#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 105
Mhe. Lissu: Kwahiyo wewe hufahamu mtu anayeteua Mawaziri nchi hii wewe humfahamu?
Kaaya: Mawaziri wanateuliwa na Rais.
Mhe. Lissu: Kwahiyo Mohamed Mchengerwa ni mteule wa Rais Samia? Huyo ni waziri wa TAMISEMI.
Kaaya: Ni kweli.
Mhe. Lissu: Je ni kweli au sio kweli ni Waziri ambae anatoa tangazo la uchaguzi na ratiba yake ya huo uchaguzi wa serikali za mitaa?
Kaaya: Sina Uhakika.
Mhe. Lissu: Ni kweli au sio kweli wasimamizi wakuu wa uchaguzi huo ambao ni returning officer ni wakurugenzi wa halmashauri mbalimbali?
Kaaya: Sijui.
Mhe. Lissu: Ni kweli au sio kweli Wakurugenzi wote wa halmashauri za Wilaya ni wateule wa Rais?
Kaaya: Sifahamu.
Mhe. Lissu ; Askari Polisi mwenye cheo cha Inspector hafahamu wakurugenzi wanateuliwa na nani? Vituko na aibu. (Nimechomekea mimi hii)
Mhe.Lissu: Ni kweli kwamba watumishi wote wa serikali za mitaa wanaohusika na uchaguzi wa serikali za mitaa wanafanya kazi kwa niaba ya Rais au maelekezo ya Rais?
Kaaya: Sina Uhakika.
Mhe. Lissu: Ni kweli uchaguzi wa serikali za mitaa 2024 kwa maelfu walienguliwa na kuzuiwa kugombea?
Kaaya: Sina uhakika.
Mhe. Lissu: Ni kweli au si kweli baada ya kuenguliwa kelele ikawa kubwa hadi Dr. Nchimbi katibu mkuu wa CCM alielekeza pia warudishwe?
Kaaya: Sina Uhakika.
Mhe. Lissu: Ni kweli baada ya kelele zote hizo Waziri wa Tamisemi Mchengerwa aliomba muda uongezwe na kubadili ratiba ya Uchaguzi?
Anasimama Renatus Mkude anasema Mheshimiwa Jaji imefika saa tano kamili naomba turuhusiwe kwenda msibani na tutafikisha salamu za rambirambi pia za Mshitakiwa.
Jaji Ndunguru: Shahidi tukutane kesho saa tatu asubuhi.
Tunaahirisha shauri hili.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Leo Oktoba 16, 2025
Jana tuliishia part 105 so leo tunaendelea na-;
Part 106
Muda huu ni saa tatu asubuhi.
Tumefika Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es salaam.
Hali ya Mahakama ni nzuri.
Tunawashuhudia Waandishi wakichukua picha mgando na mnato kwa watu mbalimbali waliopo hapa Mahakamani.
Askari Magereza wale wa Kikosi Maalum yaani KM wako hapa ndani ya Chumba cha Mahakama wanazunguka zunguka kama wanakagua lindo vile.
Wasaidizi wawili wa Majaji tunawaona wako hapo mbele, Mwanamke mmoja na Mwanaume Mmoja kwa wasiofahamu hawa wanaoitwa Wasaidizi wa Majaji kitaaluma ni Mahakimu Wakazi.
Cheo chao ni sawa na Mahakimu waliopo Kisutu pale hawa hufanya kazi ya kuwasaidia majukumu ya kufanya research mbalimbali za masuala ya kisheria.
Wameingia hapa Majaji watatu kama kawaida ambao ni Jaji Dunstan Ndunguru, James Karayemaha na Ferdinand Kiwonde. Wakiwa kwenye magauni yao nasikia yanaitwa majoho mekundu.
Limesomwa shauri hapa na karani na amesimama Renatus Mkude Wakili Mkuu wa Serikali na ametambulisha wenzake muda huu, anasema upande wa Jamhuri wako tayari.
Mhe. Lissu ameulizwa yuko tayari na anaomba akumbushwe shahidi aliishia wapi kujibu maswali yake.
Amekumbushwa anasema anaomba aanze sasa.
Mhe. Lissu: Shahidi umeamka salama?
Kaaya: Nimeamka salama Mheshimiwa Lissu.
Mhe. Lissu: Waeleze Majaji kama ulieleza kwamba fomu No. 145 kwamba haikusomwa wakati wa committal Kisutu?
Kaaya: Sikuwepo Kisutu.
Mhe. Lissu: Je umeileta hapa Mahakamani?
Kaaya: Sijaileta pia.
Mhe. Lissu: Sasa turudi tulipoishia jana. Maelezo yako Polisi ulitoa maneno mengi ikiwemo "Baadhi ya maneno mengine aliyotamka Rais alitoa maelekezo kuwa hakikisheni wapinzani hawaendi kokote....."
Naomba majaji shahidi apewe Exhibit D1 ili twende pamoja.
Sasa shahidi baada ya kelele nyingi za wapinzani kuenguliwa akiwemo Nchimbi alisema mambo kuhusu uchaguzi.
Je unafahamu Mchengerwa Waziri wa Tamisemi alisema wakikata rufaa wagombea walioenguliwa watarudishwa?
Kaaya: Sikumbuki.
Mhe. Lissu: je unafahamu Mchengerwa aliongeza muda wa rufaa ili watu wakate rufaa?
Kaaya: Sikumbuki.
Mhe. Lissu: Unafahamu wagombea angalau wa Chadema kwa maelefu walikata rufaa ndani ya huo muda wa rufaa ambao uliongezwa na Mchengerwa?
Kaaya: Sikumbuki.
Mhe. Lissu: Rufaa za Uchaguzi wa serikali za mitaa zinasikilizwa na Kamati za Wilaya?
Kaaya: Sina kumbukumbu.
Mhe. Lissu: Je unafahamu wenyeviti wa kamati za rufaa za Wilaya ni Makatibu tawala wa Wilaya ambao ni wateule wa Rais?
Kaaya: Sina Uhakika.
Mhe. Lissu: wote waliokata rufaa waliorudishwa hawafiki hata 10?
Kaaya: Hilo silifahamu.
Mhe. Lissu: Ila maneno yangu unasema ya uongo kuhusu uchaguzi wakati wewe kila kitu hujui?
Kaaya: Kimya.
Mhe. Lissu: Sasa watu wanaosimamia uchaguzi wote wa serikali za mitaa ni watu wa Rais kama nilivyokuonyesha mimi nakosea wapi?
Kaaya: Rais akishachaguliwa anafanya kazi kwa niaba ya Serikali na sio Chama chake.
Mhe. Lissu: Kwahiyo akikosea na mimi nikimpinga nikisema anafanya mambo ya hovyo kuengua watu wa Chadema nakosea wapi? Hapo anakuwa ameacha kuwa mwana CCM?
Kaaya: Haachi kuwa Mwanaccm.
