Na, John Marwa
Hivi karibuni kumeibuka mjadala mkubwa hapa Nchini lakini sasa mjadala huo unaendelea kuota mizizi kila uchwao kwani sasa umefika kwenye 'vijiwe', Vyombo vya Habari vya ndani na hata Nje ya Nchi ikiwemo shirika la Utangazaji la Kimataifa la Uingereza (BBC)
Mjadala huu unahusisha ukimya wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango, ukimya wake umekuwa ukiibua maswali na mijadala lukuki kutoka kwa Watanzania na hata wasiokuwa Watanzania wengi wao wakihoji aliko kiongozi huyo ambaye kiuhalisia ni msaidizi namba moja wa Rais Samia Suluhu Hassan katika shughuli zake za kila siku
Yuko wapi?, Je anaumwa?, Yuko likizo?, Yuko ndani ya Nchi au nje ya Nchi? na kama ni nje ya Nchi ni Nchi gani?..., haya ni baadhi ya maswali mengi yanayochomoza kwenye mjadala huu ambao kimsingi kabisa maswali na sintofahamu inakuwa kubwa zaidi kutokana ukimya wa Serikali,
Kila mmoja wetu anaamini kuwa Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan, Chama chake (CCM) na pengine familia yake ndio wenye majibu ya maswali yote hayo, swali ni kwa nini wako kimya?
Kwenye jambo kubwa, muhimu na nyeti kama hili, tunaweza kuiweka kando familia yake na Chama chake lakini Serikali katu haikustahili kuwa kimya kiasi cha kufikia hatua inayoleta mashaka zaidi, kwa kuwa uwongo ukivuma sana hugeuka kuwa kweli, binafsi sitaki kukubaliana moja kwa moja na mijadala hasi inayochomoza kwenye mitandao ya kijamii, lakini kwa nini wenye mamlaka wanairuhusu mijadala hii iote mbawa?, kuna ugumu gani kwa Serikali kutoka hadharani kutoa taarifa rasmi kuhusu aliko Makamu wa Rais?
Ikumbukwe kuwa anayeuliziwa hapa si Dkt. Mpango bali ni Makamu wa Rais wa Tanzania na ndio maana hata hivi karibuni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliposema Makamu wa Rais yuko nje ya Nchi kikazi hivyo tupuuze yale yanayoendelea mitandaoni, badala ya kupunguza maswali maelezo yake yaliongeza maswali maradufu kwa kuwa kama yuko nje ya Nchi je, ni Nchi gani na amekwenda kufanya kazi gani?, bila shaka kazi aliyoenda kuifanya ni kwa niaba ya Watanzania kwa nini iwe siri?, kama safari na ziara za Rais za ndani na nje ya Nchi zinawekwa wazi iweje ziara za Makamu wake ziwe siri?, majibu ya haya yote inayo Serikali
Kwa mujibu wa taarifa ambazo Jambo TV na Watanzania wote tulizipata mara ya mwisho kutoka Ofisini kwake ilikuwa Oktoba 31.2023 ambapo Dkt. Mpango alimuwakilisha Rais Dkt. @SuluhuSamia kwenye mkutano wa dharula wa wakuu wa Nchi na Serikali wa Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) ambapo mkutano huo ulifanyika kwa njia ya mtandao na Makamu wa Rais alishiriki akiwa Dodoma,
Lakini kubwa kuliko yote linalokoleza jambo hili ni uwepo wa maafa yalioyotokea Katesh, Wilayani Hanang, Mkoani Manyara, wakati Watanzania sote tukiwa kwenye msiba huu mzito, na maafa haya ambayo yamelikumba Taifa bila shaka unahitaji kusikia sauti au kauli za viongozi wakuu wa Serikali, Rais Samia Suluhu aliyelazimika kukatiza ziara ya kikazi Dubai tumemshuhudia akirejea Nchini kwa haraka na kuibukia Hanang kuwafariji wahanga, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Mawaziri, Makatibu Wakuu na viongozi wengine waandamizi kutoka serikalini na nje ya Serikali ni kama wameweka kambi huko kuhakikisha mambo yote yanawekwa sawa, Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Mwinyi naye katuma salamu za pole na rambirambi, viongozi mbalimbali Duniani tumeona wakituma salamu zao za pole kwetu lakini cha kushangaza hadi sasa hakuna kauli yoyote ya Makamu wa Rais aliyoitoa sio kwa sauti au maandishi, hii ina maana gani?, nikubaliane na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuwa yuko nje kikazi je hafahamu kinachoendelea Nchini? na kama anafahamu ukimya wake una maanisha nini?
