Jana nilipoona taarifa ya kufariki kwa Lucas Masawe niliumia sana.
Sijamfahamu Lucas kwa muda mrefu, na tulijuana humu humu X kwenye mijadala mbali mbali ambayo tulikuwa tunashiriki.
Siku pekee iliyonifanya nikamkubali zaidi ni ile siku ambayo alinitafuta DM "INSTAGRAM" kunishauri niongeze uchangamfu kwenye content zangu.
Hii ilikuwa January mwaka huu, yeye ni miongoni mwa watu wachache walioamini kwenye ninachofanya na akawa mtu wa kushauri ili niboreshe mbeleni nije kuwa mtu bora zaidi.
Mimi sio mtu wa kujibu na kusoma DM za watu wanaonitafuta, ila ya LUCAS nilifungua na tulichat kwenye maoni ambayo alitamani niyafanyie kazi.
Baada ya pale nilianza kubadilika na naamini nilivyokuwa nayafanya baadae pale instagram, facebook & tiktok huenda yeye mwenyewe ni shahidi kuwa NILIFANYIA KAZI ushauri wake kwa asilimia 200%.
Tunakuja duniani kuja kuacha IMPACT KWENYE MAISHA YA WATU WENGINE. Mimi kwenye maisha yangu Lucas kaacha hiyo impact itakayoishi miaka na miaka.
Pumzika kwa amani Lucas Masawe, kama kuna kesho nyingine kama tunavyoahidiwa kwenye Biblia basi naamini tutaonana tena sote njia ni moja wewe umetangulia tuu.
Familia yake pia Poleni, najua mnapitia kipindi kigumu kwa kijana kama Lucass kuondoka akiwa bado ana umri mdogo sana.
R.I.P BROTHER๐
UKIONA jambo wenzako hawakuungi mkono, liache kwanza. Rudi nyuma. Jipange. Huo ndio uongozi. Kungโangโania jambo linalopigwa na wengi, ni kutaka kushindana na maji ndani ya mkondo wake.