Mhe. Lissu: Sasa wewe fundi wa Viyoyozi hebu tuambie kazi za Mwenyekiti wa CCM anazifanya nani kipindi akiwa Rais?
Kaaya: Anaendelea kuzifanya mwenyewe.
Mhe. Lissu: unafahamu zaidi ya asilimia 98 ya wenyeviti wa mitaa waliochaguliwa ni wa CCM?
Kaaya: Sifahamu.
Mhe. Lissu: Je unafahamu kwamba mwaka 2014 kwenye Uchaguzi wa Vijiji na mitaa ambao wagombea wa upinzani hawakuenguliwa walipata asilimia 33 ya viti vyote vya serikali za mitaa?
Kaaya: Sina Takwimu hizo.
Mhe. Lissu: Je unafahamu mwaka 2014 asilimia zaidi ya 20 walienda kwa upinzani ulienda kwa upinzani?
Kaaya: Hilo nilisikia.
Mhe. Lissu: Uchaguzi wa 2019 ambao wagombea walienguliwa wa upinzani CCM ilipata wenyeviti wa mitaa 100%?
Kaaya: Sikumbuki.
Part 107 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 127
Anaendelea Katuga
Shahidi alitambua vielelezo pale kizimbani na ndio maana tunasema vipokelewe, alisema hawezi kutufundisha na sisi tunataka akitufundisha atufundishe kutoka kwenye Sheria.
Naomba niende kwenye hoja ya tatu ambayo inasema shahidi sio competent kutender hii exhibit na kwenye hoja hii aliialika Mahakama kwenye vile vifungu vingi kuanzia 216 hadi 221 vya CPA.
WAKATI KATUGA ANAENDELEA NI KAMA NIMEWAONA HAWA ASKARI MAGEREZA WANAOMLINDA MH. LISSU WAPO WAGENI NA SURA ZAO ZIMEKAA KAMA WALE WENZETU KWELI. WAPO WAGENI NDIO WAMELETWA HAPA. SIJUI WANA MPANGO GANI NA HAWA WALINZI WAO.
Acha tuendelee na Katuga sasa
Anataja vifungu vyote alivyovitaja Mh. Lissu na vinazungumzia nini? Kingereza chake ni kibovu sana. Akisoma mahali ZE ZE ZE ZE ZE ni nyingi sana.
PW 3 amejieleza kama yeye ni mtaalamu na alialikwa kufanyia kazi vielelezo na amejipambanua kuhusiana na umri wake na utaalamu wake. Na alifanyia kazi vielelezo hivi hivyo basi kifungu cha 52 cha Evidence Act Cap. 6 kinasema mtu mwenye uelewa na fingerprints, na ujuzi mwingine basi yanapokelewa.
Kila shahidi yuko entitled kuaminiwa unless Mahakama ije na sababu za kutomuamini.
Kesi ya Goodluck Kyando Vs Jamhuri TLR 2006 Every witness is entitled to credence.
Shahidi wetu anaomba kutoa memory card yenye video, flash yenye video.
Kifungu cha 70 cha Evidence Act Cap. 6 kinasema in any proceedings electronic evidence shall be admissible.
Mahakama ya rufaa imetoa visifa vya vitu inavyotakiwa kuzingatia kabla ya kupokea vielelezo.
Kesi maarufu ya DPP VS Sharif Mohamed, Athumani and 6 others CA 74 2016.
Kesi inasema mtu aliyefanyia kazi kielelezo ni competent ku tender pia kesi ya DPP vs Mirzai inatoa utaratibu huo wa kisheria.
Naomba kesi hizi zote nizitoe kwa Mahakama na mshitakiwa pia.
Amekuwa appointed na gazetted kwa kufanya uchunguzi na kutoa taarifa ndio kazi ya shahidi huyu.
Yeye ni shahidi wa picha mnato na mjongeo Gazeti la serikali no. 745/2022 ndio lilimtangaza kwa ajili ya kufanya uchunguzi na kutoa taarifa.
Tangazo hilo limesainiwa na DPP na kwamba title ya tangazo lile ni amri ya uteuzi wa wataalamu wa picha na mambo mengine.
Mtaalamu wetu anasema yeye ni mtaalamu wa picha mnato na picha mjongeo na mimi naialika mahakama itafute meaning ya picha, is video a picture? Vifungu vya 216 na kuendelea havioneshi mtaalamu wa video, hayupo.
Kifungu cha 220 cha CPA kwamba video ni cyber forensic expert, tafsiri ya CYBER ziko nyingi sana ikiwa ni pamoja na ushahidi wa Computer ndo maana yake.
Anachunguza devices utambuzi wa uhalisia wa picha utabaki kwa mtambuzi wa picha. Is a video a picture? Video ni picha za muendelezo.
Hapa cyber experts na photographic expert wasichanganywe ni watu wawili tofauti.
Kuna definition mbalimbali lakini kuna dictionary ya computer and internet terms ukurasa wa 363 alitafsiri photograph is a picture created by a camera whether digital or video. Ukurasa wa 513
Anasema Jaji unaenda kwa kasi sana hatukuelewi kwakweli hata unakimbilia wapi.
Au Mshitakiwa unasemaje Jaji anamuuliza. Lissu anajibu Mimi namuangalia tu naona anaongea ongea, nimemuacha.
Jaji sasa sisi tunaona ujielekeze vizuri ukiendeleea kujiongelea wewe sisi hatutaandika.
Haya rudia hapo sasa kwenye Dictionary taratibu.
Part 128 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 109
Katuga: Uliulizwa kuhusu suala la Notebook kama hiyo notebook umeileta. Je kwanini hujaileta.
Lissu anasimama napinga hilo swali la sikufika huko hakutoa sababu za kwanini hakuileta.
Katuga: Mhe. Jaji alimzuia shahidi asiendelee kutoa maelezo kwanini hakuleta.
Jaji: Hayo mambo ni mapya hatuwezi kukuruhusu. Uliza swali lingine.
Katuga: uliulizwa nani aliyechapisha ulisema ni wewe siku nyingine ukasema sifahamu na leo pia umesema ni yeye kupitia Jambo Tv. Sasa sisi tunataka ufafanuzi
Kaaya: Kupitia Jambo TV alichapisha maudhui yaliyopo kwenye hati ya mashitaka kitendo cha yeye kuwaalika wanahabari na kutoa maudhui yale ni tayari alikuwa ameridhia kutoa maudhui yale mtandoani.
Katuga kila baada ya swali moja anafanya vikao na mawakili wenzake sita hapa Mahakamani. Hii Re Examination yao imekuwa ngumu sana aiseee. Wanahangaika halafu ni kama shahidi anawajibu namna ambavyo walikuwa hawatarajii. Hawayafurahii majibu ya shahidi wao kabisa.
Katuga: Waheshimiwa Majaji naomba tuishie hapa kwenye maswali ya ufafanuzi kwa shahidi wetu. 😂
Hadi majaji wamecheka hapa kimya kimya. Hii re examination ilikuwa ngumu sana. Mhe. Lissu kamshona shahidi hadi upande wa Jamhuri wameshindwa kujua Shahidi atoe ufafanuzi wa jambo gani.😀
Jaji shahidi unaruhusiwa kuondoka. Tunakushukuru kwa ushahidi wako.
