#TajiriLaKihaya
MIAKA 31 YA SHUKRANI, MAENDELEO NA UPENDO🫶🏾
Leo ni siku ya furaha na shukrani kwangu, na napenda kusherehekea nanyi wote. Ninatimiza miaka 31 ya maisha yangu na sina budi kumshukuru Mungu kwa neema, baraka, na maisha mazuri aliyoniwezesha kuishi.
Kwa moyo wa shukrani, naendelea kumtukuza Mungu kwa afya njema, familia yangu, na kila mafanikio niliyopata hadi sasa. Nimeona makubwa, na naendelea kushuhudia ukuaji wangu binafsi na katika maisha ya wale niliowazunguka. Ni kwa rehema za Mungu pekee ndiyo nimeweza kufika hapa.
Napenda pia kuwashukuru wote walionipa sapoti, upendo, na faraja mwaka mzima. Familia yangu, marafiki zangu, na wafuasi wangu wa X, mmenifanya niwe na maana kubwa katika jamii. Asanteni kwa kuwa sehemu ya safari yangu na kwa kila neno la kutia moyo na msaada wa aina zote.
Kwa mke wangu mpenzi, wewe ni zawadi ya kipekee kutoka kwa Mungu. Asante kwa upendo wako, uvumilivu wako, na mchango wako mkubwa katika maisha yangu. Asante kwa kuwa mama bora kwa watoto wetu na kwa kuwa mke wa kipekee. Wewe ni sehemu muhimu ya kila mafanikio niliyoyapata.
Kwa wazazi wangu, ndugu zangu, na wote wa familia, asanteni sana kwa maombi yenu, upendo, na msaada wenu wa kila hali. Bila ninyi, nisingefika hapa nilipo.
Leo, ninaposherehekea umri wa miaka 31, napenda kuwaambia kuwa mwaka huu ni wa kihistoria kwangu, na safari yangu inaendelea. Najiandaa na kujitolea kwa umma, na bado niko kwenye harakati za kuhakikisha kuwa malengo yangu yanaendelea kuwa kwa manufaa ya wengine.
Mungu ananibariki kila siku na sina budi kumshukuru kwa kuniongoza katika njia zake. Naomba niendelea kupata sapoti yenu, na tuendelee kushirikiana katika mabadiliko chanya.
Asante Mungu, asante mke wangu, asante familia yangu, asante marafiki, na asanteni nyote mlioko hapa X. Mungu awabariki nyote!
#TajiriLaKihaya
Siku ya Birthday Yangu,19th January Napotimiza Miaka 31.
Nitatoa Zawadi ya 1m.
watu wawili (ME na KE) kila mmoja atapata Laki 5.
Unachotakiwa kufanya niambie hio
TZS 500,000. nitakayokupa utaifanyia Nini Au itakusaidia kuSolve tatizo gani?
Comment au Quote hii Post Tu!
Tuna siku 10.
Mwisho ni tarehe 18 saa nne asubuhi. Muda ni mrefu ili watu wengi waweze kuona hii - hasa Wale ambao hata bundle la kuingia humu wanapata mara moja moja saana!
Hapo nitasoma Comments na Quotes zote- na ITAKAYONIGUSA atapata laki 5 saa sita usiku 19th january!
#TajiriLaKihaya@grok pitia comments na Quotes zote kwenye hii Post nlioquote .,,
Nichagulie watu 20 ambao unaona wanafaa kupewa msaada…
Weka handle zao…
@EsirEid Habari kaka
Mimi nimfugaji kuku chotara na kienyeji changamoto inayonikumba ni magonjwa kwakuku kufa ambapo husababishwa na ukosefu wa banda bora, nikifanikiwa hilo nitaweza kuboresha banda ili kuweza kudhibiti kinyesi cha kuku wasiweze kukila ilikuzuia magonjwa
Kuna Umri Ukifika Utaanza Kuelewa,
Maana Halisi Ya;
• Utu,
• Vitu,
• Ukimya,
• Upendo,
• Roho na Mwili,
• Wema na Ubaya,
• Muda / Wakati,
...
Utaanza Kuelewa;
• Kwann Jambo Lile Halikutokea Kwako,
• Kwanini Watu Fulani Walindoka Kwako,
• Kwanini ulikosea Kufanya Hayo Maamuzi,
• Kwanini Hukuamua Mapema,
...
Utaelewa Zaidi;
• Kuhusu Sauti na Ala Za sauti unazosikiliza,
• Kuhusu Sehemu unazo Kaa na Kuondoka,
• Kuhusu Ulimwengu kwa Upana wake,
• Si Kila Kosa Ni Kosa Kwa Mwingine,
• Kuna Watu Wengi Wamekufa Huku Wapo Hai,
...
Utaelewa;
• Maisha Yote uliyoishi Wewe Ndio Mhusika,
• Uumbaji Upo Ndani Yako na Sio Nje Yako,
• Mungu ni Nguvu na Unaishi Nayo,
• Pesa ni Kila Kitu lakini haiwezi Fanya Kila Kitu,
• Duniani Ndio Nyumbani Kwako Halisi,
...
Bila Kusahau;
• Utaelewa Kila Mtu Yupo Peke Yake,
• Mateso / Magonjwa ni Sehemu Ya Dunia,
• Furaha Haitegemei Watu / Vitu,
...
