Ombwe lina tabia ya kumshughulisha mtu. Ukiwa na ombwe, mfano huna kitu kikubwa cha maana unachopambania zaidi ya sifa nyepesi nyepesi, unajiweka kwenye hatari ya kuteketeza muda na nguvu nyingi kwenye ubobezi wa mambo yasiyo na maana—majoring in minor things.
Kwa ngazi ya maisha binafsi mtu mzima na ombwe lako unaaga asubuhi unaenda kazini lakini huko uliko nguvu zote unazielekeza kwenye AOB —‘mambo mepesi yanayojitokeza.’ Ikitokea ukabahatika kuwa kiongozi wa taasisi ndio kabisa unakuwa mbobezi kwenye shughuli zinazowashughulisha watu na haziwasaidii.
“Kumtafutia mtu kazi sio kumtumia tangazo la kazi aombe bali ni kumwambia tarehe flani aende kwenye interview au apeleke vyeti Jumatatu aanze kazi”
Sijui nani aliandika hii tweet ila aliandika ukweli.
Tangu 'Siri ya Mtungi' itoke, hakuna TV show ya Bongo iliyofika level yake. Kuanzia ubora wa sauti, machaguo ya location, mpaka uhalisia wa story vilikuwa ni top notch.