CCM inapata kiburi cha ku parade wafanyabiashara kukusanya fedha kwa sababu WALIUA Bunge. Miaka ya nyuma wafanyabiashara walichangia CCM lakini sio hadharani kwa sababu walijua kuwa kashfa zao zitaibuliwa Bungeni. Wafanyabiashara ilibidi wachangie vyama vyote kisiri ili kuhakikisha wanalinda maslahi yao. Baada ya kupata Bunge Kibogoyo mwaka 2020 CCM inaamini kuwa itaendelea kuwa na Bunge kibogoyo tena na hivyo imejenga kiburi cha ajabu kabisa na wafanyabiashara nao bila kujali sensitivities za wateja wao wamejawa na kibri. Watanzania wanayo nafasi ya kuwaonyesha Watawala kuwa wao ndio wenye nchi.
Tafrija ya jana Mlimani City ya MONEY LAUNDERING inapaswa kuwa TURNING POINT ya Siasa zetu.