Mhe. Thabo Mbeki, Rais mstaafu wa Afrika ya Kusini, amewasili nchini leo Mei 20, 2025, kushiriki mhadhara wa Siku ya Afrika ulioandaliwa na Taasisi ya Thabo Mbeki kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania.
Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam, Thabo Mbeki amepokelewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Cosato Chumi.
Mhadhara huo utafanyika Mei 24, 2025 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) mkoani Dar es Salaam. Mhadhara huo ambao ni wa 15 kuandaliwa na Taasisi ya Thabo Mbeki, unatarajiwa kujadili mustakabali wa Bara la Afrika, na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwemo wanataaluma, wadau kutoka Serikalini, viongozi wastaafu, vijana, na wawakilishi wa sekta binafsi.
Mhadhara huo nafanyika nchini baada ya Taasisi ya Thabo Mbeki kuichagua Tanzania kuwa mwenyeji kwa ukanda wa Afrika Mashariki. Aidha, Mhe.Rais mstaafu Mbeki pia anatarajiwa kushiriki katika mijadala mbalimbali ukiwemo ule kuhusu Uchumi wa Buluu na Utalii, na mjadala wa Wanataaluma wa Vyuo Vikuu.
BREAKING: Prof. Mohamed Janabi, proposed by Tanzania🇹🇿, has been nominated as the next @WHOAFRO Regional Director during a Special Session of the WHO Regional Committee for Africa, held today in Geneva.
Prof. Janabi will be appointed by @WHO Executive Board, to be held on 28-29 May, and take office thereafter.
Kwa nafasi yangu ya Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Vatican mwenye Makazi Berlin, Ujerumani nimewasilisha salamu za pongezi na kheri kutoka kwa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Baba Mtakatifu Leo wa XIV.
Kwenye salamu hizo, Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amempongeza Papa leo XIV kufuatia kuchaguliwa kuwa Papa wa 267 na Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani. Aidha, amemuahidi ushirikiano katika kutekeleza majukumu yake.
Kwa upande wake Papa Leo XIV ameeleza kuwa amefurahi kupokea salamu kutoka Tanzania, nchi ambayo anaipenda kwa kuwa ameshawahi kuitembelea mara kadhaa akiwa anatekeleza majukumu ya kikazi.
Ameelezea utayari wake kufanya kazi kwa karibu na Tanzania pamoja na nchi nyingine za Afrika.
Salamu hizo ziliwasilishwa baada ya Sherehe ya Kusimikwa rasmi kama Rais wa Vatican na Kiongozi wa Kanisa katoliki Duniani.
Sherehe hizo zilifanyika kwenye Basilica la Mt. Petro, Vatican leo tarehe 18/05/2025.
Zikiwa zimebaki siku mbili tu kabla uchaguzi wako wa WHO Africa Regional Director, utakaofanyika hapa Geneva (the battle ground) allow me to wish you all the best and take heed of your efforts. All the Best Prof! Kwa Imani zetu tuendelee kumuomba Mungu🙏. Mungu Mbariki Mgombea wetu, Mungu Ibariki Tanzania na Mungu Ibariki Afrika! #janabi4whoafro
Tanzania na Finland kuimarisha Ushirikiano katika Usimamizi wa Amani na Usuluhishi wa migogoro
Rais wa Jamhuri ya Finland, Mhe. Alexander Stubb amesema Serikali ya Finland itaendelea kuimarisha ushirikiano na Tanzania ili kuhakikisha juhudi za pamoja zinatekelezwa katika usimamizi wa amani na usuluhishi wa migogoro Barani Afrika na duniani kwa ujumla.
Mhe. Rais Stubb ameyasema hayo Mei 15, 2025 wakati akifungua semina ya kuenzi mchango wa Rais wa zamani wa Jamhuri ya Finland, Hayati Martti Ahtisaari katika kuleta amani na upatanishi duniani, iliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.
Mhe. Rais Stubb amesema kuwa, Hayati Martti Ahtisaari ni hazina na mwongozo kwa dunia ya leo, kwani aliifuindisha Dunia kuwa amani ni kitu kinachowezekana, kama watatuzi wa amani watakuwa tayari kusikilizana na kushirikiana kwa dhati.
“Hayati Ahtisaari, alijulikana kwa juhudi zake za kusuluhisha migogoro katika nchi za Kosovo, Namibia, na jimbo la Aceh nchini Indonesia, ambapo alitumia njia ya mazungumzo na maridhiano, katika kuleta usuluhu endelevu kwenye maeneo yaliyoathirika na migogoro ya muda mrefu” alifafanua Mhe. Rais Stubb.
Awali, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb.), ameishukuru Finland kwa ushirikiano na mchango wake katika miradi ya maendeleo nchini na ufadhili wa program mbalimbali katika Taasisi ya Uongozi na Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Dkt. Salim Ahamed Salim, hatua ambayo imeimarisha utekelezaji wa majukumu ya taasisi hizo katika ngazi ya Kitaifa na Kimataifa.
