βWatu wengi wanaenda chuo kwa sababu wazazi wao ndio wanataka, ila wao binafsi hawajui hata wanataka nini.
Maisha ni kuhusu kuwa tajiri na furaha, siyo digrii. Mara nyingi huwa nawaambia watu kuwa chuo ni chaguo, lakini kwenda high school ni lazima.β
βYe
Soma Zaidi:ππ
Kanuni Sita za Uongozi Tunazoweza Kujifunza Kutoka kwa Tai
1. Tai huruka peke yao na tena anga za juu. Hawaruki na kunguru, mwewe au ndege wadogo.
MAANA: Kaa mbali na watu wenye mitazamo midogo(dhaifu), wale ambao hukuangusha chini. Tai huruka na tai wenzake. Kaa kati ya watu bora.
2. Tai wanaona kwa usahihi mkubwa. Wana uwezo wa kufokasi kwenye kitu tokea umbali wa kilomita 5. Haijalishi aina ya kikwazo, tai hataondoa macho yake kwenye windo lake hadi pale atakapolikamata.
MAANA: Kuwa na maono na endelea kufokasi bila kujali aina ya kizuizi hadi pale utakapofanikiwa.
3. Tai hawali mzoga. Hula mawindo yasiyolala(freshi).
MAANA: Usitegemee mafanikio yako ya kale(jana), endelea kutafuta maeneo mapya ya kuteka. Iache historia yako huko ilipo, zamani.
4. Tai hupenda dhoruba. Mawingu yanapojikusanya, tai hufurahia, tai huutumia upepo wa dhoruba kupanda juu zaidi. Mara tai anapokutana na upepo wa dhoruba, huitumia dhoruba kupanda juu ya mawingu. Hii humpa tai fursa ya kuelea na kupumzisha mabawa yake. Wakati huo ndege wengine hujificha kwenye matawi na majani ya miti.
MAANA: Kabiliana na changamoto zako uso kwa uso huku ukitambua kuwa zitakuacha ukiwa imara na bora kuliko ulivyokuwa. Tunaweza kutumia dhoruba za maisha kupanda ngazi za juu zaidi. Wapambanaji huwa hawaogopi kufika hatua za juu zaidi. Wapambanaji huwa hawaogopi changamoto, zaidi huzikabili na kuzitumia kwa faida.
5. Tai hujiandaa kwa Mafunzo.
Huondoa manyoya na majani malaini kwenye kiota ili watoto wao wajisikie usumbufu katika maandalizi ya kuruka na hatimaye huruka pale ambapo huwawia vigumu kuendelea kukaa kwenye kiota.
MAANA: Achana na utulivu uliouzoea na raha, Hakuna kukua hapo.
6. Tai anapozeeka, manyoya yake huwa dhaifu na hushindwa kumpeleka kwa kasi na kumpandisha juu kama atakavyo. Hii humfanya kuwa dhaifu na huweza kumsababishia kifo. Hivyo huenda kupumzika mbali milimani. Akiwa huko, hunyofoa manyoa yote dhaifu mwilini mwake na huvunja mdomo wake kwenye mawe na makucha yake kwenye miamba hadi pale anapobakia mtupu kabisa; ni mchakato wenye kumwaga damu nyingi na maumivu makali. Kisha hubakia huko mafichoni hadi pale anapoota manyoya mapya, mdomo mpya na kucha mpya, kisha hutokea akiruka juu kuliko awali.
MAANA: Tunawiwa mara kadhaa kuachana na tabia za kale bila kujali ugumu uliopo katika kuziacha, mambo yanayotuwia mzigo au vitu ambavyo haviongezi thamani katika maisha yetu vinatakiwa kuondoka.
Asante kwa kusoma na ππΏππΏππΏ