Insp. John Kaaya amejaribu kutoka kwa speed kidogo amejikwaa hapa kwenye kiti ametaka kumdondokea Askofu Mwamakula maana amekaa nae karibu na kizimba pale. 😂
Watu wamecheka inaonekana huyu Polisi alikuwa amechoka sana hii kazi kwakweli. ametoka kama haamini kweli amemaliza huu msala.
Amesima Renatus Mkude anasema tunae Shahidi wa tatu ambae ni SAMWEL ELIBARIKI KAAYA.
Jaji sasa huyu shahidi nae aje tuendelee.
Ananingia hapa Askari Mfupi wa kimo, ana kipara na ndevu nyinginyingi kidogo ambazo hazina afya zile ndevu kipilipili.
Jaji unaitwa nani?
Naitwa Samwel Elibariki Kaaya.
Mkaguzi wa Jeshi la Polisi.
Anaangalia kwa chini chini kwa kumuangalia tu muonekano wake inaonekana ana roho ngumu sana.
Anasema ana miaka 39.
Dini yangu ni Mkristo.
Anapelekewa Biblia aweze kuapa.
Anaishika mkono wa Kulia na amenyanyua juu.
Naapa ushahidi nitakaoutoa ni wakweli ewe Mwenyezi Mungu nisaidie.
Renatus Mkude anasimama naomba aongozwe na Thawabu Issa Wakili wa Serikali.
Huyu Thawabu Issa Wakili wa Serikali ndo yule alijifanya kurusha ngumi juzi kati anajikuta Rashid Matumla.
Amesimama ana kipara kama cha ushahidi.
Thawabu: Uongee kwa Sauti shahidi.
Jaji: Na wewe Wakili ongeza sauti sasa.
Thawabu: Kitengo gani upo?
Samwel Kaaya: Kitengo cha picha Kamisheni ya Uchunguzi sayansi jinai.
Sasa I tabidi huyu Shahidi nimuite Samweli maana na yeye ni Kaaya kama aliyetoka.😂
Thawabu: Kinajihusisha na nini kitendo hicho.
Samwel: Kitengo hicho kinajihusisha upigaji picha wa matukio mbalimbali lakini pia kurekodi matukio mbalimbali ya uhalifu. Kurekodi picha mjongeo za watuhumiwa wa uhalifu.
Thawabu: Upo kama nani kitengoni hapo?
Samwel: Niko kama mtaalamu wa picha baada ya kuteuliwa na DPP na kutangazwa na gazette la serikali GN. No. 745/2022.
Thawabu: Majukumu yako ni nini?
Samwel: Kupiga picha, kurekodi matukio ya uhalifu, kufanya uchunguzi wa picha mbalimbali kwa maana ya picha mjongeo na mnato.
Elimu yangu imegawanyika katika makundi mawili.
Elimu ya Kipolisi mwaka 2013/2014 nilihudhuria mafunzo ya awali ya Polisi. Recruit Course chuo cha Polisi Moshi CCP. Na mwaka 2014 nilimaliza na kutunukiwa Certificate of Competence.
Huko CCP Moshi nilijifunza criminal Laws, Evidence Law, Criminal Procedure, Bionnet, Parade Training, Parade la kutuliza ghasia, Self defense kwa maana ya Judo na Karate na Medani za Kivita.
Thawabu: Ulitunukiwa nini?
Samwel: Cheti cha Umahiri.
Thawabu: Kingine nini?
Samwel: Nilipata cheo cha awali cha Police Constable.
Part 110 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 124
Hio GN ndo iliyomthibitisha kama mtaalamu wa picha na anaetakiwa kuandaa ripoti ya uchunguzi kisheria.
Huyu ni mtaalamu wa picha za mnato au karatasi kisemo cha Mhe. Lissu pia proof ni kifungu cha sheria kilichotumika kumteua, ambacho amekitaja mwenyewe ambacho ni kifungu cha 216(1) cha Sheria Ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (2023) utaiona kwenye maelezo yake na pia kwenye Order ya Uteuzi wake.
Kwahiyo ni fundi wa picha za kawaida
kwenye sheria pia wanasema ateuliwe na DPP na ukisoma order hii aliofanya uteuzi ni AG badala ya DPP.
Kasheshe tayari hapa ni kama maji yamelowana na moto umeungua tena.😂
Uteuzi huu umefanywa na Adelardus Kilangi inatosha kabisa kubatilisha kila kitu alichofanya.
Anachosema hapa huyu sio mtaalamu wa chochote kwa mujibu wa hii order ambayo anasema yeye mwenyewe ameteuliwa, ni sababu mamlaka ya uteuzi sio mamlaka halali.
Katuga anashusha kamiwani hapa akitafakari utadhani amebanwa na mlango, mawakili wa Serikali kazini kwao kuna kazi sana aiseee.
Waheshimiwa Majaji, sihitaji kupoteza muda mrefu wakusema kwamba DPP na AG ni ofisi mbili tofauti zenye mamlaka mbili tofauti na sheria zinazogovern exercise zao of power ni mbili tofauti.
AG ana sheria yake inaitwa Office of AG dischare of duties act sura ya 278 na DPP sheria yake ni NPS ACT SURA YA 430.
Ofisi mbili za Kikatiba tofauti, mamlaka tofauti na sheria tofauti, AG hana mamlaka yoyote kwenye mashauri ya Jinai. Kiherehere hiki kimetokea wapi?
Sasa waheshimiwa Majaji what about ile GN alioitaja jana maana nimeisema ambayo hakuitaja, alietaja jana ilikuwa iko kwenye nyaraka zake akastuka akasema eeh huyu mtuhumiwa anaesoma kila kitu huyu���eeh.. ataniletea shida huko mbele nikienda kuchwakichwa.
What about GN NO 745 16TH December 2022?
Hii nayo imetungwa kwa Kifungu kilekile cha sheria ya CPA.
Mhe. Lissu anakisoma hapa ili aendelee kushusha nondo.
Mahakama imetulia sana watu wako kama wanasubiri kuchomwa na Sindano kuna kautulivu kakubwa sana ka kusikiliza hizi nondo.😂
Waheshimiwa Majaji wa Mahakama Kuu.
Amri hii imesainiwa Dodoma Tar. 28/10/2022 na Sylivester Anthony Mwakitalu, Mkurugenzi wa Mashtaka.
Na waheshimiwa Majaji katika jedwali lililoambatanishwa lina majina ya maafisa 184 na mtu wa 182 ni H6108 D/C Samweli Eliariki Kaaya, imeandikwa Eliarikis sio Elibariki lakini waheshimiwa majaji niko tayari kusema labda walimaanisha ni huyu shahidi Samweli Elibariki Kaaya.
