Utawala unapaswa kuwa na hela na ndo maana kila siku nasema Mungu abariki wanaume wote pesa. Yani pesa ni muhimu sana mwanaume kuwa nayo
Ni maombi yangu leo wanaume wote mbarikiwe na kufunguliwa milango ya kifedha🙏
Watu watakuhukumu.
Wengine watakutazama na kupata inspiration.
Lakini mwisho wa siku, hakuna hata mmoja wao anayelipa bili zako.
Ishi maisha yako, Sali Zaidi, Fanya yako.
Moja ya mambo nimejifunza in a hard way, ni nadra watu kuhahirisha mambo yao kukusaidia.
You will be there starving, wakati Kaka yako anamalizia ujenzi wa apartment na anasema hana hela, na hakuna kitu utamfanya, ni hela yake.
Just survive to treat people the same 😆😆
TUJIELIMISHE ILI KUJISAHIHISHA.
KESI YA LISSU: HAKUSHINDWA BALI MAHAKAMA ILIAMUA KUWA ANA KESI YA KUJIBU HIVYO UTETEZI UNAFUATA.
Pamoja na kuheshimu uamuzi wa Mahakama, mimi ninaendelea kuhimiza busara na hekima zitumike katika ngazi zote za maamuzi ili taifa letu liondokane na jambo hili la kusikitisha. Tuweze kuambizana ukweli, kusameheana na kuridhiana.
Sizungumzii hatia au kutokuwa na hatia kwa Lissu; hilo ni jukumu la Mahakama. Ninazungumzia mazingira ya kesi hii, historia yetu na umuhimu wa sheria kutumika kwa usawa. Tutambue:
1. Kesi ya Tundu Lissu ina tofauti kubwa na kesi nyingi za uhaini zilizowahi kutangulia hapa nchini. Katika kesi hizo za kihistoria kulidaiwa kuwepo njama, washirika, mipango ya pamoja ya kuipindua Serikali, na katika baadhi ya kesi washirika kutoka jeshini na madai ya kupanga kumuua Rais.
Katika kesi hii Lissu ameshtakiwa peke yake, na kiini cha shtaka kinahusu kauli zake za hadharani. Hii ni tofauti muhimu inayostahili kutafakariwa bila kuingilia kazi ya Mahakama.
2. Lissu anashitakiwa kwa uhaini chini ya kifungu cha 39(2)(d) cha Kanuni ya Adhabu, kutokana na kauli alizotoa katika mkutano wa CHADEMA tarehe 3 Aprili 2025. Kaulimbiu yake ilikuwa “No Reforms, No Election.” Upande wa mashtaka unadai kwamba kauli zake kuhusu “kukinukisha”, kuzuia au kuvuruga uchaguzi zilivuka mipaka ya siasa za kawaida.
Kauli hizo ni kali. Lakini katika historia ya siasa zetu tumewahi pia kusikia kauli kali zaidi. Mfano wimbo maarufu: “Wapinzani tuwashike, tuwachanechane, tuwatupe.”
Hata Bungeni wimbo huo uliwahi kulalamikiwa lakini ikachukuliwa ni utani wetu wa jadi. Pia mitandaoni leo tunasikia kauli za kutishia watu, kuwaua au kuwapoteza bila hatua zinazoonekana kuchukuliwa kwa kiwango sawa.
Ndiyo maana wapo wananchi wanaojiuliza: Je, sheria inatumika kwa usawa kwa kauli za wanasiasa wa pande zote? Bibi yangu aliwahi kunikanya kuwa :Ukitania uwe tayari kutaniwa".
3. Lissu alitoa matamko yake hadharani au katika mikutano ya kisiasa. Wananchi wengi waliyasikia na wanayajua. Kwa hiyo, pamoja na kuacha Mahakama ifanye kazi yake kwa uhuru, ni vigumu kuzuia mjadala wa wananchi kuhusu jambo ambalo liko hadharani na linagusa siasa, sheria na haki za kiraia.
Ili mradi staha izingatiwe na mjadala huo usibadilishwe kuwa hukumu ya hatia au kutokuwa na hatia kabla ya Mahakama kumaliza kazi yake.
