Wafuasi wa MBOGAMBOGA wenyewe wamechanganyikiwa kama raia wengine tu. Hata wao hwaelewi mambo yanayotokea. Wanashangaa mtandaoni tu. Mambo ni mzobe mzobe. Ipo hivi, hamuwezi kuua watu wengi kwa kiwango kile halafu mkatawala watu kwa amani na utulivu. Damu za watu zitawatesa sana.
#UPDATES_KESI_YA_MAWAKILI_WA_MHE_LISSU_DHIDI_YA_MKUU_WA_MAGEREZA
Part 3
Anaendelea Mhe. Lissu
Mhe.Lissu: Nenda kwenye supplementary affidavit ya wajibu maombi wa 3 ya Tarehe 12/05 anasema kuwa wewe na Paul Kisabo hampo kwemye orodha ya mawakili niliyowasilisha kwake?
Wakili Maduhu: Ni sahihi.
Mhe. Lissu: Amewasilisha SUPP 1 kwenye supplimentary affidavit na anasema hakuna jina la Kulwa maduhu na Paul Kisabo. Sasa angalia hiyo annexure SUPP 1 na uwaeleze majaji kama maneno yake haya ni ya kweli?
Wakili Maduhu: Kwenye SUPP 1 hayapo.
Mhe. Lissu: Je pamoja na wewe na Paul Kisabo kutokuwepo kwenye orodha hii mmewahi kuja kuniona gerezani na kuongea na mimi?
Wakili Maduhu: Ni sahihi tumewahi kuja na kama mara tatu nimewahi kuingia na kuja kukuona.
Mhe.Lissu: Katika hizo mara tatu zote je ulijiandikisha pale magereza kabla ya kuniona na ukaonesha kitambulisho chako?
Wakili Maduhu: Sahihi nilifanya hivyo.
Mhe. Lissu: Je wewe ni mtunzaji wa hizo kumbukumbu za watu wanaoingia na kutoka Gereza la Ukonga?
Wakili Maduhu: Sio mimi kabisa. Ni Bwana Jela huyo hapo amekaa kwenye kiti ndio kazi yake. Anamuonesha kwa kidole chake.
Mhe. Lissu: Sasa waeleze majaji kama jina lako lipo kwa watu waliotembelea gereza?
Wakili Maduhu: Ndio tar. 28/10 jina langu lipo lakini hii siku sikumuona niliambiwa sitaweza kumuona. Na mara tatu zote nilizowahi kumuona hizo nyaraka hazijaletwa na Bwana Jela. Mkuu wa Gereza yani.
Mhe. Lissu: Nenda SUPP 2 angalia hiyo nyaraka halafu useme item no. 10 aliyekuja ambae ni Paul Kisabo ameoneshwa jina lake na shida yake wameandika shida za kisheria.
Wakili Maduhu: Namuona hapa ndio yupo.
Mhe. Lissu: Tarehe 30/09 angalia jina la kwanza hapo la watu waliotembelea Gerezani ni akina nani?
Wakili Maduhu: Jina ni la Paul Kisabo.
Mhe. Lissu: Je yupo kwenye ile orodha ya kwanza ya watu niliowatambulisha kwa mujibu wa Bwana Jela?
Wakili Maduhu: Kule hayupo.
Mhe. Lissu: Kumbe hayupo kule na magereza walimruhusu aingie?
Wakili Maduhu: Ndio kabisa
Mhe. Lissu: Nenda sasa SUPP 3 na yenyewe. Majina ya mawakili unaowaona na wataje.
Wakili Maduhu: Andrew Mathew Chima na Nashon Nkungu.
Mhe. Lissu: Hao mawakili walikuja kuniona mimi?
Wakili Maduhu: Ndio
Mhe.Lissu: Huyo Andrew aliyekuja kuniona ni mmoja wao au sio mmoja wao kwenye ile orodha aliyosema Bwana Jela?
Wakili Maduhu: Hayumo kabisa.
Mhe. Lissu: Nenda SUPP 5 sasa kwenye hicho kielelezo ni register book ya Gereza la Ukonga. Pembeni imeandikwa SUPP 5 ukurasa unaofuata unaonesha entry ya Tar. 07/05 mwaka jana kuna mtu wa kwanza kabisa anaitwa Nashon Nkungu kazi yake ni wakili amekuja kumuona Mahabusu Tundu Lissu. Shida za kisheria.
