#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 270
Mhe. Lissu anaendelea kutoa utetezi wake.
Anasema baada ya Magufuli na Samia kuingia 2015 Kazi waliyoifanya ndo imetuleta leo hapa mpaka nimepewa kesi ya Uhaini.
Sikusema Ijumaa kuwa 2020 nilirudi kutoka uhamishoni kutoka Ubelgiji kuja kumkabili Magufuli ni wazi sikuchaguliwa lakini ningechaguliwa, nisingekuwa hapa.
Baada ya matokeo ya Uchaguzi Tume itapaswa kuchapisha matokeo ya jimbo kwa jimbo.
Ukiangalia chaguzi za kabla ya mwaka 2020 Tume huwa zina gazette matokeo yote jimbo kwa jimbo na Kata kwa kata nchi nzima.
Ya Ubunge Jimbo kwa Jimbo nchi nzima lakini ya Urais huwezi kuona kokote kule.
The results were never gazetted na sheria inasema baada ya miezi 6 yatachomwa moto. Hatutakuja kujua Magufuli alipata kura ngapi? Kwanini? kwasababu Tume ni ya KiCCM.
Toka mwaka 1995 wagombea wa upinzani wameenguliwa kila mwaka.
Toka mwaka 1995 na uchaguzi wa 2020 ndo ulitia fora, Wabunge wa majimbo 28 walipita bila kupingwa, aliyeengua ni Mkurugenzi wa Uchaguzi ambae kwa sasa ni mbunge wa CCM.
2020 kwenye General Election ilikuwa ni mass disqualification walioenguliwa ubunge walikuwa 63 kati ya 244 tukapambana nao sana.
Madiwani 832 walienguliwa na kwa mara nyingine kukawa na mauaji sana.
Sasa Waheshimiwa Majaji ukisoma taarifa za watazamaji wa kimataifa walisema uchaguzi sio wa huru na haki na CCM inapendelewa. Uchaguzi ulikuwa na fujo na sisi huwa tunapigwa na Mapolisi na sio wanaCCM, watu wetu wanatekwa na Mapolisi sio wanaCCM.
Kwenye hotuba yangu ninaposema polisi wanatembea na vibegi mgomboni vimejaa kura. That is the truth of our heart, hakuna uongo.
Samia anasema tuliwapiga fix tukawaengua. Samia anasema hivyo kwenye ripoti.
Watazamaji wakasema bila mabadiliko ya Uchaguzi kutakuwa na maafa mwaka 2025. Ripoti ya watazamaji wa Umoja wa Afrika kuwa kuna haja ya kuwa na mabadiliko ya Sheria za Uchaguzi.
CCM walisema Katiba haitaleta Chakula nyumbani sisi tukasema hapana tutapigania Katiba Mpya, wakamkamata Mbowe na kukaa jela miezi 8 kwa kesi ya uwongo ya Ugaidi na waendesha mashitaka ni hawa hawa.
Waliposema ajiteteee waka enter nolle hakujitetea tukashtukia yuko Ikulu. Nasikia jana AMEIBUKIA BWAWA LA MWALIMU NYERERE, MWENYEKITI WAKE YUKO JELA YEYE ANAIBUKIA HUKO YUKO NA MAMA.
Watu wanacheka kwa maumivu huku ndani.
Anasimama Wakili wa Serikali Ajuaye anasema Muda umeisha twende Mapumnziko tafadhali. Twende lisaa limoja.
Jaji sasa tukirudi utamaliza.
Mhe. Lissu hapana nafikiri tutaenda enda vizuri niachieni tu niende.
Kesi inaahirishwa baada ya lisaa tutarudi.
Naomba Repost yako.