Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi Mhe. Shaaban A. Othman azindua ripoti ya kitaalamu katika kutambua mahitaji ya teknolojia kwenye Sekta ya Uvuvi upande wa Bahari ya Hindi, ambapo amesema Sekta ya Uvuvi inayo maeneo mahsusi ya kimkakati ili kukuza sekta hiyo
Uzinduzi wa Tathmini ya Mahitaji ya Teknolojia (TNA) – Jamhuri ya Muungano wa Tanzania utakaofanyika siku ya tarehe 25 Juni 2025, Hyatt Regency – The Kilimanjaro, Dar es Salaam.
Mgeni Rasmi, Mhe. Dkt. Ashatu K. Kijaji (Mb), Waziri wa Mifugo na Uvuvi.
Uzinduzi wa Tathmini ya Mahitaji ya Teknolojia (TNA) – Jamhuri ya Muungano wa Tanzania utakaofanyika siku ya tarehe 25 Juni 2025, Hyatt Regency – The Kilimanjaro, Dar es Salaam.
Mgeni Rasmi, Mhe. Dkt. Ashatu K. Kijaji (Mb), Waziri wa Mifugo na Uvuvi.
Mkutano wa wadau wa sekta ya uvuvi uliofanyika tarehe 16 April 2025 katika ukumbumbi wa mikutano wa Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi Zanzibar jengo la ZURA kuhusu kutoa maoni juu ya andiko la kuiomba Serikali ya Tanzania kuridhia mkataba wa UNFSA wa mwaka 1995.
Ujumbe wa wanafunzi kutoka World Maritime University - Sweden wamefanya ziara katika ofisi za Mamlaka ya Kusimamia Uvuvi wa Bahari Kuu (DSFA) na kuweza kufahamu majukumu mbalimbali ya Mamlaka. Ujumbe huo ulikaribishwa na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa DSFA Dkt. Saleh A. Yahya.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji amefanya ziara katika Mamlaka ya Kusimamia Uvuvi wa Bahari Kuu (DSFA) na kuzungumza na watumishi wa mamlaka hiyo. Mhe. Dkt. Kijaji amewataka watumishi wa DSFA kuongeza juhudi katika kufanya kazi ili kuengeza pato la nchi.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt. Ashatu Kachwamba Kijaji akikagua maeneo mbalimbali ya Mamlaka ya Kusimamia Uvuvi wa Bahari Kuu (DSFA) ikiwa ni kufuatia matayarisho ya ziara ya Rais wa Somalia Mhe. Hassan Sheikh Mohamud itakayofanyika tarehe 29/01/2025.
Mafunzo ya matumizi ya mifumo ya kusimamia mienendo ya meli baharini (MDA Tools and resources) yaliyofanyika kuanzia tarehe 2 hadi 13 Disemba 2024. Yametolewa na UNODC na wanufaika Taasisi za DSFA, KMKM na Police Marine. Mafunzo hayo yanasaidia kudhibiti vitendo haramu vya Uvuvi.
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo ikiongozwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalla Hamis Ulega, ilitembelea Mamlaka ya Kusimamia Uvuvi wa Bahari Kuu (DSFA) na majukumu na kazi zinazofanywa na DSFA.
Wajumbe wa Kamati ya Bajeti ya Baraza la Wawakilishi wakiongozwa na Mwenyekiti wa kamati Mhe. Mwanasha Kh. Juma, walifanya kikao na uongozi wa DSFA chini ya uongozi wa Mkurugenzi Mkuu Dkt. Sweke katika kufuatilia taasisi hiyo juu ya bajeti kwa mwaka wa fedha 2024/2025.
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa DSFA Dkt. Saleh A. Yahya akiwa na Wataalam wa DSFA pamoja na timu ya Mkandarasi Mshauri wa Upembuzi yakinifu kuelekea ujenzi wa Bandari ya Uvuvi ya Bagamoyo. Timu hiyo ikiongozwa na Professor Sang-youl Kim wa Pusan National University waliitembelea DSFA.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Batilda Burian akiwa pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa (DSFA) Dkt. Sweke na Mkurugenzi wa Albacora, Bw. Imanol Loinix na Maafisa kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkuu wa Mkoa wakiwa katika kikao kujadili kiwanda cha kuchakata samaki kitakachojengwa Tanga.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Kusimamia Uvuvi wa Bahari Kuu (DSFA) Dkt. Emmanuel Sweke, akitoa mada kuhusu Uvuvi wa Bahari na masuala ya Makubaliano (Negotiations) katika Ukumbi wa Chuo Kikuu Huria (OUT) Jijini Dar es salaam yakiwa na lengo la kuwajengea Maafisa wa Serikali uwezo
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Riziki Silas Shemdoe akihutubia wavuvi 96 wa Kizimkazi, Kusini Unguja waliopewa mafunzo ya uvuvi kuelekea Maadhimisho ya Tisa ya Tamasha la Kizimkazi 2024 litakalofanyika kuanzia tarehe 18 hadi 25.
Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi Zanzibar Mhe. Shaaban Ali Othman amefanya ziara katika Ofisi za Mamlaka ya Kusimamia Uuvi wa Bahari Kuu (DSFA) na kuzungumza na watumishi wa Mamlaka hiyo. Mhe. Shaban alipokelewa na Mkurugenzi Mkuu wa DSFA Dkt. Emmanuel Andrew Sweke.
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar Mhe. Dkt. Said Mohammed Dimwa (aliyesimama kati) Leo 11/03/2024 ametembelea katika banda la maonesho la DSFA katika Maonesho ya saba ya Kilimo ya nane nane katika viwanja vya Dole Kizimbani Zanzibar.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi Capct. Hamad Bakar Hamad akiwa na uongozi mzima wa Wizara katika siku ya Uchumi wa Buluu iliyofanyika katika Maonesho ya saba ya Kilimo ya nane nane huku Kizimbani. Siku hii ilinogeshwa na ngoma maarufu katika visiwa vya Zanzibar.
Ujumbe kutoka Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora imetembelea Mamlaka ya Kusimamia Uvuvi wa Bahari Kuu (DSFA) na kufanya kikao na uongozi pamoja na watumishi wa DSFA. DSFA ni moja ya Taasisi ambayo ni mdau wa Tume hiyo.
Naibu Katibu Mkuu (Uvuvi), wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Edwin Mhede, alifanya ziara ya kutembelea Mamlaka ya Kusimamia Uvuvi wa Bahari Kuu (DSFA ) na kukagua shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na Mamlaka na kuongea na Menejimenti ya DSFA.
Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Hassan Khamis Hafidh akipata maelezo juu ya uvuvi wa bahari kuu kutoka kwa Afisa Udhibiti Nd. Juma Haji baada ya kutembelea banda la Mamlaka ya Kusimamia Uvuvi wa Bahari Kuu katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar Es Salaam.