Mgombea Uenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, amempongeza Tundu Lissu na wenzake, akiwemo John Heche, kwa ushindi walioupata katika uchaguzi uliofanyika kuanzia jana hadi usiku wa kuamkia leo. Ingawa matokeo rasmi hayajatangazwa, hatua hii inaashiria kuwa Lissu ndiye mshindi.
Rais mteule wa Marekani Donald Trump atarejea tena katika Ikulu ya White House baada ya kuapishwa rasmi kuwa rais wa 47 wa taifa hilo leo Jumatatu tarehe 20 Januari.
Rais mpya anatarajiwa kutoa wito wa umoja wa kitaifa katika hotuba yake ya uapisho.
Nchi ya marekani rasmi imetangaza kufungia mtandao wa Tiktok katika nchi hiyo, Rais mteule Donald Trump amesema "uwezekano mkubwa zaidi" angeipa TikTok ahueni ya siku 90 kutokana na marufuku hiyo baada ya kuchukua madaraka siku ya Jumatatu.
Kocha wa Fenerbahçe, Jose Mourinho, amesema kwamba kwa mtazamo wake, Arsenal FC haijapata sifa ya kuwa timu kubwa. Ingawa mara nyingi tunasikia kuhusu nguvu zao, Timu kubwa ni ile inayothibitisha uwezo wake kwa mafanikio ya kudumu uwanjani.
Ni kweli Arsenal ni sio timu kubwa?
Ajali ya lori katika kijiji cha Changombe, kata ya Segera, wilayani Handeni, mkoa wa Tanga, imesababisha vifo vya watu 11 na majeruhi 11 baada ya lori lililokuwa limebeba saruji kufeli breki na kugonga watu waliokuwa wakishuhudia ajali ya gari dogo aina ya Tata.
Timu ya @simbasctanzania leo imerejea nchini Tanzania kutoka Angola bada ya mchezo wao dhidi ya Bravos Fc, Mchezaji wa Simba SC Captain
@official_mohamedhussein15 Amesema malengo yao kwa sasa ni kuchukuwa ubingwa wa kombe la shirikisho baada ya kuvuka hatua ya makundi