Hata hivyo waheshimiwa majaji kwa mujibu wa Tangazo hilo la Serikali huyu ni mtaalam wa picha (still pictures) sio forensic expert. Hayo mamlaka hana.
Waheshimiwa majaji, mtu asiyekuwa na utaalamu wa mambo ya videos na ameandaa ripoti ya kitaalamu na anataka kuiwasilisha mahakamani, anawezaje kuruhusiwa kuwasilisha chochote cha kitaalamu?
Sio mtaalamu wa cyber, sio mtaalamu wa videos, hajateuliwa kwenye kazi hiyo. Tukisema amekuja kufanya umbea tutakuwa tunakosea? 😂😂
Waheshimiwa Majaji nawaalikeni mkaangalia ripoti ya Tume ya Kuangalia Jinsi ya Kubooresha Taasisi za Haki Jinai Nchini ya Julai 2023 maarufu kama Tume ya Jaji Mkuu Mohamed Chande Othman.
Waheshimiwa Majaji pengine sitakosea nikisema kuwa wakili wa serikali Mkuu Ignas Mwinuka alikuwa mjumbe kwenye hii tume, ameandikwaa huyu hapa (Mahakama kichekoo 😂 Mhe. Lissu anasema ni sifa maana wangapi wanateuliwa katika Tume kama hizi).
Waheshimiwa majaji nawaalika ukurasa wa 58 ambapo inasema hivi Tume imebaini kuwa weledi umepungua kwasababu askari wanapangiwa mambo wasiokuwa na taaluma nayo kama hili.
Mahakama kicheko.😂😂
Kinachoendelea hapa Mahakamani ni zile story za unasikia utamu hapohapo unasikia uchungu. 😂
Kuna Muda unapata hasira ukisikia haya mambo halafu ukimaliza unaanza kucheka tena hapo hapo.
Kwamba Mapolisi wanapangiwa majukumu ambayo hawana sifa nayo kuna muda wanalaumiwa kwenye mambo ambayo hawakutakiwa kupangiwa.
Part 125 itaendelea kwenye post inayofuata
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 116
Anaendele Shahidi Samuel Elibariki Kaaya
Tunafanya huu uhakiki kwasababu programu endeshi ndiyo inayoendesha hardware computer, kwa maana nyingine kama programu linzi isipokuwa compatible / isipoendana na hardware kwa maana ya compute hiyo, it cannot execute any task.
Sambamba na hilo programu chunguzi lazima iwe compatible na programu endeshi ili iweze kufanya majukum yake mahususi.
Waheshimiwa majaji hali ya programu kwa siku hiyo ya tarehe 08/04 ilikuwa timilifu kwa maana programu zilikuwa updated/zilikuwa salama kwaajili ya kufanya majukumu yake mahususi.
Waheshimiwa majaji baada ya kufanya uhakiki wa vifaa nilifanya uchunguzi wangu wa awali kwa maana ya preliminary examination.
Nilifungua computer yangu maalum kwa maana ya kuiwasha, nilichukua flash disk aina ya XIOXIA kwaajili ya kuifanyia uchunguzi.
Baada ya kufungua computer yangu niliiweka kwenye universal serial bus (USB).
Baada ya kuiweka kwenye USB niliifungua ili kutazama kilichopo ndani ya flash.
Baada ya kuifungua nilikuta ina nywila yaani passwords hivyo niliwasiliana na mamlaka iliyoleta vielelezo kwa ajili ya kupata nywila.
Baada ya kupata nywila niliendelea na uchunguzi wangu wa awali na nilikutana na video mjongeo moja ilikuwa na heading Tundu Lissu uso kwa uso na watia nia majimboni, no reforms no election njia panda.
Na hiyo Video ilikuwa na urefu wa masaa matatu na dakika 38 na ilikuwa katika mfumo wa MP4 file format.
MP4 inatokana na neno MPEG part 14 (kirefu cha MPEG ni Movable Picture Expert Group).
Huyu Bwana Samweli Elibariki Kaaya nae miongoni mwa kitu anatufurahisha hapa Mahakamani ni kujifanya anapenda vingereza fulani kutaja misamiati yake ya kitaalamu.
Sasa anakosea sana kutamka hayo maneno Mh. Lissu kuna muda anauliza mara mbili mbili kuwa umetamka nini?
Akirudia anawaambia tamkeni vizuri jamani kingereza cha wapi hicho, Nafikiri kama Taifa hili swala la kizungu ni ugonjwa mkubwa, inafaa utafutiwe dawa halafu huu ugonjwa kwa mapolisi unaweza kuwa ni mkubwa sana kuliko makundi mengine yote. 😂😂😂
Thawabu Issa: Kingine nini uliona:
Shahidi: Waheshimiwa majaji pia niliona maudhui yafuatayo:
Wanasema hivi msimamo huu unaashiria uasi ni kweli maana tutazuia uchaguzi hivyo tutahamasisha uasi na hiyo ndio namna pekee ya kuapata mabadiliko, tunakwenda kukinukisha sana sana tunaenda kuuvuruga uchaguzi huu, tunaenda kukinukisha vibaya sana.
Waheshimiwa majaji maudhui haya yanapatikana kwenye lisaa la pili na dakika 58.
Pia nilibaini mwendelezo wa matukio kwa maana ya continuity, pia nilibaini jup shoot kwa maana ya kuwa hakukuwa na kukatika kwa picha.
Nilibaini pia necessary or unnecessary movements, kulikuwa na movement za watu mbalimbali au mtu mmoja mmoja kutoka sehemu moja Kwenda sehemu nyingine.
Nilibaini pia uwepo wa rangi halisi na mwanga halisi wa picha mjongeo.
Naomba nifafanue kuhusu rangi na mwanga halisi.
Waheshimiwa majaji unaporekodi picha au picha mjongeo kuna kitu kinaitwa white balance.
White balance kazi yake ni kuseti mwanga na rangi asili ya vitu vinavyorekodiwa.
Hii white balance ina component chache kwa ajili ya kufanya hayo.
Mfano kama unarekodi wakati wa mvua utaiseti camera yako kwenye cloud setting, kama ni kwenye kivuli utaseti camera yako kwenye shadow, kama ni majira ya kawaida ya jua utaseti kamera yako kwenye day.
White balance ilituonyesha kwamba video hii ina mwanga halisi.
Waheshimiwa majaji pia nilitazama mstari mshazari na ninaomba nizungumzie hapa ili pakae sawa.
Katika mizania ya informatics object near the length of the camera is much greator than the object far from the length of the camera.
Mfano mzuri ni mtu anapojipiga selfie, sehemu ya Kichwa itakuwa ni kubwa kuliko sehemu ya miguu ambayo iko mbali na camera.
Kwa maana hiyo waheshimiwa majaji focal length is the basic attribute in this fact.
Part 117 itaendelea kwenye post inayofuata
Naomba Repost yako kwenye tweet hii.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 115
Anaendelea Shahidi namba 3 wa Jamhuri Samuel Elibariki Kaaya
Baada ya hilo kutokea nilienda maabara kwa ajili ya kuandaa vifaa vya uchunguzi.