Wakili Maduhu: Ni kweli kabisa.
Mhe. Lissu: Sasa waeleze majaji kwanini aliruhusiwa kuja kuniona huyo Nashon.
Wakili Maduhu: kwasababu ni wakili wako.
Mhe. Lissu: Tarehe inayofuata aliruhusiwa tena kuingia?
Wakili Maduhu: Ndio anaonekana hapa kwenye ukurasa unaofuata. Kwenye kurasa kadhaaa. Ukurasa wa 9 na tarehe 28/07 alikuwa mtu wa kwanza kuja kukuona.
MheLissu: Tar. 24/12 jina namba 2 ni Nashon Nkungu tena?
Wakili Maduhu: kweli kabisa.
Mhe. Lissu: Kisabo je yupo au hayupo?
Wakili Maduhu: Na Kisabo nae yupo kabisa.
Mhe. Lissu: 04/03/2026 mtu wa pili Nashon Nkungu aliruhusiwa kuja kuniona?
Maduhu: Sahihi kabisa.
Part 4 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_MAWAKILI_WA_MHE_LISSU_DHIDI_YA_MKUU_WA_MAGEREZA
Part 2.
Anaendelea Mhe. Lissu
Mhe. Lissu: Nenda ukurasa wa 27 angalia defence counsels angalia jina la Kulwa Maduhu na Paul Kisabo kama hayapo?
Wakili Maduhu: Yapo majina ya hao mawakili.
Mhe. Lissu: Ukurasa wa 40 kwenye huo mwenendo wa Kisutu angalia upande wa corum useme kama Paul Kisabo na Kulwa Maduhu.
Wakili Maduhu: Wapo wote wawili.
Mhe. Lissu: Sasa waeleze majaji kama kuna utaratibu wowote wa kisheria wa unaopaswa kuufuata kumuona mteja?
Wakili Maduhu: Hakuna utaratibu wowote wa kisheria zaidi ya kuonesha kitambulisho tu cha uwakili.
Mhe. Lissu: Haya Maneno ya Bwana jela kuwa sijakutambulisha ni maneno ya bure tu?
Wakili Maduhu: Kabisa maneno ya bure kabisa.
Mhe. Lissu: Unazifahamu kanuni za maadili za mawakili?
Wakili Maduhu: Nazijua ndio.
Mhe. Lissu: Je kwa kanuni hizi wakili anaruhusiwa kumuonesha makubaliano yake na mteja mtu anayeitwa Bwana Jela?
Wakili Maduhu: Duty to confidentiality hairuhusu. Kwahiyo siruhusiwi kabisa kutoa siri za mteja wangu.
Mhe. Lissu: Sasa unasemaje kuhusu hizi habari za Bwana Jela kuwa sijakutambulisha kwake?
Wakili Maduhu: Hizo ni kauli za bure kabisa. Mimi silazimiki kufanya hivyo. Nina miaka 6 ya uwakili kwa sasa huo utaratibu haupo kabisa.
Mhe. Lissu: Nenda Ukurasa wa 41 hadi 43 wa proceedings za Kisutu. Soma Tar. 16/06 sema kama mahakama ya Kisutu haikuandika malalamiko yangu kuhusu mawakili wangu kunyimwa kuniona.
Wakili Maduhu: Ni kweli malalamiko yapo.
Mhe. Lissu: Ni kwamba nilikuwa nazuiwa kuonana na mawakili wangu?
Wakili Maduhu: Kweli yapo hapa
Mhe.Lissu: Kwamba ni kinyume na kanuni za uendeshaji wa magereza?
Wakili Maduhu: Ni sahihi kabisa yapo yote kwenye hizi kurasa za mambo ya Kisutu.
Mhe. Lissu: Pia kuna malalamiko specific kuwa kitendo hicho cha mimi kuninyima nisionane na mawakili wangu ni kinyume na sheria na kanuni za kimataifa?
Wakili Maduhu: Ni sahihi kabisa.
Mhe. Lissu: Nikalalamika kuwa naishi na wafungwa waliohukumiwa kifo? Na natendewa sawa na watu hao?
