Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) wakati akitokea Dubai, tarehe 06 Februari, 2026.
Alipokuwa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Mhe. Rais Dkt. Samia alishiriki katika Mkutano wa Dunia wa Serikali (World Governments Summit – WGS) 2026 pamoja na Uzinduzi wa Jukwaa la Kimataifa wa Uwekezaji Afrika (GAIS).
_______
#TanzaniaNaUwekezaji
#DiplomasiaYaKiuchumi
#KaziNaUtuTunasongaMbele
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na Viongozi mbalimbali kwenye hafla ya kutunuku Nishani ya miaka 60 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika ukumbi wa Jakaya Kikwete, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 29 Agosti, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiondoka katika uwanja wa Ndege wa Waterkloof Pretoria nchini Afrika Kusini mara baada ya kuhudhuria hafla ya Uapisho wa Rais wa nchi hiyo Mhe. Cyril Ramaphosa iliofanyika Pretoria tarehe 19 Juni, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye Dua ya pamoja na Waumini wa Dini ya Kiislam mara baada ya kumalizika kwa Sala ya Eid Al Adha iliyosaliwa katika Msikiti wa Mikocheni kwa Warioba Jijini Dar es Salaam tarehe 17 Juni, 2024.
It was an honour to meet the charismatic President of the United Republic of Tanzania, Her Excellency @SuluhuSamia. Fascinating to hear her deep insights about the future of Africa and discuss the possibilities for forging a long-term partnership with one of Africa's most promising and strategically important nations. We are excited about the Adani Group leveraging its expertise across various infrastructure sectors, including ports, renewable energy, airports, transmission, distribution and rail to help build world-class infrastructure in Tanzania.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipiga makofi mara baada ya kutunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari (Honoris Causa) ya Uchumi katika Chuo Kikuu cha Ankara nchini Uturuki tarehe 18 Aprili, 2024.
Katika mazungumzo na Waziri Mkuu Mstaafu, Mheshimiwa Cleopa David Msuya (Waziri Mkuu wa 3 wa Tanzania), Ikulu ya Chamwino leo. Mheshimiwa Msuya aliungana nasi katika ununuzi wa hisa zaidi kutoka kwa mwekezaji ili kutekeleza nia ya kuongeza umiliki wa serikali katika kitalu cha gesi asilia cha Mnazi Bay.
Mabadiliko ya tabianchi yamefanya mahitaji ya gesi na nishati nyingine mbadala kuwa kipaumbele katika kujenga uchumi shindani hivyo basi, kama nchi hatuna budi kuongeza uzalishaji na usambazaji.
Lengo la kila Mtanzania ni kuona rasilimali za nchi ikiwemo gesi asilia zinawanufaisha wananchi na Taifa kikamilifu. Matarajio yangu na ya kila Mtanzania ni kuona watu wote tunaowapa dhamana ya kusimamia mashirika na taasisi za kutekekeleza malengo yetu kama Taifa wanaelewa matarajio yetu, wanaelewa wanapaswa kufanya kazi kwa ubunifu na weledi wa hali ya juu, na kutanguliza mbele maslahi ya Taifa letu, na si vinginevyo.
I am deeply saddened to learn of the passing of the President of Namibia, His Excellency @hagegeingob, a dear brother, a venerable Pan Africanist and a great friend of Tanzania.
On behalf of the people of the United Republic of Tanzania, I send my condolences to the people of the Republic of Namibia, the Acting President, His Excellency Dr. Nangolo Mbumba, Madam First Lady, Her Excellency Monica Kalondo, family, friends and comrades in SWAPO.
May you all be comforted during this difficult time. May his soul rest in peace. Amen.
Mapema leo mkoani Mwanza, nilipogawa vizimba vya kufugia samaki na boti za kisasa kwa baadhi ya Watanzania wenzetu hasa vijana wanaojishughulisha na uvuvi katika Ziwa Victoria, ambapo pia nilipata wasaa wa kuzungumza na wananchi.
Nimeagiza Wizara ya Mifugo na Uvuvi kuhakikisha inaendelea kutekeleza kwa kasi programu za mafunzo na utoaji wa vifaa vya kisasa kwa makundi mengi zaidi, kama mbinu mojawapo ya kuondoa uvuvi haramu, unaotishia uhai wa sekta hii ambayo ni nguzo ya uchumi kwa mamilioni ya Watanzania.
MWAMKO NI MKUBWA SANA Jakarta 🔥
Wawekezaji na wafanyabiashara wa INDONESIA wamejitokeza kwa wingi kukutana na wenzao kutoka Tanzania.
Serikali ya Mh Rais Dkt Samia S Hassan imeweka kipaumbele kukuza wawekezaji watanzania kwa kuwakutanisha na wenzao ili kuwekeza pamoja nchini.