The Government Chemist Laboratory Authority is the “Legal Referral Laboratory”. Established under the Government Chemist Laboratory Authority Act,No.8,2016.
Tembelea banda la @Gcla1895 katika maonesho ya Sabasaba upate elimu kuhusu huduma za maabara, usalama wa bidhaa, uchunguzi wa sampuli, na mchango wa Mamlaka katika kulinda afya, mazingira na maslahi ya wananchi.
Karibu Sabasaba, jifunze, uliza, na upate huduma bora.
@Gcla1895 imetoa mafunzo ya uchukuaji, utunzaji na uhifadhi wa sampuli za matukio ya moto kwa maafisa na askari 62 wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kutoka mikoa mbalimbali nchini. Mafunzo hayo yalilenga kuimarisha uwezo wa washiriki katika ukusanyaji na usimamizi sahihi wa sampuli
Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali Inashiriki maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (Sabasaba) 2026.Karibu utembelee katika Banda letu na upate kufahamu huduma mbalimbali zinazotolewa ikiwemo Huduma za Uchunguzi wa kisayansi wa kimaabara
Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali wamekagua maendeleo ya Ujenzi wa Jengo jipya la Ofisi ya Kanda ya Mashariki, ukaguzi uliofanyika Dar es Salaam Juni 25, 2026.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, Prof.Riziki Shemdoe amesema Serikali imepata mrejesho wa moja kwa moja kutoka kwa wananchi na Serikali itatumia mrejesho huo kuboresha huduma.
ameyasema hayo Juni 23, 2026 Wakati akifunga maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, Dodoma.
@Gcla1895 Ofisi ya Kanda ya Nyanda za Juu Kusini imetoa Mafunzo ya Usimamizi Salama wa Kemikali kwa Wasimamizi wa Kemikali kutoka mikoa mbalimbali ikiwemo Songwe, Geita,Tanga.Mafunzo yamefanyika kwa siku mbili Julai 18 na 19, 2026 jijini Mbeya. Zaidi ya wadau 100 wameshiriki.
Kamishna Jenerali wa @dceatanzania Aretas Lyimo na Mkemia Mkuu wa Serikali,Dkt.Fidelice Mafumiko wameshiriki kuzindua Chama cha Wadau wanaojihusisha na Kemikali Bashirifu (Tanzania Chemical Stakeholders Association TCSA), uzinduzi ambao ulifanyika Dar es Salaam Juni 18,2026.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwani kikwete, amefungua maadhimisho ya wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika katika viwanja vya Chinangali Dodoma , Juni 16-23, 2026.
@Gcla1895 ni miongoni mwa Taasisi za Umma zinazoshiriki
Ofisi ya Kanda ya Mashariki imeendesha kampeni ya uhamasishaji wa usafirishaji salama wa kemikali uliofanyika kuanzia Dar es salaam hadi Tunduma mkoani Songwe.
Kampeni imefanyika maeneo yanayohusisha ukaguzi wa kiforodha, mizani, maegesho ya magari na vituo vya ukaguzi wa Polisi
Ofisi ya Kanda ya Mashariki, imetoa mafunzo ya Usimamizi na usafirishaji salama wa Kemikali kwa madereva wanaosafirisha Kemikali. mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Kanda ya Mashariki, jijini Dar es Salaam, Juni 12, 2026
@Gcla1895 imetoa Mafunzo kwa Jeshi la Polisi wa Upelelezi, Waendesha Mashtaka,TAKUKURU na Uhamiaji katika Wilaya ya Tarime ya namna Bora ya Utunzaji, uchukuaji na usafirishaji wa Sampuli za Jinai kwa ajili ya uchunguzi wa kimaabara yaliyofanyika Juni 12,2026,Tarime, Mkoa wa Mara
Ofisi ya Kanda ya Mashariki, imetoa mafunzo kwa madereva wanaosafirisha Kemikali, mafunzo hayo yamefanyika mkoa wa Pwani, Kibaha katika Ukumbi wa kampuni ya Delina Oil and Gas Distributors, Juni 10, 2026.
Mkuu wa Wilaya ya Nzega,Mhe. Naitapwaki Tukai amewataka wachimbaji wa dhahabu kuzingatia usimamizi na matumizi salama ya Kemikali ili kuepukana na madhara ya kemikali hizo yanayoathiri Afya za watu na mazingira
Mh.Tukai amesema hayo wakati akifungua mafunzo wilayani Nzega, Tabora
Mkemia Mkuu wa Serikali,Dkt. Fidelice Mafumiko,amefanya kikao cha Majadiliano kati ya @Gcla1895 na chama cha walimu Tanzania, Idara ya Afya na usalama kazini juu ya namna ya kuendesha mafunzo kwa walimu wa masomo ya sayansi dhidi ya utunzaji na uteketezaji wa kemikali mashuleni.
@Gcla1895 imehitimisha siku mbili za Mkutano wa Wakaguzi wa Kemikali na Maabara za Kemia uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Arusha Corridor Springs Hotel jijini Arusha Juni 6, 2026
@Gcla1895 imeibuka mshindi wa kwanza wa Tuzo ya utoaji huduma ubora wa kitaifa kwa taasisi za umma iliyotolewa na Wizara ya Viwanda na Biashara Kupitia Shirika la Viwango Tanzania “TBS”
Tuzo hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Mhe. Dennis Londo.
@Gcla1895 Ofisi ya Kanda ya Mashariki, imetoa mafunzo ya Usimamizi na Uhifadhi salama wa Kemikali kwa Wanafunzi wa fani ya Sayansi Kemia, Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, Mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa Jengo la Ushirika jijini Dar es Salaam, Juni 2,2026.
Watumishi wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali wametembelea Shule ya Sekondari Bihawana Mkoani Dodoma na kutoa elimu juu ya Majukumu ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu w Serikali kwa umma. Zoezi hilo limefanyika shuleni hapo, Mei 29, 2026