongozi na wadau mbalimbali kwenye Kongamano la Nishati Safi ya Kupikia lililofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete (JKCC) Dodoma.
Kongamano linalokwenda pamoja na ugawaji wa mitaji na vitendea kazi vya Nishati Safi ya Kupikia.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amefungua Mafunzo ya Uongozi kwa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa yanayofanyika katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere β Kibaha Mkoani Pwani. Tarehe 22 Agosti 2023.
#Kaziiendelee
Leo nchi yetu inaadhimisha siku adhimu kuwakumbuka mashujaa wetu. Hii ni miamba na majabali ya kihistoria ambayo kwa kujitoa kwao kwa hali na mali kumetufanya sisi kuwa huru, kuishi huru, kuwa na Taifa letu, nyumbani kwetu, na kuwa hapa tulipo kama nchi.
Tunajenga mnara mrefu zaidi barani Afrika katika Jiji la Dodoma kama sehemu ya kuendelea kuwaenzi mashujaa wetu. Mnara huu ni alama nyingine ya uhuru wetu, shukrani yetu na kujitambua kwetu wapi tumetoka, wapi tupo na wapi tunakwenda. Nawaelekeza Ofisi ya Waziri Mkuu, Wizara ya Fedha na wote wanaohusika na ujenzi huu wa kihistoria kuhakikisha unakamilika kwa wakati na kwa viwango.
Siku hii pia ni siku ya tafakari. Tafakari ya kuendelea kuyaishi waliyoyaamini na kuyasimamia mashujaa wetu kwa kutunza amani, umoja, utulivu, mshikamano na kufanya kazi kwa bidii kwa Taifa letu.
Katika siku hii muhimu, tuendelee pia kukumbuka na kuzingatia kuwa Tanzania ni moja, itabaki kuwa moja na kamwe haitagawanyika. Tusikubali na hatutaruhusu mtu yeyote au kikundi chochote kutugawa kwa kisingizio chochote kile.
Mwenyezi Mungu Ibariki Afrika.
Mwenyezi Mungu Ibariki Tanzania.