Barua zote mbili tukianza na ile ya FB/PH/LAB/106/2025 Ilikuwa inahusu jalada la kuchunguza uchapishaji wa taarifa za uongo na lile lenye namba /PH/LAB/107/2025 ikiwa na kosa la uhaini.
Thawabu ; umesema baada ya kuwa assigned ulienda maabara, ieleze mahakama nini ulifanya nini?
Nilifika maabara na kufanya maandalizi ya vifaa vyangu vya uchunguzi.
Maandalizi niliyoyafanya ni kuandaa vifaa chunguzi kwa maana ya computer maalumu kwaajili ya uchunguzi.
Baada ya kumaliza kuandaa computer, printer kwaajili ya uchunguzi.
Tukumbuke kwamba nilikuwa na barua mbili ambazo nilikuwa assigned kuzifanyia kazi hivyo niliamua kusoma barua hizo ili kufaham matakwa ya requesting authority wanataka nini.
Mhe Jaji Barua moja ilikuwa inahusu kuchapisha taarifa za uongo mtandaoni na nyingine ilikuwa inahusu uhaini.
Barua ya uhaini ilikuwa na kumbukumbu namba DA.223/476/01B/169.
Barua hiyo pamoja na muhtasari ilinihitaji kufanya mambo yafuatayo; ilihitaji chanzo cha picha mjongeo inayopatikana kwenye flash disk aina ya XIOXIA, kuchunguza uthibitisho wa uhalisia wa maudhui ya picha mjongeo iliyopo kwenye flash disk, nichunguze chanzo cha picha mjongeo iliyopo kwenye memory card.
Pia nichunguze uhalisia wa maudhui ya picha mjongeo iliyopo kwenye memory card aina ya Aldeepo, kufanya ulinganisho wa maudhui ya picha mjongeo iliyoko kwenye flash disk aina ya XIOXIA kama yanafanana na maudhui ya picha mjongeo iliyokuwepo kwenye memory card aina ya Aldeepo.
Kiuhalisia huyu shahidi anazungumza jambo hilo hilo moja na Wakili wa Serikali anarudia kuuliza swali hilo hilo mara tatu tatu mpaka mtu unaona uvivu kuandika.
Mfano hiyo habari ya video ilisema nini au Mh. Lissu alisema nini kwenye mazungumzo yake na watia nia kwa namna kesi inavyoenda hata sio tatizo na amekuwa hapingi kuwa maneno yale sio yakwake. Swali lake na hoja yake ni kwamba je hayo aliyosema ni kosa kisheria? Ni Uhaini?
Sasa hawa mashahidi watupotezea muda wa siku kadhaa kutuambia namna walivyochunguza video wakati hiyo video mtuhumiwa hana pingamizi nayo. Nafahamu zipo hatua za kisheria zinapaswa kufuatwa ili exhibits zipokelewe Mahakamani lakini kwa shahidi huyu nimewauliza hata Mawakili wanasema kwa kiasi kikubwa wanapoteza tu muda. Mengine hata sio matakwa ya kisheria.
Acha tuendelee nae na tunasubiri muda wa yeye kuanza kuulizwa maswali ya Dodoso na Mshitakiwa ndio tutaelewana zaidi.
Samuel Kaaya: Pia niliambiwa nichunguze maudhui yafuatayo kama yanapatikana kwenye flash disk hiyo, maudhui hayo ni haya;
"wanasema hivi msimamo huu unaashiria uasi, ni kweli kabisa maana tutazuia uchaguzi, hivyo tutahamasisha uasi, hiyo ndio namna ya kupata mabadiliko, tunaenda kukinukisha sana sana, uchaguzi huu tutauvuruga maana tunaenda kukinukisha vibaya sana."
Nilifanya uhakiki wa vifaa vya uchunguzi kwa maana ya computer maalumu kwaajili ya kufanyia uchunguzi huo, printer maalum aina ya Epson, nilikagua program endeshi kwa maana ya operating system window eleven, programu chunguzi kwa maana ya forensic software and security software amped five na ampend authenticate.
Waheshimiwa majaji naomba nieleze maana ya amped five na amped authenticate.
Ampend authenticate inafanya basic and advance image analysis, pia inafanya basic and advance video analysis pia inafanya utambuzi wa sura kwa maana ya facial recognition Waheshimiwa majaji nilitazama pia programu linzi kwa maana ya security software.
Hii programu linzi ni Kaspersky antivirus ambayo kazi yake ni kulinda programu endeshi pamoja na programu zote zilizopo kwenye computer hiyo na pia inalinda vielelezo unavyovipokea visiliwe na virus au malware.
Part 116 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 112
Anaendelea Wakili wa Serikali Thawabu Issa
Hii Meta Data ni nini hasa?
Meta Data ni Data about Data. Yaani picha mjongeo ni Data ndani ya Picha mjongeo kuna Data nyingine ambazo ni taarifa. Hzio taarifa zinaweza kuwa tarehe, jina na kadhalika. Taarifa hizo mjongeo zilizopo kwenye picha mjongeo ndio tunaita Meta Data.
Anasimama Renatus Mkude Wakili Mkuu wa Serikali huyu Baba ni mstaarabu kwakweli. Yeye muonekano wake hana nouma. Anaongea kistaarabu sana. Hana arrogance yoyote. Kwa kumuona tu haoneshi kuwa kisirani kama mawakili wengine wa Serikali.
Anasema kwa sasa ni saa saba naomba tupate break watu wakapate Chakula.
Majaji wanaandika kidogo.
Wanamuuliza Mshitakiwa. Anasema sina pingamizi.
Wanaandika kidogo. Wanasema sasa twendeni break tukutane baada ya lisaa limoja kutoka sasa. Tumeishia hapo kwa sasa. Tukirudi Shahidi ataendeelea kutoa ushahidi wake kwa maana ya EXAMINATION IN CHIEF ITAENDELEA.
Kumbuka jina la Shahidi ni SAMWEL ELIBARIKI KAAYA alkiongozwa na Wakili wa Serikali Thawabu Issa.
Tukutane baadae kidogo.
Naomba Repost yako
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 117
Thawabu: Shahidi uliona nini ulipotazama video uliyokuwa unachunguza kuhusiana na mstari mshazari?
Waheshimiwa majaji nilibaini uwepo wa mstari mshazari kwa maana kuwa picha mjongeo ile ilikuwa ni halisi.
Mwisho wa Ushahidi wa shahidi kuhusu uchunguzi wa awali, sasa anaingia uchunguzi wa kisayansi kuhusu picha mjongeo.
Shahidi anaulizwa baada ya kumaliza uchunguzi wa awali kumalizika ulifanya nini? Waheshimiwa majaji nilifanya uchunguzi wa kisayansi maana uchunguzi wa awali hauwezi kuthibitisha kila kitu.
Hii ni kwasababu huwezi kuthibitsha uchunguzi wa kisayansi kwa kutazama tu lazima uingie kwa ndani.