4. Kama Mahakama ingelikuwa imeamua kuwa hakuna kesi ya kujibu, hatua ya utetezi isingefunguliwa. Sasa Lissu ameomba kuwaita baadhi ya viongozi wakuu, akiwemo Rais Samia na viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama, kutoa ushahidi.
Historia ya nchi nyingine inaonyesha kuwa jambo la Rais aliye madarakani kutoa ushahidi katika shauri la jinai lina utata lakini si geni kabisa.
Mwaka 1807, katika kesi ya uhaini ya aliyekuwa Makamu wa Rais wa Marekani Aaron Burr, Burr aliomba ushahidi kutoka kwa Rais Thomas Jefferson, bosi wake. Jaji Mkuu John Marshall ndiye alikuwa muamuzi na alikataa "dhana kwamba Rais ana kinga ya moja kwa moja dhidi ya mchakato wa Mahakama pale ushahidi wake unapohitajika katika kesi ya jinai".
Jefferson hakulazimishwa kusimama mwenyewe kizimbani, lakini alitoa ushahidi kwa nyaraka na kanuni muhimu ikawa: hadhi ya Urais haimaanishi kwamba ushahidi muhimu kwa mtuhumiwa hauwezi kupatikana.
Baadaye, Marais wengine wa Marekani wamelazimika kutoa ushahidi au taarifa katika mashauri ya jinai inapohitajika. Ni pamoja na:
James Monroe — 1818
Ulysses S. Grant — 1876
Gerald Ford — 1975
Jimmy Carter — 1978
Jimmy Carter tena — 1980
Bill Clinton — 1996
Richard Nixon mwaka 1974 aliamriwa kutoa kanda za Watergate.
Mara nyingi ushahidi huo ulitolewa kwa maandishi, nyaraka, viapo/deposition au video badala ya Rais kufika mwenyewe mahakamani.
5. Hakika Hatua inayofuata katika kesi ya Lissu ni nyeti. Itatuonyesha mwanga katika masuala haya muhimu kuhusu utawala wa sheria na haki ya mshitakiwa kupata utetezi stahiki.
6. Kiuhalisia Wengine tumejikita kwenye swala la HEKIMA, BUSARA na HURUMA YA MUNGU.
‼️MSIKILIZENI MZEE WETU‼️
Wazee kuwashwa washwa kunasaidia ila hawa watawala makaidi waliwapuuza huko nyuma ndo maana leo Taifa lipo kwenye mkwamo!
Asante Mzee wetu Warioba kwa kusema UKWELI bila kupindapinda!
Leo wasipokusikiliza kuhusu maridhiano wakaleta ujinga wao tena watazidi kudidimiza Taifa ili lipotee
Full interview yake na @raiyajenerali iko:
https://t.co/dtHIbEq6DG
Kusema la Ukweli kabisa naomba ni Appreciate watu ambao hawana kazi, but still they Show up when needed, sio rude, hawana malalamiko na sio watu wakujieleza
Wamekubali situation na wapambana nayo in silent with big Faith kua wataondokana nayo
Mungu awafungulie njia wakuu🙌🏽
Siku tutakayokufa, hatutaitwa tena kwa majina yetu. Watasema, “Leteni mwili” au “Shusheni mwili kaburini.” Jina hubaki nyuma. Hivyo, tuishi kutafuta ridhaa ya Muumba, si sifa na makofi ya viumbe.
Kwa kuwa UTEKAJI, UTESAJI, UPOTEZAJI na MAUAJI ya watu wasio na HATIA, yamekuwa ni TATIZO LISILO NA MAJIBU, kwa nini Serikali HAIMUOMBI MSAADA WA KIJESHI Shehe SAID MWAIPOPO 👇 ili AKOMESHE mambo hayo HARAMU?
Zamani ukiwa peke yako njiani giza kali halafu ukamuona binadamu mwenzako anakuja, Unashukuru.
Ila siku hizi upo njiani giza kali halafu ukamuona binadamu mwenzako anakuja kwambali na wewe huku unaanza kujiandaa kwa lolote litakalo tokea.
Mambo yanabadilika kwa kasi sana.