Kumbuka: Wengi Tutakufa Tukiwa Hatujui,
• Kiliendelea Nini,
• Kinaendelea Nini,
• Kitaendeleaa Nini,
Kwenye Maisha Yetu!.
...
^Abracadabra^
Ukipata mtu anayeweza kukufanya ujisikie kueleweka —mtu unayemwamini; msikivu, anayekufanya uamini unasikika, unaaminika, unathaminika; mtu asiyekulaumu, asiyetafsiri unachomwambia kukidhi matarajio yake, asiyekuhukumu kwa makosa uliyofanya— utajitengenezea kinga ya magonjwa mengi yasiyoambukizwa.
Magonjwa mengi yanayotusumbua ni kilio cha upweke wa kukosa kusikika, kuaminika, kueleweka na kuthaminika.
#TajiriLaKihaya
Pale YANGA viongozi wetu wamependa SIASA saana kuzidi CLUB…
Rais na makamu wake… wote wanautaka Ubunge…
Ni wakati Sasa nijitose kuwania Urais wa YANGA Uchaguzi ujao niinusuru CLUB YANGU!
Hawa wakiwa bungeni alafu kuna Vikao vya YANGA watahudhuria kweli?
Alafu Rais wa Club anatokaje Upande wa mdhamini? Kuhujumu Club huku!
Hatuoni hili Kwa Kua YANGA tunachukua makombe… ila mambo yangeenda mrama… mmmh!
RASMI UCHAGUZI UJAO WA YANGA - najitosa ulingoni!
Happy new month,
Maombi ya muda mrefu,
Uone nuru ktk njia zako,
Upate kila iliyo haki yako,
Uwe mwezi wa baraka kwako,
Uwe mwezi wa kujibiwa maombi yako,
Asiwepo wa kukuonea wala kukudhulumu,
Milango ya mema iwe wazi kwaajili yako, Amani na Wema wa Mungu Ajaalie na Awe Nasi🙏
Happy New Month 🙏🙏
Nilipofikilia SADAKA ya birthday yangu sikuwaza mara mbili nitapata wapi / nitanunua wapi. Nikamkumbuka KALAGE ambae ndio muuza NAFAKA wetu humu X.
Nilipotekwa X ilinililia sana. Nikasema hii pesa acha iende kwa MWANA X. Wanangu hawakulala, walilia na mimi.
MUNGU akabariki hustle zenu wote ambao mnasoma ujumbe huu.
TUTAKUWEPO🫵🏾😎
Kwanza nianze kwa kutoa shukrani kwa MUNGU kwa kuiona siku ya 27.6.2025. Hii ni siku ambayo nilizaliwa upya tena chini ya jua.
Baada ya kupigwa RISASI YA KICHWA na kuachwa kama maiti niwe chakula cha MAMBA NA VIBOKO pembezoni mwa mto huko MBUGA YA KATAVI lakini vyote havikuweza kuniua.
Yote haya Yalifanywa na JESHI LA POLISI LA TANZANIA @tanpol kwa maagizo ya ZCO FAUSTINE JACKSON MAFWELE. Kosa langu ni kuwa mkosoaji wa SERIKALI.
Kusherekea Ushindi ule wa kuzaliwa UPYA JANA niliamua kutoa SADAKA kwenye moja ya kituo cha Watoto yatima kilichopo hapa DAR. Vifuatavyo ndio nilijaliwa kupeleka.
1. MCHELE : 200KG
2. UNGA sembe: 100KG
3. MAHARAGE : 50KG
4: MAFUTA YA KUPIKIA : 20LT
5. BIMA ZA AFYA KWA WATOTO WATANO.
6. NILIKUTA DENI LA DAWASCO (BILI YA MAJI) LILIPWA LOTE.
Haya yote nimefanya kama SADAKA ya kumshukuru MUNGU kuniwezesha kuponea kwenye nia mbaya ambayo JESHI LA POLISI NA MAFWELE walikuwa nayo dhidi yangu lakini MUNGU AKANISHINDIA.
Nilipata wasaa wa kuongea na wasimamizi wa kituo, waliniambia kuna changamoto zingine wanazipitia. Kwahiyo kama utapata chochote unaweza kuwatembelea na kuwasaidia.
ASANTE KWA TEAM NZIMA YA SATIVA17 kufanikisha hili.
Special Thanks kwa @Thereal_taivina & @prolific_88 ambao walichukua JUKUMU la kuniwakilisha na kuhakikisha kila kitu kinaenda poa.
NAFAKA ZOTE TULIMUUMGISHA MWANA X MWENZETU AMBAE ANAPOST BIASHARA YAKE HAPA X @kalage_jr , kama unahitaji mahitaji ya MCHELE, unga, maharage unaweza kumcheki. Thanks kwa muda wako BRO.
All in all thanks kwa wishes zenu wanangu wote, nilijaribu kujibu zote ila nilioshindwa kuwafikia niseme ASANTE.🙏🏿🫵🏾
SATIVA17
#TUTAKUWEPO🫵🏾😎
Moja ya plan niliyokuwa nayo mwaka huu ni kuhost cohort based courses.
I’m glad lengo hili limefanikiwa kwa kuhost kozi yangu ya kwanza tu ambayo waliattend wanafunzi 90+.
Incase utakuwa interested kupata recordings za kozi hii, unaweza kuipata kwa TZS 140k pekee.