Katika kufanya uchunguzi wa kisayansi nilifungu application yangu ya amped authenticate nilienda sehemu imeandikwa file na kuna menu ndani inaitwa open, niliielekeza sehemu inayosomeka flash disk XIOXIA.
Niliifungua na baada ya kuiona niliihakiki then baada ya kufungua flash hiyo nili double click picha mjongeo hiyo iliyopo kwenye flash kwaajili ya kuivuta (to export) kwenye amped authenticate interface.
Amped authenticate interface ni pale ambapo the examiner anaweza kuiona video na kuifanyia uchunguzi.
Thawabu : ulifungua nini tuendelee.
Samweli: baada ya kufungua nili click baada ya kufungua nili double click picha mjongeo iliyopo kwenye flash kwa ajili ya kuivuta kwenye Amted Authenticate interface (kuivuta ni export)
Thawabu : Tuendelee
Samweli: Amted authenticate interface ni sehemu ambayo examiner anaweza kuiona video yake na kuifanyia uchunguzi.
Samweli: baada ya kufungua export video yangu nilianza uchunguzi wa kisayansi.
Thawabu: ambapo ulifanya nini?
Samweli: Nilienda moja kwa moja kwenye media info ambayo nini JSOM.
Lengo la kwenda hapo ni kutafuta info za picha mjongeo kwa maana ya meta data.
Baada ha kwenda kwenye JSOM Kutafuta data za kidigitali za picha mjongeo nili screenshot pia nilikuwa na police notebook kwa ajili ya kurekodi kila hatua ninayofanya
Thawabu: Ulichobaini hapo ni nini?
Baada ya kupata taarifa za kidigitali nilibaini picha mjongeo ninayochunguza ni picha iliyopakuliwa kwa maana ya downloaded
Picha iliyopakuliwa kwenye mtandao wa kijamii unaotokana na website au web inayotambulika kwa URL
Thawabu : URL ni ya mtandao gani?
Samweli: youtube
Thawabu: kitu gani kingine uliona?
Samweli: Niliona URL upload ilikuwa ni at jambo Tv.
Pia nilibaini viewers walioona walikuwa takribani 52,406 lakini pia niliona wafuasi kwa maana ya subscribers ambao ilikuwa jumla ya watu 1,010,000.
Pia niliona walio-like kwa maana ya kupenda hayo maudhui walikuwa 578, vingine nitavionyesha nitakapokuwa nawasilisha taarifa yangu ya uchunguzi.
Shahidi anamaliza kueleza kuhusu uchunguzi wa kisayansi sasa anaeleza hatua inayofuata ya clone analysis.
Shahidi anaulizwa baada ya kumaliza uchunguzi wa kisayansi alifanya nini?
Baada ya kumaliza uchunguzi wa kisayansi nilifanya clone analysis.
Waheshimiwa majaji hapa tunaangalia kama kuna pandikizi labda la sura ama sauti. Clone analysis may determine if there is a deep fake.
Waheshimiwa majaji kupitia hiyo menu ya clone analysis inayopatikana kwenye amped authenticate, hii inasaidia to identify sehemu ambazo zimepandikizwa na mtu akiwa anongea itakuwa inaonyesha mark mtu akiwa anaongea ila kwenye video itakuonyesha trace ya maungio kama mtu amevalishwa sura ya mtu mwingine. Mimi nilibaini kuwa picha mjongeo niliyoletewa haikuwa na pandikizi lolote.
Shahidi anamaliza kueleza kuhusu uchunguzi wa clone analysis sasa anaeleza hatua inayofuata ya noise analysis.
Thawabu: tupo kwenye hatua ya noise analysis hebu tuendelee.
Samweli: Kwa mantiki hiyo tunapofanya mambo ya noice analysis ni namna gani kinaweza ku affect hichi kitu kinaitwa pixel
Thawabu Issa: ulibaini kitu gani kwenye noise analysis na pixel?
Samweli: Picha hiyo mjongeo ilirekodiwa day time.
Part 118 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 141
Mhe. Lissu: Ulisema maneno ya kuwa msimamo wetu unaashiria uasi yaanzia dakika 8 kwenye video. Je hayo nayo yapo kwenye maelezo yako Polisi?
Samuel Kaaya : Hayapo.
Mhe. Lissu: Ulisema ukitumia Amped Authenticate inaweza kukusaidia ukajua camera iliyotumika kupiga hizo video?
Samuel Kaaya : Sahihi nilisema.
Mhe. Lissu: Je ulieleza hiyo camera uliyoitaja ilikuwa ni mali ya nani?
Samuel Kaaya : Sijaeleza ilikuwa ni mali ya nani?
Mhe. Lissu: Je umeeleza nani alikuwa anaitumia siku hiyo pale Mikocheni Makao makuu ya Chadema?
Samuel Kaaya : Sijui pia.
Mhe. Lissu: kwahiyo hujui aliyekuwa anapiga picha na aliyekuwa anaimiliki hiyo camera.
Samuel Kaaya : Sijui kiukweli.
Renatus Mkude: Anasimama Mh. Imefika saa saba na dakika tunaomba mapumnziko ya lisaa limoja.
Mhe. Lissu: Naomba niulize la mwisho tu halafu tukapumnzike.
Sasa shahidi swali la mwisho mtu ambae hana password wala username anaweza ku upload video kwenye ukurasa wa Jambo TV?
Samuel Kaaya : Akihuck anaweza kuingia.
Mhe. Lissu: Sasa kwenye mazingira ambayo hakuna Hacking tuhuma zinasema mimi ndio nimeupload hizo video kwenye mtandao wa Jambo TV. Tusaidie kwa ufahamu wako unaelewaje?
Samuel Kaaya : Hakuwa mtu anaweza kuingia kwenye mtandao wa mtu kama hana hizo credentials za kuingilia au ku hack ndio unaweza kuingia.
Mhe. Lissu: kwahiyo ni either una password, password creaker au unafanya Hacking?
Samuel Kaaya : Ni sahihi kabisa.
Mhe. Lissu ; Je mimi nina password?
Samuel Kaaya : Sijasema unazo na sijui pia.
Mhe. Lissu: Password creaker je?
Samuel Kaaya : Sijui na sijasema unayo..
Mhe. Lissu: Je nilifanya Hacking?
Samuel Kaaya : Hukufanya.
Mhe. Lissu: Waheshimiwa Majaji Tukale sasa.
Jaji anasema tutakutana baada ya lisaa limoja na nusu.
Turudi hapa saa nane na nusu.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 125
Kwahiyo kwa kumalizia hoja hiyo ni kwamba shahidi huyu hana Competence ya kutoa hii nyaraka hapa Mahakamani.
Sababu ya nne ni Chain of custody.
Msingi wa hoja hii ni kesi maarufu ya Paulo Maduka na Wenzake 4 vs R Criminal Appeal No. 110 of 2007.
