Tafiti za Kisayansi zinaonesha kuwa Mtoto wa Kiume anaweza kuanza kuwa na uume ulio simama (Erection) akiwa tumboni mwa mama. Hili hutokea kama sehemu ya ukuaji wa kawaida wa mfumo wa Uzazi wa Kiume.
Kwa mujibu wa watafiti, hali hii inaweza kuonekana kupitia Uchunguzi wa Ultrasound, hasa kuanzia wiki ya 16 ya Ujauzito na kuendelea. Ni sehemu ya maendeleo ya mwili na mfumo wa fahamu, na haimaanishi msukumo wa hisia za kingono. Badala yake, ni mwitikio wa kawaida wa mwili unaotokana na ukuaji wa Homoni na mzunguko wa damu kwenye viungo vya Uzazi.
Kwa hivyo, kusimama kwa uume kwa mtoto tumboni ni sehemu ya mchakato wa Asili wa ukuaji na hakuna jambo la kushangaza au la kuogopesha kuhusu hili