Baada ya Mamlaka za Angola kutuzuia kwa muda wa takriban Saa Nane (8) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Quatro de Fevereiro wa Luanda, Jana Machi 13, 2025, Mimi pamoja na Viongozi wengine Mashuhuri wakiwemo Marais Wastaafu kutoka Botswana na Colombia, Waziri Mkuu Mstaafu wa Lesotho, na baadhi ya Wakuu wa Vyama vya Siasa kutoka Mataifa mbali mbali, Barani Afrika na kwengineko Ulimwenguni; hatimaye Majira ya Saa Nne (4.00) Usiku tuliachiliwa huru na kupelekwa katika Hoteli ambazo tulipangiwa, huku tukiwa na machofu.
Wakati hayo yakitokea, nlikuwa nimeambatana na Balozi wa Tanzania Nchini Zambia Luteni Jenerali Matthew Edward Mkingule, ambaye pia anaiwakilisha Tanzania nchini Angola.
Kitendo hiki cha aibu kidiplomasia kilichotekelezwa na Namlaka za Angola, hakikuwa na sababu hata kidogo, na kimetia doa dhana ya Umoja wa Afrika, tena katika wakati ambao Rais wa Angola ndiye Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU).
Hiki ni Kitendo ambacho Kinapaswa kulaaniwa vikali na Waafrika wote, na Watu wengine Duniani, wanaothamini na kutukuza Misimgi ya Udugu iliyowekwa na Viongozi Waasisi Waliopigania Uhuru wa Bara hili.
Hata hivyo, napenda niweke wazi kwamba pamoja na kukerwa na kuchukizwa na yaliyotendwa dhidi yetu, sina kinyongo na Raia Wema wa Taifa hili jema, ambalo Tanzania tumekuwa na mahusiano mema ya kihistoria na madhubuti kwa muda mrefu.
Baada ya kuzingatia tukio la Jana, nimeamua kutoshiriki katika Mkutano Muhimu nilioalikwa, wa Jukwaa la Demokrasia Afrika, na badala yake ninarejea Tanzania.
Naamini nahitaji muda wa kufanya tafakuri ya kina na kutathmini kile kilichotendwa dhidi yetu, ambacho kilikuwa ni shambulio dhidi ya Diplomasia na Demokrasia ndani ya Afrika.
Ahsanteni sana!
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar ambaye pia ni Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Taifa, Othman Masoud Othman amesema kuwa kitendo cha yeye pamoja na viongozi mbalimbali kuzuiliwa kuingia Angola kushiriki Mkutano wa Jukwaa la Demokrasia Afrika, kumetia doa dhana ya Umoja wa Afrika.
"Baada ya Mamlaka za Angola kutuzuia kwa muda wa takriban Saa Nane (8) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Quatro de Fevereiro wa Luanda, Jana Machi 13, 2025, Mimi pamoja na Viongozi wengine Mashuhuri wakiwemo Marais Wastaafu kutoka Botswana na Colombia, Waziri Mkuu Mstaafu wa Lesotho, na baadhi ya Wakuu wa Vyama vya Siasa kutoka Mataifa mbali mbali, Barani Afrika na kwengineko Ulimwenguni; hatimaye Majira ya Saa Nne (4.00) Usiku tuliachiliwa huru na kupelekwa katika Hoteli ambazo tulipangiwa, huku tukiwa na machofu.
Wakati hayo yakitokea, nlikuwa nimeambatana na Balozi wa Tanzania Nchini Zambia Luteni Jenerali Matthew Edward Mkingule, ambaye pia anaiwakilisha Tanzania nchini Angola.
Kitendo hiki cha aibu kidiplomasia kilichotekelezwa na Namlaka za Angola, hakikuwa na sababu hata kidogo, na kimetia doa dhana ya Umoja wa Afrika, tena katika wakati ambao Rais wa Angola ndiye Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU).
Hiki ni Kitendo ambacho Kinapaswa kulaaniwa vikali na Waafrika wote, na Watu wengine Duniani, wanaothamini na kutukuza Misimgi ya Udugu iliyowekwa na Viongozi Waasisi Waliopigania Uhuru wa Bara hili.
