Ninawatakia Waislamu na Watanzania wote kheri ya Sikukuu ya Eid al-Adha. Tafakari na mafundisho ya Sikukuu hii yanatuasa kuishi katika utii kwa Mola wetu, katika ukweli na kumtegemea Mwenyezi Mungu, huku tukiwajali wenye uhitaji na wote ambao Mola amewaweka katika njia ya kuhudumiwa nasi kwa namna mbalimbali.
Sikukuu hii iendelee kutudumisha sote na Taifa letu katika amani, upendo na umoja. Mwenyezi Mungu Mtukufu aendelee kuzipokea na kuzikubali dua zetu katika yote mema kwa nchi yetu.
Eid al-Adha Mubarak.
On behalf of the Government and the People of the United Republic of Tanzania, I extend my heartfelt congratulations to His Excellency, President Vladimir Putin on being re-elected as the President of the Russian Federation. We are looking forward to continue working together to strengthen the bilateral relations between Tanzania and Russia.
Hongereni sana Klabu ya Simba kwa kufanikiwa kufuzu hatua ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Mafanikio yenu si tu furaha na fahari kwa mashabiki na wanachama wa Klabu ya Simba, bali pia kwa Taifa na Watanzania wote.