Wakili Maduhu: Kweli kabisa ulisema.
Mhe. Lissu: Baada ya hayo nilisema nitajiwakilisha mwenyewe kwasababu sitaki mawakili wangu waje kulaumiwa bure?
Wakili Maduhu: Ni kweli ulisema hivyo na ikawa hivyo.
Mhe. Lissu: Ulipoamua kujiwakilisha mwenyewe nilisema waendelee kunisahuri na kunipa nyaraka wakati kesi inaendelea. Nilisema hivyo?
Wakili Maduhu: Ni kweli kabisa.
Mhe. Lissu: Sasa waeleze toka siku hiyo tar. 16/05/2026 hadi leo mmeendelea kunipa ushauri wa kisheria na kunipa nyaraka Gerezani?
Wakili Maduhu: Ni kweli tumeendelea kufanya kazi hiyo.
Mhe. Lissu: Je una kumbukumbu za kilichotokea Mahakama Kuu kuhusu shauri hilo lilipofika Mahakama kuu niliwaeleza waheshimiwa majaji kuwa nina mawakili wanaonisaidia kwa research na ushauri.
Wakili Maduhu: Ni sahihi ulisema.
Mhe. Lissu: Naomba nimuonyeshe proceedings za Mahakama Kuu. Tuambie from page 4 to 6 wambie majaji kama huo mwenendo unaonesha niliwaambia Majaji wa Mahakama kuu nina mawakili ambao wananisaidia na nikaomba waingizwe kwenye corum.
Wakili Maduhu: Nimeona ndio.
Mhe. Lissu: Na Katuga alipinga ombi langu hilo.
Wakili Maduhu: Ni sahihi naona hapa.
Mhe. Lissu: Mahakama ikasema hatutawaingiza kwenye corum lakini mawakili wako waendelee kukusaidia?
Wakili Maduhu: Naona iko hapa.
Mhe. Lissu: Kwahiyo ni kweli sio tu Kisutu hata Mahakama kuu hii inakutambua wewe na wenzako kama mawakili wangu?
Wakili Maduhu: Ni kweli kabisa.
Part 3 itaendelea kwenye post inayofuata
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_MAWAKILI_WA_MHE_LISSU_DHIDI_YA_MKUU_WA_MAGEREZA
Part 1
Maombi haya yanasikilizwa na jopo la majaji watatu ambao ni Mh. A. Mruma, Dr. A. Rumisha na Dr. E. Longopa.
Kiongozi wa Jopo hili ni Mheshimiwa A. Mruma.
Nawaona waleta maombi wote wapo. Lakini pia Mawakili wao wapo ambapo jopo la mawakili wao linaongozwa na Wakili John Seka, akisaidiwa na Edson Kilatu na Selemani Matauka.
Lakini pia Chama cha Mawakili Tanganyika kinawakilishwa na Wakili Emmanuel Ukashu.
Namuona Mkuu wa Gereza la Ukonga tayari ameshaingia hapa Mahakamani amekaa nyuma ya mawakili pale. Ni Dingi mmoja mrefu, mweusi amevaa Kaunda Suti na kitambi kile cha maaskari wa magereza.
Maandalizi ya majaji kuingia yamechukua muda mrefu sana.
Wanaingia sasa imepigwa High Courtttttttttt.
Mhe. Lissu hajaingia bado.
Majaji ni kama wanashangaa, mbona Lissu hayupo maana hawamuoni kizimbani.
Anatoka karani kwenda kuwatafuta magereza kwasababu hawapo kabisa hapa Mahakamani.
Wameanza kuingia maaskari magereza wa kutosha. Wanajipanga, muda sio mrefu ataingia Mwenyekiti. Tunamsubiri.
Ameshaingia akiwa na na Kombati yake ya Kaki na mifuko yake iliyobeba nyaraka zake, anazitoa taratibu pale anaweka mezani na majaji wanateta.
Anasimama Wakili wa Serikali baada ya jalada kusomwa hapa.
Naitwa Stanley Kalokola, Wakili wa Serikali nitasaidiwa na Francis Wisdom. Mjibu maombi wa nne yupo mbele ya Mahakama yenu na interested party TLS wapo.