Kuhusu mchango wa Finland katika kukuza amani na utatuzi wa migogoro Waziri Kombo amesisitiza, Tanzania itaendelea kuwa mstari wa mbele katika juhudi za kutafuta amani, huku ikizingatia falsafa nne ambazo ni, Maridhiano, Ustahimilivu, Mageuzi na Kujenga upya taifa (4R), zilizoanzishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ili kujenga jamii zenye mshikamano na amani ya kudumu.
“Kwa Tanzania, Hayati Rais Ahtisaari ni mtu wa kipekee kwetu, aliishi nasi na kushiriki nasi katika kumbukumbu nyingi nzuri tangu mwaka 1973, alipochaguliwa kuwa Balozi wa Finland hapa Tanzania. Urafiki wake wa muda mrefu na marehemu Rais Benjamin William Mkapa unakumbusha kuwa alikuwa na uhusiano wa kipekee na Watanzania” Mhe. Kombo alieleza.
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Kutetea Amani la Martti Ahtisaari, Bw. Marko Ahtisaari, amesema kuimarika kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Jamhuri ya Finland kunatokana na msingi imara uliowekwa na viongozi waasisi wa mataifa hayo, akiwemo Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Hayati Benjamin Mkapa na Hayati Martti Ahtisaari, ambao wamewezesha nchi hizo kukuza maeneo ya ushirikiano kwa manufaa ya wananchi wa pande zote mbili.
Tanzania na Morocco zakubaliana kuimarisha ushirikiano wa matumizi ya teknolojia katika Sekta ya Nishati ili kuiwezesha sekta hiyo kuwa na mchango endelevu nchini.
Hayo yamebainishwa Mei 14, 2025 na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko wakati alipokutana na mwenyeji wake Waziri wa Mageuzi ya Nishati na Maendeleo Endelevu wa Ufalme wa Morocco, Mhe. Leila Benali kuzungumza kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu sekta ya nishati ili kuimarisha ushirikiano na nchi ya Morocco.
“Mwaka 2016 Tanzania na Morocco zilisaini hati ya makubaliano (MoU) ya kuimarisha ushirikiano katika sekta ya umeme, mafuta na matumizi ya nishati mbadala ili yapewe kipaumbele katika nchi hizo”. Amesema Dkt. Biteko
Mhe. Dkt. Biteko amesema pamoja na maendeleo ya nishati yaliyofikiwa, bado nchi inahitaji uwekezaji zaidi katika sekta ya nishati mbadala ikiwa na matarajio ya kukuza shughuli za kiuchumi hususan katika sekta za viwanda na madini jambo ambalo linahitaji uwekezaji wa kimkakati zaidi katika sekta ya nishati.
Kwa upande wake, Waziri wa Mageuzi ya Nishati na Maendeleo Endelevu wa Ufalme wa Morocco, Mhe. Leila Benali amesema kuwa Tanzania inaweza kubadilisha sura yake kwa kuwa na juhudi za pamoja za kuunganisha rasilimali zilizopo kuhakikisha nishati ya umeme inawafikia wananchi wengi zaidi.
Aidha, Mhe. Benali amepongeza kwa dhati juhudi za Rais Samia kuwa kinara wa maendeleo ya nishati safi ya kupikia, Tanzania na Afrika kwa ujumla.
Katika ziara hiyo, Dkt. Biteko ameongozana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Mhe. Dennis Londo, Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa, Mhe. Ally Mwadini, Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Africa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Rosemary Jeiro, wataalam mbalimbali kutoka Wizara ya Nishati, Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC).
Tumepata heshma kumpokea Ubalozini @UbaloziGermany Mhe. Dkt. Stergomena Lawrence Tax (Mb), @DrTaxs Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mheshimiwa Waziri Tax yuko Ujerumani kushiriki Mkutano wa Mawaziri wa Nchi zinazoshiriki Operesheni za Amani za Umoja wa Mataifa (UNPeacekeeping Ministerial Conference 2025) kuanzia tarehe 13 - 14 Mei 2025 - Berlin, Ujerumani.
Honoured to welcome Hon. Minister Masauni to Oslo. @vpo_tanzania
His visit builds on H.E. President Samia’s 2024 State Visit — strengthening 🇳🇴🇹🇿 ties on:
• COP30 & AGN
• Climate finance
• Clean cooking
• Plastic & waste solutions
#ClimateAction#COP30
The Ambassador of the United Republic of Tanzania to the Democratic Republic of Congo, H.E. Said J. Mshana recently met with Dr. Deo Mwapinga, the newly appointed Secretary-General of the Forum of Parliaments of Member States of the Great Lakes Region (FP-ICGLR), at his office in Kinshasa. Dr. Mwapinga has arrived in DRC to begin his duties at the FP-ICGLR headquarters. @UbaloziDRC
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiongoza ujumbe wa Tanzania kwenye mazungumzo rasmi na ujumbe wa Finland ulioongozwa na Rais wa Nchi hiyo Mhe. Alexander Stubb, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 14 Mei, 2025.