"Wanawake wengi ni nguvu kazi katika sekta ya kilimo, wengine vijana wametoka vyuoni, wengi wanashindwa kukopesheka kwa sababu ya kukosa dhamana, niwatie shime watanzania, serikali ya awamu ya 6 imetuongezea mataji katika mfuko wa dhamana, waende Exim bank kukopa" - @FNyabundege
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kikao cha kuwasilisha taarifa ya mwaka mbele ya Msajili wa hazina ndugu Nehemia Mchechu, Mkurugenzi wa benki ya TADB @FNyabundege amesema thamani za mali za benki zimekua kutoka shilingi bilioni 448 hadi shilingi bilioni 647.
"Mwaka 2023-24 serikali imeipatia benki ya TADB mtaji wa shilingi bilioni 170 ili tuweze kuwafikia wananchi wengi zaidi, benki yetu ni benki ya maendeleo, tunaendelea kukua ili tuweze kuleta maendeleo katika sekta za kilimo, mifugo na uvuvi nchini" - @FNyabundege
🐂 🏦 Mkurugenzi mwendeshaji wa benki ya maendeleo ya kilimo @tadbtz Bw. Frank Nyabundege @FNyabundege amekipongeza Chama cha wafugaji wa ng'ombe kibiashara TCCS kwa kuandaa maonesho ya mifugo na mnada na kuahidi kuwa TADB itaendelea kuwa mdhamini mkuu wa maonesho hayo. #TADB🇹🇿
Nawatakia nyote kheri ya Miaka 62 ya Uhuru wa Tanzania Bara. Tumshukuru Mwenyezi Mungu kwa hatua hii kubwa kwa nchi yetu na kuwaombea viongozi waliotangulia mbele ya haki ambao walikuwa mstari wa mbele katika kupigania uhuru wetu.
Miaka hii 62 ya ujenzi wa Taifa letu inatupa kipimo cha kufanya tathmini ya tulikotoka, tulipo na pale ambapo tunakusudia kufika. Tumepiga hatua kubwa za maendeleo katika kila sekta. Tumefanikiwa kuendelea kutunza amani, umoja na mshikamano wa taifa letu ambayo ni chachu kubwa ya maendeleo yetu. Tujipongeze. Tusonge mbele.
Ujenzi wa nchi ni suala endelevu. Mafanikio tuliyonayo leo ni matokeo ya uongozi thabiti, maono na kazi ya viongozi wetu walionitangulia. Nawashukuru na kuwapongeza Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere, Mzee Ali Hassan Mwinyi, Hayati Benjamin Mkapa, Mzee Jakaya Kikwete na Hayati Dkt. John Magufuli. Ahadi yangu ni kuendeleza mema yote waliyoiletea nchi yetu na kujifunza kutokana na changamoto walizokutana nazo, ili kuendelea kuifanya vyema kazi ya kuitumikia nchi yetu na watu wake.
Benki ya maendeleo ya kilimo @tadbtz imethubutu kuwafikia wafugaji wa kimasai ambao walionekana kuachwa na huduma za kifedha(mikopo) na benki nyingine. Baada ya TADB kuingia katika sekta ya mifugo; mikopo imewawezesha pia wafugaji kuanza kufuga kisasa.🐂🇹🇿 | Cc: @FNyabundege
Taarifa sahihi ni kuwa Wizara ya Kilimo imewakilishwa na wajumbe WATANO tu ambao ni Waziri wa Kilimo, Mheshimiwa Hussein Bashe (Mb) pamoja na wataalaam wanne ambao ni Mchumi, mtaalamu wa Mawasiliano, mtaalamu wa Masoko na mtaalamu wa Mazingira.
TADB, BoT wazindua programu ya mafunzo ya kuboresha ukopeshaji katika sekta ya Kilimo
TADB kwa kushirikiana na Chuo cha Mafunzo cha Benki Kuu (BoT Academy) wamezindua programu ya udhibiti wa wataalamu wa ukopeshaji sekta ya kilimo katika Ofisi ndogo ya BoT, Dar Es Salaam.
Naibu Gavana, Bi. Sauda Msemo, leo katika Ofisi za BoT Dar es Salaam, amezindua Programu ya Ithibati ya Huduma za Kifedha( Certified Professional in Agricultural Finance) inayolenga kuwajengea uwezo wadau wa Sekta ya Kilimo kupitia elimu ya Huduma za Fedha katika sekta hiyo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Waziri Mkuu wa India Mhe. Narendra Modi mara baada ya kuwasili Ikulu ya India (Rashtrapati Bhawan) New Delhi nchini humo tarehe 09 Oktoba, 2023.
Heri ya miaka 73 ya kuzaliwa Mheshimiwa Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete. Ahsante kwa utumishi wako kwa umma wa zaidi ya miaka 50 kwenye Chama Cha Mapinduzi, Jeshi la Wananchi wa Tanzania, na baadaye kama Rais wa nchi yetu. Nakutakia afya njema na wakati mwema unapokumbuka siku hii.
MIKOPO YA KILIMO
"Idadi ya mikopo imekuwa ikipanda; tulikuwa na mikopo ya Sh. Bil 110; hadi kufikia Juni 30, 2023 tulikuwa na jumla ya mikopo ya Sh. Bil 317 na tunaamini hadi kufikia mwezi Desemba mwaka huu itaongezeka zaidi” -@FNyabundege mkurugenzi @tadbtz#MamaYukoKazini
Kheri ya Wiki Mpya
Kusini Kilimo Kina Benkika!
📍Lindi📍Mtwara📍Ruvuma
Tembelea ofisi zetu Jengo la Raha Leo Mtwara mjini karibu na ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa mikopo ya kilimo, uvumi na ufugaji.
#TADB#KilimoKinaBenkika#Mtwara#Lindi#Ruvuma
Bajeti 2023/2024: Serikali kuiongezea mtaji TADB
Hayo yamesemwa na Mhe.Dkt. Waziri Nchemba alipokuwa akiwasilisha Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2023/2024 Bungeni, Dodoma.
Ahsante Mama,
Kazi iendelee!
#TADB#KilimoKinaBenkika#KilimoNiBiashara
Mkurugenzi Mtendaji @tadbtz@franknyabundege amekutana na Makamu wa Rais wa @afdb_group anaeshughulikia Sekta ya Kilimo, Maendeleo ya Kibinadamu na Kijamii Dkt. @beth_dunford kuzungumzia ushiriano baina ya taasisi hizi mbili katika kilimo, mifugo na uvuvi.
#kilimoUshirikiano
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb) na Naibu Waziri wake, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb) (katikati), wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Wizara hiyo pamoja na Taasisi zake baada ya Bunge kupitisha Bajeti ya Mafungu (9) ya Wizara ya Fedha na Mipango yenye jumla ya shilingi trilioni 15.94 pamoja na Fungu 45 – Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi (CAG), yenye jumla ya shilingi bilioni 97.13, kwa mwaka wa fedha 2023/24.