Hata hivyo, napenda niweke wazi kwamba pamoja na kukerwa na kuchukizwa na yaliyotendwa dhidi yetu, sina kinyongo na Raia Wema wa Taifa hili jema, ambalo Tanzania tumekuwa na mahusiano mema ya kihistoria na madhubuti kwa muda mrefu.
Baada ya kuzingatia tukio la Jana, nimeamua kutoshiriki katika Mkutano Muhimu nilioalikwa, wa Jukwaa la Demokrasia Afrika, na badala yake ninarejea Tanzania.
Naamini nahitaji muda wa kufanya tafakuri ya kina na kutathmini kile kilichotendwa dhidi yetu, ambacho kilikuwa ni shambulio dhidi ya Diplomasia na Demokrasia ndani ya Afrika.
Ahsanteni sana!"
Ameandika Mwenyekiti wa Chama cha ACT wazalendo @ACTwazalendo Taifa ambaye ni makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud Othman kupitia ukurasa wake wa X, leo Machi 14,2025.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama cha ACT Wazalendo Taifa, Othman Masoud Othman (OMO), ameeleza kusikitishwa na kitendo cha kuzuiwa kwa muda wa saa nane katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Quatro de Fevereiro, Luanda, nchini Angola.
Kwa mujibu wa taarifa yake rasmi iliyotolewa Machi 14, 2025 na Kitengo cha Habari, Ofisi ya Makamu wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud alizuiwa akiwa pamoja na viongozi wengine mashuhuri, wakiwemo marais wastaafu kutoka Botswana na Colombia, Waziri Mkuu mstaafu wa Lesotho, pamoja na wakuu wa vyama vya siasa kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika na duniani.
Tukio hilo, ambalo limetajwa kuwa aibu kwa diplomasia ya Afrika, lilitokea licha ya uwepo wa Balozi wa Tanzania nchini Zambia, Luteni Jenerali Matthew Edward Mkingule, ambaye pia anawakilisha Tanzania nchini Angola.
Othman Masoud amelaani kitendo hicho, akikitaja kuwa kimeweka doa kwa Umoja wa Afrika (AU), hasa ikizingatiwa kuwa Rais wa Angola ndiye Mwenyekiti wa umoja huo kwa sasa.
"Kuzuiwa kwetu bila sababu yoyote ni shambulio dhidi ya diplomasia na demokrasia ndani ya Afrika," amesema Othman. "Hiki ni kitendo kinachopaswa kulaaniwa vikali na Waafrika wote wanaothamini misingi ya udugu iliyowekwa na viongozi waasisi wa bara letu."
Hata hivyo, amesema hana kinyongo na raia wa Angola, akisisitiza kuwa Tanzania imekuwa na uhusiano wa kihistoria na taifa hilo kwa muda mrefu.
Kutokana na tukio hilo, Othman Masoud amesema ameamua kutoshiriki katika mkutano wa Jukwaa la Demokrasia Afrika, ambao alialikwa kuhudhuria nchini Angola. Badala yake, atarejea Tanzania kwa ajili ya kufanya tafakuri na kutathmini hatua zilizochukuliwa dhidi yao.
Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo pia Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Othaman Masoud Othoman (OMO), ameeleze adha walizopata wakati wamezuiliwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Luanda nchini Angalo.
OMO aliyechapisha kupitia ukurasa wake wa 'X' leo tarehe 14 Machi 2025 , amesema kuwa Mamlaka za Angola ziliwaachia saa nne usiku wakiwa wamechoka.
"Baada ya Mamlaka za Angola kutuzuia kwa muda wa takriban Saa Nane (8) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Quatro de Fevereiro wa Luanda, Jana Machi 13, 2025, Mimi pamoja na Viongozi wengine Mashuhuri wakiwemo Marais Wastaafu kutoka Botswana na Colombia, Waziri Mkuu Mstaafu wa Lesotho, na baadhi ya Wakuu wa Vyama vya Siasa kutoka Mataifa mbali mbali, Barani Afrika na kwengineko Ulimwenguni; hatimaye Majira ya Saa Nne (4.00) Usiku tuliachiliwa huru na kupelekwa katika Hoteli ambazo tulipangiwa, huku tukiwa na machofu." ameandika OMO.
