Ujinga ni tatizo linalotatuliwa na kujua sio kuombewa, mambo mengi tunayoyaombea ni kwasababu hatujui namna ya kuyapata, ambayo Mungu ameiachilia katika neno lake.
Ulinzi wa taifa si kulinda mipaka pekee.
Ni pia kulinda misingi inayolifanya taifa libaki taifa.
Taifa hulindwa si kwa bunduki tu, bali pia kwa:
Taasisi imara,sheria zinazoheshimiwa, mahakama huru, bunge lenye uwezo wa kuisimamia serikali, uchaguzi unaoaminika, na wananchi wanaoamini kuwa haki inaweza kupatikana bila nguvu wala hofu.
Kwa sababu mipaka inaweza kubaki salama…
lakini taifa ndani likaanza kuoza.
Mahakama zikikosa uhuru,
bunge likigeuka muhuri wa kupitisha kila kitu,
taasisi za umma zikianza kuogopa watu kuliko sheria,
ndipo taifa huanza kupata ufa wa ndani ambao ni hatari kuliko adui wa nje.
Historia inaonyesha:
mataifa mengi hayakuanguka kwanza kwa kuvamiwa
yalianguka pale ambapo taasisi zilianza kudhoofika, ukweli ukaogopwa, na mamlaka ikawa kubwa kuliko sheria.
Ulinzi wa taifa wa kweli ni kuhakikisha:
Hakuna mtu aliye juu ya sheria,taasisi zinafanya kazi bila hofu,na madaraka yanabaki kuwa dhamana ya wananchi, si mali binafsi ya watawala.
Kwa sababu mwisho wa siku:
jeshi linaweza kulinda mipaka,
lakini ni taasisi huru zinazolinda roho ya taifa.”
“Msimamo wa mwanadamu haupaswi kuwa gereza la dhamira yake.
Kuna nyakati ambapo ukimya huwa mzigo kuliko maneno.
Sidai kuwa mimi ni mkamilifu, lakini nimeamua kutii dhamira yangu kuliko kuigiza consistency isiyo na ukweli. Si busara kushinikizwa kuonyesha “uanaume wa kisiasa” kwa kubaki sehemu ambayo dhamira yako haiwezi tena kutulia”
Nimefikiri na kutafakari kwa muda mrefu baada ya matukio ya ukiukwaji wa haki, utu na dhuluma dhidi ya uhai wa binadamu yaliyotokea tarehe 29 Oktoba 2025. Siwezi kuendelea kuishi katika huzuni na ukimya tena.
Kwa dhamira yangu binafsi, leo nimejiondoa rasmi kutoka CCM na kurejea CHADEMA kwa kufuata taratibu zote za CHADEMA.
Kwa Watanzania wote, na wanachama wa CHADEMA wale walioumizwa au kukatishwa tamaa na msimamo wangu wa awali, naomba radhi kwa dhati pale nilipokuwa kinyume na matarajio yetu ya pamoja katika safari ya kutafuta haki, utu na demokrasia ya kweli.
Naam, binadamu hukosea, lakini dhamira inapozinduka ni wajibu kusimama upande unaouona kuwa wa kweli na wa haki.
Asanteni Sana.
Hii hapa nyingine kubwa kutoka Msimbazi kuja kwako Mwanasimba kindakindaki.
Sasa unaweza kuwapa burudani wakupigiao kwa kufanya goli la Chama dhidi ya mtani kuwa muito wa simu yako. Nani kwenye simu yako unatamani awe wa kwanza kukutana na goli lile la mwaka wa mbele? 😄 #NguvuMoja
“Kumekuwa na majaribio na vitisho kutoka kwa watawala kunizuia nisiongee. Kuna wakati niliambiwa nizime simu yangu, nisiitumie mpaka (wao) watakapo niambia. Nikawauliza, kwa sheria gani? Kuna wakati nilikaribishwa mahali fulani, nikapigiwa simu na watawala, wakasemam mzee usiendee kwenye huo mkutano. Kwanini? Hauna manufaa. Nikawauliza, nani anaamua hayo manufaa? Nikakataa. Wakawafuata watu walio karibu na mimi ili wanishawishi nisiende, nikakataa pia. Mnakumbuka nilifanya mahojiano hapa na Jamhuri? Wakatoa summary, wakasema watachapisha mahojiano yote, neno kwa neno. Baadae Jamhuri wakanieleza wamezuiwa wasitoe yale mahojiano. Kuna viongozi wanaogopa kuzungumza na mimi, wanatuma ujumbe kupitia mbali huko. Marafiki zangu wanaogopa wakisema nitatekwa au kupewa sumu. Nawaeleza mimi ni mali ya Mungu, ndiye atakayeamua lini ananihitaji.”
— Jaji Mstaafu Joseph Sinde Warioba, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais Tanzania.