Tuko tayari kuendelea na zoezi la DODOSO kwa siku ya leo.
Wamehojiwa waleta maombi na pande zingine wote wako tayari.
Mhe. Jaji Mruma anasema sasa 4th Respondent usikae kwenye kizimba ukae huku kawaida maana hii ni kesi ya Kikatiba.
Mhe. Lissu amesema naomba nikae hapa hapa maana nina meza na nitakaa vizuri nikiwa hapa.
Jaji Mruma akasema hakuna shida kaaa hapo hapo.
Basi ameitwa mleta maombi wakwanza Maduhu William aanze kuulizwa maswali ya Dodoso na Mhe. Lissu.
Jaji anasema ni vema ukaapa kwanza. Wewe ni afisa wa Mahakama unajua kuapa haya apa sasa.
Wakili Maduhu: Nina miaka 36 ya kuzaliwa. Mkristu, na anaaapa hapa tena.
Jaji: Bwana Tundu Lissu karibu.
Mhe. Lissu: shaidi naomba nikuulize maswali kuhusu kiapo ulicholeta mahakamani na kesi uliyoileta Mahakamani dhidi ya sisi walalamikiwa wanne.
Waeleze majaji kama hapo ulipo una nakala ya hati ya madai na kiapo chako.
Wakili Maduhu: Vyote ninavyo hapa.
Mhe. Lissu: Je una nakala ya hati ya viapo kinzani yaani counter affidavit za walalamikiwa wakwanza hadi wanne pamoja na interested party.
Wakili Maduhu: Ninazo hizo nyaraka zote.
Mhe. Lissu: Tuanze na hati yenu ya madai na kiapo chako katika aya ya kwanza ya originating summons na aya ya pili ya kiapo chako.
Angalia Je kwenye hizo aya umesema wewe ni mmojawapo wa mawakili wangu katika kesi ya jinai iliyopo katika mahakama hii. Umesema wewe na wenzako ni mawakili pia wa kesi yangu iliyopo kisutu.
Wakili Maduhu: Ni kweli
Mhe. Lissu: Naomba uangalie aya ya nne ya hati ya kiapo kinzani ya wajibu maombi wa kwanza hadi watatu na hicho kiapo kilitolewa na Andrew Shaban kilitolewa Tarehe 09/04.
Huyu Andrew anasema wewe hujawahi kutambulishwa kwake kuwa ni mmoja wa Mawakili wangu.
Wakili Maduhu: Ni kweli huyu Andrew amesema mimi sio Wakili wako.
Mhe. Lissu: Ni kweli au si kweli hii kesi iliyopo Mahakama Kuu ilianzia Mahakama ya kisutu ambako ilikuwa ni (P.I)
Wakili Maduhu: Ni kweli.
Mhe.Lissu: Na hiyo kesi ilikuwa mbele ya Kiswaga pale Kisutu?
Wakili Maduhu: sahihi.
Mhe. Lissu: Angalia majibu yangu kwenye hili shauri lenu, kwenye majibu yangu kuna viambatanisho kadhaa. Angalia annexure A2N24R umekiona?
Wakili Maduhu: Nimekiona.
Mhe. Lissu: Nenda Ukurasa wa 19 wa hizo proceedings angalia waliokuwepo Mahakamani tar. 06/05 angalia corum kuhusu mtuhumiwa. Je jina la Maduhu lipo?
Wakili Maduhu: Ni kweli lipo.
Part 2 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba nisaidie kushare ujumbe uende mbali.
Kwenu Gen Z,
Oyaa! Mzigo umepanda. Target imehama, sasa tunaelekea Bilioni 5.
Msiache hii iwe kazi ya watu wachache. Kizazi chenu kimeonyesha mara nyingi kuwa kikiamua, hakuna kisichowezekana.
Mmebadilisha mijadala, mmeamsha matumaini, mmefanya sauti ya mabadiliko isikike kila kona ya nchi. Sasa ni wakati wa kuipa sauti hiyo nguvu ya mchango.
Tusibaki kwenye likes, reposts na hashtags pekee. Tuweke pia alama zetu kwenye Tone Tone.