OMO ameandika kuwa mkasa huo haujawakuta viongozi wa upinzani pekee yao hata Balozi wa Tanzania nchini Zambia aliyekuwa kwenye msafara huo .
"Wakati hayo yakitokea, nlikuwa nimeambatana na Balozi wa Tanzania Nchini Zambia Luteni Jenerali Matthew Edward Mkingule, ambaye pia anaiwakilisha Tanzania nchini Angola" ameandika OMO.
OMO amekilezea kitendo hicho kuwa ni cha aibu katika mawanda ya uhusiano wa kidiplomasia"Kitendo hiki cha aibu kidiplomasia kilichotekelezwa na mamlaka za Angola, hakikuwa na sababu hata kidogo, na kimetia doa dhana ya Umoja wa Afrika, tena katika wakati ambao Rais wa Angola ndiye Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU)".
"Hiki ni Kitendo ambacho Kinapaswa kulaaniwa vikali na Waafrika wote, na Watu wengine Duniani, wanaothamini na kutukuza Misimgi ya Udugu iliyowekwa na Viongozi Waasisi Waliopigania Uhuru wa Bara hili" ameandika.
OMO ameweka wazi kuwa pamoja na kuchukizwa na kitendo hicho lakini moyoni mwake hana kinyongo na wananchi wa taifa hilo kwa kuwa uhusiano wa kirafiki wa raia wa mataifa hayo haujawahi kuwa na dosari.
OMO amesema kuwa leo ameamua kurejea nchini Tanzania na kwamba hana mpango wa kuendelea kushiriki Kongamano la Jukwaa la Demokrasia lililotarajiwa lianze leo nchini Angola.
Chama cha ACT Wazalendo kimesema Kiongozi wa Chama hicho Dorothy Jonas Semu akiwa ameambatana na Naibu Katibu wa Mambo ya Nje ACT, Nasra Nassor Omar na Katibu wa Haki za Binadamu Pavu Juma Abdalla wamerejea nchini Tanzania saa 9:40 usiku wa kuamkia leo March 14, 2025 baada ya kuzuiwa kuingia nchini Angola.
Taarifa iliyotolewa na Katibu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa ACT, Mwanaisha Mndeme leo March 14,2025 imesema “Kwa upande wake, Mwenyekiti wa ACT ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud Othman bado yupo Jijini Luanda nchini Angola kwa ajili ya kukamilisha taratibu za usafiri kurejea nyumbani Tanzania, Chama kitaendelea
kutoa taarifa mara kwa mara kwa umma juu ya maendeleo ya suala hili”
“Chama cha ACT Wazalendo kimesikitishwa na ukimya wa Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kulikalia kimya suala hili, ni jambo linaloshangaza na kusikitisha kwa Serikali ya Tanzania kushindwa kutoa kauli yoyote dhidi ya kitendo hiki kinachokiuka taratibu za kidiplomasia, ari ya mshikamano wa Afrika na undugu wa kihistoria baina ya Tanzania na Angola, tunaitaka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki itoke hadharani na kufafanua kilichotokea Angola na msimamo wa Serikali juu ya hilo, tunarejea rai yetu ya kuitaka Serikali kumuita mara moja Balozi wa Angola nchini Tanzania kujieleza kuhusu kilichotokea kwa Viongozi wetu nchini Angola”
Viongozi hao waliwasili Angola kushiriki mazungumzo ya Jukwaa la Demokrasia Afrika The Platform for African Democrats (PAD) yaliyoandaliwa na Taasisi ya The Brenthurst Foundation yaliyopangwa kufanyika kuanzia jana March 13-16, 2025 ambapo mbali na Viongozi hao, Viongozi wengine zaidi ya 40 kutoka nchi mbalimbali Afrika ambao pia walikuwa wanahudhuria mkutano huo wamezuiliwa na Serikali ya Angola akiwemo Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu na Viongozi wengine wa CHADEMA.
#MillardAyoUPDATES
After being detained for eight exhaustive hours by the authorities in Angola at the Quatro de Fevereiro Luanda International Airport, I, together with other dignitaries who included former Presidents of Botswana and Colombia, former Prime Minister of Lesotho, and other national leaders of political parties from across Africa and beyond, were finally released and allowed to go to our allocated hotels late night yesterday.