Ushahidi wa aina hii unahitaji uoneshwe kwamba kutoka mahali ulikoanzia mpaka unaletwa Mahakamani.
Kukiwa na break of chain of custody ushahidi haupokelewi.
Shahidi anasema kwenye ushahidi wake aliletewa hizo video na Michael gyumi.
Michael Gyumi alizitoa wapi??
Nakumbuka shahidi wa kwanza alisema ile memory card ilitokea Dodoma kwa mtu anaitwa P akaletewa Andrew churu na alisema kulikuwa na hati ya makabidhiano.
Hiyo hati ya makabidhiano mlileta mahakamani?
Andrew churu alimkabidhi peter Malugala
PW2 John kaaya akasema alimkabidhi Peter Malugala na alijaza PF 45 there is no documentation maana mashahidi hawajaleta hata moja.
Sasa Waheshimiwa kutokana na kesi tajwa hapo juu.
Chain of custody must always be maintained hawa Mapolisi wamemaintain kitu gani? Hakuna lolote.
Hiyo kesi niliyosema ya Paul Maduka
Maana yake ni kwamba Ushahidi wa aina hii unahitaji uonyeshwe kutoka mahali ulipoanzia paka kuletwa mahakamani unahitaji uthibitisho wa kinyaraka umepitia kwenye mikono gani.
Kesi hiyo ya Paul Maduka page 18 to 19 Mr Justice Edwin Rutakangwa anasema kapiga kiingereza hapa kuwa huo mlolongo inabidi usivunjike.
Kwahiyo Waheshimiwa Mahakama ya rufani baada ya Paul Maduka chain of custody should always be maintained it should not be broken.
Waheshimiwa Majaji hata PGO zimesisitiza hilo, Waheshimiwa majaji PGO 229 paragraph 8 inazungumzia Chain of Custody.
Na waheshimiwa Majaji nitawasomea inasema anaanza kusoma hapa anajaribu kuelezea umuhimu wa chain of custody hapa kwamba lazima ionyeshwe kuwa mlolongo wa kupokea kielelzo haujavunjwa au kielelezo kubadilishwa hapa.
Mhe. Lissu anasema kama hakuna chain of custody hakuna Ushahidi wa kuingizwa mahakamani kama hawajaestablish chain of custody hivyo ni rai yangu kuwa msikubali hizi video ziingie kama vielelezo katika mahakama yenu.
Mhe. Lissu amemaliza hivyo ni zamu ya Jamhuri kujibu sasa.
Ni kama wamechanganyikiwa hawaeleweki nani ajibu au wanataka kufanya nini? 😂
Wakili wa Serikali Mkuu Renatus Mkude anasimama na kujibu kuwa wako tayari kujibu hoja za Mh. Lissu lakini watatumia two hours. Majaji wanauliza hiyo two hours unamaanisha nini? 😂😂
Anajibu Wakili Mkude kuwa ni kutokana na hoja za Mshtakiwa alizosema lakini pia shahidi huyo ndo wa muhimu katika mzizi wa kesi hii.
Hivyo tunaomba two hours ili tusilipue katika kuisaidia Mahakama.
Kama itawapendeza tukaahirisha mpaka Jumatatu ni sawa pia Waheshimiwa Majaji.
Mhe. Jaji Ndunguru anasema,
Sasa sikiliza Wakili wa Serikali kimsingi tumeelewa uliposema tu habari ya masaa mawili ulimaanisha unaomba ahirisho hadi Jumatatu.
Mahakama kichekooo 😂😂😂😂
Kumbe hata Majaji wanajua janja janja za Mawakili wa Serikali.
Shauri linaahirishwa hadi Jumatatu saa tatu kamili asubuhi ambayo itakuwa ni Tarehe 20/10/2025.
Tukutane Jumatatu wapendwa,
Sasa ngoja nikanywe wine kidogo nikiwa nakusanya hizo nguvu za Jumatatu.
Mungu awabariki sana.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 139
Mhe. Lissu: Kati ya Mwaka 2021 na 2022 ulihudhuria mafunzo ya Assistant Inspector of Police kule Moshi, sasa kwenye maelezo yako Polisi mambo hayo yapo?
Samuel Kaaya : Sikuyasema.
Mhe. Lissu: Ulisema umesomea medani za kivita na masomo mengine mengi hayo nayo umesema kwenye maelezo yako Polisi?
Samuel Kaaya : Sikusema.
Kwa kifupi huyu shahidi amesema mambo mengi sana hapa Mahakamani ambayo siku anaandika maelezo yake Polisi kuhusu kesi hii hakuyaandika ila hapa Mahakamani ameyasema.
Ndio yale maeneo 75 ambayo Mhe. Lissu ameyasema hapo awali na anaendelea kumuuliza.
Kila kitu anachomuuliza shahidi kwamba ulisema hivi hapa Mahakamani je kwenye maelezo yako yapo? JIBU LA SHAHIDI NI HAPANA, HAYAPO NA SIKUANDIKA.
Yataulizwa maswali mengine ya utofauti wa statement mfano alisema hapa Mahakamani hivi na kwenye maelezo alisema tofauti tutafikia pia hatua hiyo.
Lengo la zoezi hili ni kuonesha shahidi ni muongo na hapaswi kuaminika.
Mhe. Lissu: Je ulisema sana hapa Mahakamani kuhusu mafunzo uliyopata South Africa, Je kwenye maelezo yako yapo?
Samuel Kaaya: Sikuandika kwenye maelezo yangu.
Mhe. Lissu : Ulisoma miezi sita chuoni hapo?
Samuel Kaaya : Sikuandika na hilo pia.
Mhe. Lissu: Anauliza kuhusu chuo cha IFM na Masomo aliyosoma ya kuhusu Uhasibu na Data Management anayosema alisomea na kuzawadiwa shahada ya Sayansi ya Tehama kwenye vyuo mbalimbali je yako wapi kwenye maelezo yake?
Samuel Kaaya : Sikusema.
Mhe. Lissu: Mwaka 2024 ulipata mafunzo katika Chuo Kikuu cha Taifa cha Sayansi ya Jinai. Kule India, Je yako wapi hayo kwenye maelezo yako?
Samuel Kaaya : sikuandika kwenye maelezo yangu, hayapo.
Mhe. Lissu: Ulisema mambo mengi ikiwemo utaratibu wa kuchunguza vielelezo ikiwemo ile kanuni yenu ya first inn first out kama umeuelezea kwenye maelezo yako ya pale Polisi?
Samuel Kaaya : Sikuelezea kabisa.
Mhe. Lissu: Ulisema hapa Mahakamani kuhusu kuwepo na Police Notebook muda wote ili kila unaloliona unarekodi kwenye Polisi Notebook, je hayo yapo kwenye maelezo yako?
Samuel Kaaya : Hayapo
Mhe. Lissu: Hivi nyie Mapolisi nani huwa anawafundisha kuandika maelezo yenu?
Samuel Kaaya : Tunafundishana wenyewe.