Usichangie kwa sababu umeombwa. Changia kwa sababu unaamini. Hata elfu mbili yako ni sehemu ya Bilioni 5 tunayoiandika pamoja. Hakuna mchango mdogo unapokuwa wa watu wengi wenye imani moja.
Tonesheni Tone Tone. Tufanye historia pamoja, ili kesho tukisimulia ushindi huu, kila mmoja aweze kusema, “Nilikuwepo.”
CHADEMA MPESA- 0744446969
Wenu katika Struggle,
G. J. L
GAMONDI Hajasoma script bila shaka. Ametoa pole kwa watanzania kwa yaliyotokea oktoba 29.
Dunia imesikia na imeona yote yaliyofanyika GIZANI. Kwa Hili WAPENDA HAKI tunaungana na GAMOND.
REPOST 200
TUTAKUWEPO🫵😎
Our Commander of hand to mouth battalion have been detained without being taken to the court or being given his right to bail. we request him being released or we will file Habeas Corpus for our fellow hoof heater.
#freebuyobe@fbuyobe
Katika nyakati hizi, ni muhimu kwa vyombo husika kutoa ufafanuzi wazi kuhusu hali ya Fortunatus Buyobe.
Itakuwa vyema kwao kusema neno lolote kuhusu sababu za kumshikilia, ili wananchi waweze kuelewa ni kwa makosa gani anashikiliwa.
Hii itasaidia kuepusha nadharia zisizo za kweli na kutoa nafasi kwa jamii kujua ni mchakato gani wa kisheria unaoendelea.
Kwa kuwa sheria inataka kuwa na uwazi katika taratibu za kisheria, ni haki ya raia kujua kwa nini Fortunatus Buyobe anashikiliwa.
Hakuna mtu anapaswa kukosa uwazi kuhusu mashitaka anayokabiliwa nayo, kwani hili ni jambo muhimu kwa utawala wa sheria.
Iwapo vyombo vya usalama na serikali wataendelea kudumisha kimya kuhusu hali ya Buyobe, itajengeka hali ya shaka na kuaminiwa kwa mchakato wa kisheria unaoendelea.
Kwa hivyo, ni vyema kwamba vyombo husika vikatoa taarifa rasmi kuhusu makosa anayotuhumiwa nayo Fortunatus Buyobe ili umma uwe na uelewa sahihi wa jambo hili.
Hii ni sehemu ya kujenga imani kwa mchakato wa haki na mambo ya kisheria katika jamii yetu.
Mnaua maelfu ya watu ili mjibakize madarakani… na hayo madaraka hamjui hata cha kuyafanyia..
How on earth, Nchi ya tatu kwa vyanzo vingi na bora vya maki baridi ya Binadamu kutumia, jiji kubwa kuliko yote hakuna maji… miaka 64 ya kinachoitwa Uhuru!!!
Nyie mngekua jangwani ingekuaje?
Kama kuna mtu anawaunga mkono, Basi kuna shida kubwa kwenye IQ yake.
Leo tarehe 12/12/2025 , Mwenyekiti wetu ametimiza mwezi mzima tangu mara ya mwisho alipoletwa Mahakamani.
Mlimkamata kwamba mna kesi, mna mashahidi na mmejiandaa kumaliza hii kesi. Watanzania wajue na Dunia ijue huo uhaini unaofanywa na mwanasiasa anaekupinga kidemokrasia.
Leo anakaa ndani bila sababu na hakuna kinachoendelea, vyombo vyetu vya dola, mahakama zetu zinatumika kuumiza watu kwa malengo ya kisiasa..
Unamwambia nani kufuata sheria wakati wewe haufuati sheria.
Utawashawishi vipi wananchi kuamini na kuheshimu mahakama za aina hii, nani anaweza kuja kuwekeza kwenye sehemu ambayo mahakama zake zinafanya mambo kama haya?
Mleteni Mwenyekiti mahakamani au futeni huu uhuni wa kutumia mahakama kuumiza watu ambao mmeshindwa kujibu hoja zao..
Mwenyekiti wetu hatakubali ushawishi wenu wa aina yoyote, hawezi kutoka nje ya Nchi kama mnavyotaka hapa ni kwao na hawezi kutoka kwa masharti yenu.
#FreeTunduLissu