This horrendous move by the Angolan authorities was completely uncalled for and has stained the spirit of African unity at a time when the President of Angola is chairing the @_AfricanUnion . It must be condemned in the strongest and unequivocal terms by fellow Africans who cherish and value the ideals of brotherhood as set out by our founding fathers.
I must however make it clear that I harbour no grudges against the great people of this great country with which Tanzania shares a long and chequered history and relationship.
Taking into consideration what happened yesterday, I have decided that I will not attend the Platform for African Democrats conference that I was invited to, and instead I will be going back to Tanzania. I believe I need time to reflect and take stock of what was done to us which was a fatal attack on diplomacy and democracy in the continent.
Nimerudi salama nyumbani nikijivunia nyongeza ya uzoefu wa Luanda. Hakuna kurudi nyuma!Tuhakikishe kwamba vyama makini ndani ya nchi tupo pamoja katika kudai masuala ya msingi kwa watu wetu na wana demokrasia wa Afrika tunaunganisha nguvu na mashirikiano. Aluta Continua!
#Video: Mhe. Othman Masoud Othman akitoka katika eneo la Uwanja wa ndege wa Luanda, nchini #Angola usiku wa Machi 13, 2025. Kwenye video hii anaonekana pia Mhe. Tundu Lissu.
UKIMYA WA TANZANIA HAUKUBALIKI
"Tunaitaka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki itoke hadharani na kufafanua kilichotokea Angola na msimamo wa Serikali juu ya hilo ikizingatiwa kuwa miongoni mwa viongozi waandamizi waliokumbwa na kadhia hiyo yumo pia Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar."
Katibu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa @ACTwazalendo@Mwanaishamndeme
#TaifaLaWote #MaslahiYaWote
Chama cha ACT Wazalendo kimetoa taarifa maalumu inayoeleza kuzuiliwa kwa msafara wa viongozi wake nchini Angola walioenda kwa ajili ya mazungumzo na Jukwaa la Demokrasia Afrika yaliyopangwa kufanyika kuanzia tarehe 13-16 Machi 2025.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa viongozi hao wameshikiliwa katika uwanja wa ndege wa Luanda, nchini Angola. ACT imelaank kwa nguvu kitendo hicho wakati Kamati ya Uongozi Taifa ikikutana kwa dharura kutafakari juu ya mkasa huo na hatua muafaka za kuchukuliwa.
#CrownMedia #HapaNiNyumbani
Zaidi ya masaa 20 ya kusafiri kutoka Afrika- Dar es Salaam kuelekea Afrika- Benguela, Angola. Sikuiona Benguela bali nimeendelea nimeyashuhudia ya Afrika. Ndani ya masaa hayo nimepokwa hati yangu ya kusafiria kwa maelezo kuwa mamlaka ya Uhamiaji ya Angola imenizuia nisiingie nchini humo.
WATCH: “What happened to me today was something I never expected" - Former President, Ian Khama, following reports that he was denied entry into Angola this evening.
Angolan immigration authorities are holding up and denying entry into Angola for me and a delegation of more than twenty senior leaders and representatives of political parties from across southern Africa who arrived in Luanda earlier today for a planned two day meeting.
The group includes a sitting First Vice President from Tanzania; a former President of Botswana; a former Prime Minister of Lesotho and a host of senior political leaders and delegates from Kenya, Sudan, Tanzania, South Africa, Namibia, Eswatini, Lesotho, Germany, USA, Uganda, DRC and Mozambique.
Angolans and Tanzanians are a brotherly people. Tanzania hosted Dr. Antonio Agostinho Neto and his MPLA fighters in the early years of their independence struggle. We supported Angola through thick and thin during the apartheid South African regime's occupation of Southern Angola in the '70s and '80s.
Like Angola, Tanzania is a SADC member state and, as such, we Tanzanians don't need visa to enter Angola.
This shabby treatment of the nationals of brotherly African nations by the Angolan immigration authorities is totally unacceptable and should be condemned in the strongest possible terms.