😁😁Ndo uone sasa kutenda haki kulivo kugumu pande zote mbili!!
Tusilaumu tu mbogamboga.
Tukipishana mawazo na makada wa ccm wanatuchoma kwa watekaji tunadakwa tunauliwa!!
Haya unapishana mawazo na mwanaharakati mwenzako anakuchomesha kwa ICE udakwe urudi home uuliwe!😁😁
Hapo kuna tofauti gani sasa?😁
Mulemule tu Nasoro na Cholo
Mkutano wangu na waandishi wa habari niliokuwa nifanye katika Hotel ya Golden Tulip nimeuahirisha.
Nimesikiliza hotuba za Makamu Mwenyekiti na Katibu Mkuu. Wameeleza vizuri kuhusu uvumi na upotoshaji uliokuwa ukifanyika juu yangu na misimamo juu ya chama chetu.
Nimedumu katika mapambano haya kwa zaidi ya miaka 22. Nimeenda lock-up zaidi ya mara 50. Nimezunguka nchi hii usiku na zaidi ya mara tatu. Nimewahi kuwa magerezani mara kadhaa, nimekoswa kuuawa zaidi ya mara tatu, na nimewahi kukimbia nchi.
Katika yote haya, nimekuwa nikitoa sadaka kubwa kwa ajili ya mapambano haya, ikiwemo ku-sacrifice familia yangu mara zote.
Kazi hii kwangu si ajira, si cheo, wala si njia ya kujitafutia maslahi. Ni huduma. Ni wito. Ni kama injili ninayoamini na kuitumikia.
Kwa hiyo, siwezi kuruhusu uvumi, upotoshaji au tafsiri za watu kuniondoa kwenye misingi ambayo nimeisimamia kwa zaidi ya miongo miwili.
Nitakuwa kwenye mapambano haya kwa imani, ujasiri na dhamira njema siku zote.
Sativa nakuelewa, mimi naamini wote tuna lengo moja (tunataka na kupigania mabadiliko nchini)
Tunaweza kutofautiana mitazamo lakini lengo letu bado likawa moja, tuzungumze mpaka tufanane mitazamo ili tutimize lengo!!
Mimi ni muhanga wa awali kabisa dhidi ya serikali hii dhalimu, mimi nimetekwa na kuwa tortured kabla ya wengi sana, yes kabla hata ya TAL!!
Nimetekwa na kuteswa April 5th-April 8th-2017, Baadae september ndio Lisu akashambuliwa Dodoma, wakafuata wakina Mo, Mdude,Wewe,Soka na wengine wengi!!
Since waliponitupa baharini usiku ule baada ya mateso makali 2017 bado sijapona, bado ninao uchungu na nawachukia watesi wale….pengine kuliko hata mtu anayeandika tu mtandaoni comments za kutukana ilhali hajawahi kulala hata kituo cha polisi cha mtaani kwa harakati hizi for just a single night.
Sasa pamoja na hizo hasira dhidi ya hawa watesi, bado niko na room ya huruma na upendo kwa watu wengine ambao watakutana na wanakutana na changamoto zinazofanana na hizo!!
Kinyume na hivyo nitakuwa sina tofauti na watesi!!
Hii inanifanya nikiona mtu yoyote anaanza kuunda utamaduni unaotaka kufanana na hawa watesi lazima nitamkemea!! Na hiyo ndio role ya #Activist anajikita kwenye agenda na sio taasisi!!
So lazima tuhakikishe kama ikitokea CDM akawa mbadala wa utawala wa sasa, nayeye asiwe na characters kama za mtawala huyu wa sasa!!
Kinyume na hapo tutakuwa ni waganga tunaeagua mgonjwa kwa kumtoa jini #Maimuna na kumkaribisha jini #Makata
Sa si bora hata maimuna unaweza ukalomba, makata vipi!?
Nimeona matusi na sintofahamu nyingi mtandaoni baada ya kuchapisha ujumbe wa kutoa pole kwa Mama Samia, hasa niliponukuu salamu za pole za Mwenyekiti Lissu kutoka gerezani.
Kwa sisi jamii tunaodai kupigania uhuru wa maoni na demokrasia, hili linapaswa kutufikirisha. Kutofautiana kwa hoja hakuhitaji matusi, dhihaka wala chuki.
Lissu amekaa gerezani takribani mwaka mmoja na miezi sita, akikabiliwa na kesi ambayo sisi tunaamini ni ya kisiasa na isiyo na haki. Anafahamu yaliyompata na serikali iliyomweka mahabusu. Lakini alipofahamishwa kuhusu msiba wa mume wa Mama Samia, akiwa mbele ya mahakama, alitoa salamu zake za pole kwa wafiwa mara mbili.
Huu si unyonge. Hii ni hekima, utu na ukomavu wa kiwango cha juu.