Mhe. Lissu: Neno Confimatory test ulifanya, sasa nionyeshe hapo kwenye maelezo yako hiyo confirmatory test ulipoandika.
Samuel Kaaya : Kiukweli Sijaandika hilo neno, halipo.
Mhe. Lissu: Ulisema hapa Mahakamani kuwa unafanya Chron analysis ili kugundua kama kuna Deep Fake yaani teknolojia ya AI imetumika katika video husika je hayo yapo kwenye maelezo yako uliyoandika Polisi?
Samuel Kaaya : Hayapo Sikuandika.
Mhe. Lissu: ulisema habari za kuangalia video kama iko compressed or decompressed nao upo kwenye maelezo yako?
Samuel Kaaya : Haupo.
Mhe. Lissu: Ulisema kuhusu censor pattern analysis na non Uniformity je hayo nayo yapo kwenye maelezo yako ya Polisi?
Samuel Kaaya : Hayapo.
Mhe. Lissu: Ulisema habari za kufanya noise analysis kwenye hiyo video sasa tueleze hayo mambo mengi na utaratibu wa kufanya noise analysis na unaweza kuona vichengachenga kwenye video kama yapo kwenye maelezo yako ya Polisi?
Samuel Kaaya : Hayapo
Mhe. Lissu: Nitakuwa sahihi nikisema huu ushahidi wa maeneo niliyokupitisha ulikuwa ni wa muhimu kwenye kesi hii?
Samuel Kaaya : Ni kweli.
Mhe. Lissu: Na ni kweli ni muhimu kwasababu unaonesha maabara yenu inavyofanya kazi kitaalamu?
Samuel Kaaya : Ni kweli
Mhe. Lissu: kuhusu notebook ni muhimu askari awe nayo muda wote wa uchunguzi hilo nalo ni muhimu?
Samuel Kaaya : Ni muhimu.
Part 140 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 130.
Mhe. Lissu anaendelea kufanya Rejoinder
Anasema Kwenye hoja ya pili bado nasimamia hoja ya pili kwamba video zilipaswa zitamabuliwe na taarifa ya mtaalaamu ambae ni shahidi.
Kesi ya Mirza Katuga anasema ni prosecution plan kuwa prosecution wanapanga nani wakuleta kielelezo.
Hoja nimesema kielelezo kinahusika na utaalamu basi kifuate taratibu za utaalamu.
Hoja ya tatu kuhusu competence ya shahidi vifungu kuanzia vya 216 na kuendelea, kusingekuwa na umuhimu wa sheria kusema wateuliwe.
Kinachofanya wawe wataalaamu sio maneno yao bali ni uteuzi wao.
Katuga anasema shahidi ameonysha utaalamu wake.
Je huyu ni mtaalamu? Ameteuliwa? Kama hajaonesha kuwa ni mtaalamu maneno yake ni kazi bure.
Shahidi huyu amesema kwamba ameteuliwa kwa mujibu kwa gazeti la serikali No. 799/2020 na vilevile amesema ameteuliwa kwa mujibu wa gazeti la serikali no. 745/2020
Hayo magazeti ni Sheria na ni nyaraka za kisheria. Wakili wa Serikali hakusema lolote kuhusu GN. No. 799/2020. Na anasema tusiende huko.
Na mimi nasema lazima twende huko kwasababu ni mtaalamu wa picha na sio mtaalamu wa video.
Wapo wataalamu walioteuliwa na DPP kwa ajili ya video huyu hayupo. The are withholding important information, wanaficha nyaraka muhimu na wakitaka walijibie.
Hii ni sheria ambayo walipaswa kuileta kwenu lakini walikaa kimya ni sheria inayohusiana na ni akina nani ambao ni wataalamu wa kisayansi wa mitandao ambapo wapo kwenye GN. No. 823/2024.
Ukiisoma hii GN wapo 27 hao wataalamu hayupo Samweli Elibariki Kaaya kwenye hiyo orodha.
Majaji wanateta sana hapo kama dakika 10 nadhan wanafikiria Mhe. Lissu aruhusiwe kuitoa hiyo Sheria au haruhusiwi.
Jaji ilikuwa ni haki kwa mshitakiwa kuijibia hoja hiyo maana hata Jamhuri mlituletea maana ya picha mkatuambia kuhusu dictionary.
Kwahiyo mshitakiwa endelelea.
Mhe. Lissu anawasomea hiyo GN hapo juu iliyowataja hao ma experts na anasema kwa kiswahili inaitwa AMRI YA UTEUZI WA WATAALAMU WA KISAYANSI WA MTANDAO aya ya pili ya Tangazo hilo inasema mtu ambae jina lake limetajwa katika jedwali anateuliwa kuwa mtaalamu wa kisayansi wa mtandao katika mashauri yoyote ya jinai na masuala yoyote kama hayo kwa mudhumuni hayo.
Jedwali hilo limeorodhesha watu 27 na huyu shahidi hayumo.
Amesimama Katuga anasema anaanza kutaja majina asifike huko.😂
Katuga hajui kama majina yametajwa kwenye hiyo GN yenyewe.
Huyu mtaalamu wao wamekuja nae mfukoni hayupo kisheria, hajatajwa kwenye tangazo la serikali na hajawahi kuteuliwa.
Jaji anasema hiyo ni sheria sasa kama watu wameandikwa tutaona na tutaona nani yupo na nani hayupo kwahiyo muiachie Mahakama tu.
Waheshimiwa Majaji Sharif Athuman Ukurasa wa 8 Jaji Masatti amesema:
But admissibility of evidence, it is also about the competence of the witness. It is not only about relevance, materiality and...
Jaji amesema competence ya shahidi inaweza kuwa general au specific.
Kwa huyu shahidi ni suala specific kwasababu tunazungumzia mambo ya mitandaoni na shahidi ambae anapaswa kutoa huo ushahidi ni ambae katangazwa kwa kazi hiyo.
Hivyo admissibility ya ushahidi huu inahitaji mtaalamu wa cyber forensic na sio mwingine na nimewapa hapo GN ambayo DPP ameteua watu wake.
Wakili wa Serikali anasema shahidi amesema mengi kuwa yeye ni mtaalamu.
Ni wasilisho langu kuwa kwa vile hayupo kwenye gazeti la Serikali na sio mtaalamu wa chochote huyu shahidi ni wajibu wa Mahakama kujiuliza kwa mujibu wa sheria je huyu ni mtaalamu na ameteuliwa kama nani?
Sayansi ya mtandaoni wameteuliwa yumo?
Kwenye picha za kawaida za makaratasi hilo halibishaniwi hapa, asubiri siku tukiwa na kesi ya makaratasi atakuja.
Haya ya leo ni masuala ya kimtandao.
Kifungu cha 70(1) cha Evidence Act kwamba ushahidi wa kielektroniki unakubalika hata mimi najua hilo ila hoja ni kwamba je anayeleta ushahidi kateuliwa?
Hii ndo hoja ya msingi.
Part 130 itaendelea kwenye post inayofuata
Naomba Repost yako.