Serikali inapaswa kufahamu kuwa Watanzania wanataka kufahamu Makamu wa Rais yuko wapi?, hili sio suala la Dkt. Mpango ni suala la Makamu wa Rais, koti la uongozi kwa kiongozi yeyote yule Duniani aliyekaa kwenye nafasi hiyo Kikatiba ni mali ya Wananchi husika ndio maana asilimia kubwa ya wanayofanya yanapelekwa kwa Umma kupitia taarifa rasmi.
Hivi Serikali hii ilijifunza chochote juu ya kifo cha Magufuli mwaka juzi? Kifo au ugonjwa wa kiongozi mkuu wa nchi havifichiki! Kufichaficha kunaleta hisia mbaya za mchezo mchafu dhidi yake. Jisafisheni! Tuambieni aliko Makamu wa Rais Phillip Mpango sasa! https://t.co/mcbl3dgLvA
Mzee yoyote mwenye akili timamu na kijana yoyote anayejali Nchi,awe ni mfanyakazi au mjasiriamali,kazi na ndoto ya msingi anayopaswa kuwa nayo kwa sasa ni kusaidia CCM ianguke.Nchi ina compromise attitude na good character sana kwa CCM kuendelea kuwepo madarakani. Athari za CCM kuendelea kuwepo madarakani damage zake ni kubwa sana kuliko tunavyoweza kifikiri.
Bishop : Wanajeshi wanazuia watu kupiga picha, Kila anayepiga picha kwenye janga ili ananganywa simu, ili suala ni kama hawataki taarifa itoke , Hii inakwamisha watu kupata msaada
#MariaSpaces#KatibaMpya#WenyeNchiWananchi
YT https://t.co/3C6nQcOdyW
X https://t.co/dtFwR2hChB
@Jambotv_ Tulipofkia kwa sasa hata wasipooneka serikali nzima, Bunge, mahakama na wafanyakaz wote wa Uma wala hatutahoji lolote coz hata wakionekana hawana faida yeyote kwenye Taifa letu, hawana faida yeyote kwa wananchi zaid tunaona kero tu kuona watu ambao hawana lolote wanalotusaidia.
Acheni masihara!🤨
This is getting serious
WHERE IS DR MPANGO?
#WhereIsDrMpango 😳
Mlionitumia DM eti kaonekana hapa na pale alafu hamjaniletea picha bado hamjaweza kunishawishi!
Au ndo kama Ndugai kipindi kile?
Hebu mtoeni mzee tumwone yuko mzima buheri wa afya maisha yaendelee
🚨🚨 #Tanzania update ‼️
Seems the alleged perpertrator released this video of the confession by the victim
Unfortunately for her, the video also shows that the victim’s trousers are down and he is exposed - proving that he was humiliated and possibly sexually assaulted as he claims
Stupid is as stupid gets! The former deputy minister is not the brightest apple in the barrel if you ask me!
Again the accused needs to be detained for further questioning
Cc @hrw@AmnestyEARO@HRF
Hii akiimba msanii wa Tanzania utasikia wamemfundia mpaka kibubu yake
Au wakampa maji kwenye ndoo wakasema anauza gongo
Tuna nchi ya kitumwa sana no FREE THINK, ukitumia akili wanatutanguliza mbinguni https://t.co/YAnGgKp1wb