Na si mara ya kwanza. Aliwahi pia kumtetea Sabaya katika kesi yake Moshi. Wengi tulishangaa, nami nilishangaa. Lakini nilipomuuliza baadaye, nilielewa kwamba kwake haki haichagui upande.
Hilo ndilo fundisho kubwa tunalopaswa kulibeba. Tunaweza kupinga serikali, kudai haki na kupigania demokrasia bila kujenga harakati zetu juu ya chuki na kisasi.
Lakini kama tunasema tunampenda Lissu, basi pale anaposema ana pumzi ya kuvumilia mateso na kukaa gerezani, sisi tunapaswa kuchukua kauli hiyo kama mwito wa ujasiri, si ruhusa ya kukaa kimya.
Kama tunaamini kesi hii si ya haki, basi viongozi tunanapaswa kuwaongoza wananchi katika hatua za amani, kisheria na kidemokrasia za kudai haki, pengine kwa njia ya maandamano. Sio kwenye keyboard tu na microphone.
Demokrasia inahitaji wananchi wanaothubutu kusimama kwa kile wanachoamini. Na kama siku moja tutapata nafasi ya kuongoza nchi hii, tusije tukarudia makosa tunayoyapinga leo. Lazima tutawala kwa haki, utu na dhamira njema.
Mimi nitasimama kwenye upendo, utu na haki siku zote ktk kazi hii. Anyway , hekima ya Lissu kutoa pole kwa Mama Samia was a top-class thinking. Inaonyesha kwamba hata unapoteseka, unaweza kuchagua utu, hata unapopinga, unaweza kukataa kisasi.
Wakati mwingine Mungu hataki umshinde adui yako kwa chuki, bali kwa upendo, hekima na maisha yenye ushuhuda kwamba uovu wake haukukushinda.
Mimi niko tayari kusimama kwa amani na kwa ujasiri. Katika hatua ya kupigania uhuru wa Lissu kuwa nje ya kuta za gereza na sio kusema ana pumzi ya kukaa jela hata maisha. Tuna watu wengi sana Chama hiki , pumzi yetu itoke mtandaoni , fikeni tu hata mahakamani kwa sasa na huku viongozi wakuu watusaidie kutafakari jambo muhimu la haki , sheria na amani.
“You don’t have to hate those who hurt you. Sometimes the greatest revenge is to rise above them with peace, dignity, and success.”
Thank you !!
Ukiniuliza mimi, nitakwambia game ya chadema vs wanaharakati iko so tricky and kind’f complicated.
Kuna mmoja hapo anakuwa driven na hisia kuliko uhalisia wa siasa.
Chadema ni chama cha siasa, lengo lake kuu ni kushika dola, agenda yake kuu ni kupinga,kukosoa na kushauri serikali (chama tawala)
Kwenye hizo agenda kuu sasa ndo kuna tricky hapo, chadema inampasa kujiuza kwa wapiga kura kwa kuwaambia kuwa sisi hatuko hivo kama wao watawala na tukishika dola hatutayafanya haya na yale wanayofanya hawa watawala!!
Hatutaua, kwaio inabidi wasiue hata sasa.
Hatutaiba, inabidi wasiibe hata sasa.
Hatutafurahia tukiona binadamu amekufa au ameuliwa hata akiwa ni adui!! Na inabidi waanze kuonyesha hayo sasa.
Adui akifa au akifiwa tutaenda kuzika na tutaenda kuhani msibani!!
Yote haya ni ili chadema asionekane yeye naye ni roho mbaya tu kama alioko kwenye kiti!!
Kwahiyo chadema unakuta ana jukumu la kumpenda hadi adui ili kuonyesha watu kuwa sisi hatuko hivyo.
Otherwise mpiga kura ataona aaah mtawala wa sasa ni mkatili, lakini mbona hata huyu chadema nayeye anaonekana ni mkatili kabla hata hajashika dola!!🤔 Huyu akishika dola si ndio atakuwa katili zaidi ya wa sasa!!
Finally mtu anaamua bora shetani wa zamani niliemzoea kuliko shetani mpya!!
But kwa wanaharakati sasa ni tofauti…. hisia zinawapush wawe na mentality ya ngadu kwa ngadu,
🦷 kwa 🦷, mwaga bapa namwaga kichanganyio!!
Anayekuua na kukuteka na kukutesa, siku nayeye akifa angusha party kihomeboy shangilia!!
Its very complicated hii game!!
Ndo yale yale nasemaga, kama unamkosoa kiongozi wa chadema kwenye comment then akakublock means huyo siku akiwa tu DC ukakosoa anakutia ndichi masaa 72!!
Ni lazima anayempinga mtawala asiwe na characters za mtawala!!
Sijui kama niko sahihi au nimeamka na wenge!!