RAIS SAMIA KUZINDUA MELI YA UVUVI WA BAHARI KUU APRILI 25, 2026 - DKT BASHIRU
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassani anatarajiwa kuzindua Meli ya Kwanza ya Uvuvi wa Bahari Kuu , ambapo uzinduzi wake utafanyika Makao Makuu ya
Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO ) Kigamboni Jijini Dar es Salaam.
Mhe. Balozi Dkt. Bashiru amesema hayo Aprili 17, 2026, wakati wa ziara ya Kamati ya Uchumi na Uwekezaji ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar kutembelea na kukagua ujenzi wa bahari ya uvuvi Kilwa Masoko Mkoani Lind na kuieleza kamati hiyo kuwa bandari ya uvuvi Kilwa masoko iliyogharimu shilingi bilioni 280 baada ya kukamilika itafanyiwa majaribio kabla ya kukabidhiwa kwa serikali.
MNYIKA: WANAHARAKATI WAANZISHE CHAMA CHAO WASITUTEGEMEE CHADEMA
Tumesikia na kuona baadhi ya wanaharakati waliopo nje ya nchi wakitengeneza mazingira ya kutaka Mwenyekiti wetu abaki gerezani. Inabidi tutathmini jambo hili kwa kina, Chama chetu kina uongozi hakipaswi kutegemea mitazamo ya wanaharakati ambao hatujui malengo yao. Ikifika muda kama wataona tuna wadisapoint ni vyema waanzishe Chama chao kuepuka mgongano wa Maslahi.
Chanzo: EAST AFRICA RADIO
𝐇𝐈𝐒𝐓𝐎𝐑𝐈𝐀 𝐈𝐌𝐄𝐖𝐄𝐊𝐖𝐀
Kwa mara ya kwanza Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando, Mwanza imepandikiza figo.
Hospitali nyingine zinazotoa huduma hiyo nchini ni Hospitali ya Taifa Muhimbili na Hospitali ya Benjamin Mkapa.
#HABARI Iran imetangaza kuwa meli za Iraq zitaruhusiwa kupita kwa uhuru katika Mlango wa Bahari wa Hormuz, hatua inayomaanisha kupunguza udhibiti wake katika njia hiyo muhimu ya usafirishaji wa nishati ya mafuta Duniani.
Makao Makuu ya Khatam al-Anbiya ya Iran imesema kuwa Iraq haitakabiliwa na vikwazo vyovyote katika kupita katika mlango huo wa bahari, huku wakieleza heshima kwa uhuru wa taifa la Iraq na uhusiano wa karibu kati ya nchi hizo mbili.
Mlango wa Hormuz ni mojawapo ya njia muhimu zaidi duniani kwa usafirishaji wa mafuta na gesi, hivyo uamuzi huo una umuhimu mkubwa kiuchumi na kisiasa kimataifa.
Hata hivyo, Iran imesisitiza kuwa vikwazo vitaendelea kutumika kwa nchi inazozitaja kuwa “nchi adui,” hasa zile zinazohusishwa na migogoro au mashambulizi dhidi ya Iran.
Hatua hiyo inaonyesha kuwa Iran bado inadhibiti kwa karibu usafiri wa meli katika eneo hilo, na inatumia udhibiti huo kama sehemu ya mkakati wake wa kisiasa na kijeshi katika mgogoro unaoendelea katika Mashariki ya Kati. #EastAfricaTV
PASAKA ya Mwaka jana ilikukuta ndani ya kuta za Gereza Ukonga,
Pasaka ya Mwaka huu na yenyewe imekukuta ndani ya kuta za Gereza la Ukonga.
WEWE SIO MUHAINI
Wewe ni mtu wa Haki mwenye msimamo thabiti, wewe ni sauti ya Tanzania, wewe ni fahari yetu Watanzania wote ambao tuna mapenzi mema na Taifa letu.
Nduli Idd Amin Mama pamoja na washirika wake wanakuogopa sana, hawawezi kushindana na wewe kwa hoja so baada ya kuona kwamba hawana uwezo wa kujibu hoja zako wakaona wakubambike kesi ya Uhaini ili ukafie jela.
Wakati wanatamani wewe ufie jela, huku uraiani kila siku tunasikia wao wanakufa kwa mshtuko wa moyo.
Wanasahau kwamba Biblia inasema kwamba Mbeba maono hafi mpaka maono yatimie so wewe huwezi kufa kabla hujatimiza maono ambayo Mungu ameweka ndani yako ndo maana kila ambae alijaribu kukuuwa kwa namna yoyote ile Mungu alishughulika nae.
Hata aliyeagiza upigwe risasi 36, leo yupo kaburini hata huyu ambae anataka ufie jela naamini Mungu atashughulika nae.
Sisi tunaendelea kupambana huku tukimuomba Mungu.
Heri ya Pasaka Mwenyekiti wetu wa viwango, Mhe. Tundu Lissu.🙏
Wizara ya Mambo ya Nje ya Ufaransa imetangaza kwamba Mfaransa mwenye umri wa miaka 62 ambaye alikuwa amehukumiwa kifo na China kwa ulanguzi wa dawa za kulevya amenyongwa.
Ufaransa imesema alipatikana na hatia ya ulanguzi wa dawa za kulevya mnamo 2010.
Serikali ya Ufaransa imesema kwamba mtu huyo alikuwa hapaswi kuhukumiwa kifo, kwamba badala yake angepewa msamaha lakini ombi hilo halikukubaliwa kamwe.
Wizara ya Mambo ya Nje ya Ufaransa ilisema Mawakili hawakuruhusiwa kumwakilisha katika kesi yake ya mwisho katika Mji wa Guangzhou, Kusini mwa China.
Kifungu cha 347 cha sheria ya jinai ya China kinasema kuwa usafirishaji, usambazaji na utengenezaji wa dawa za kulevya ni uhalifu mkubwa.
Ukipatikana na hatia, unaweza kuadhibiwa kulingana na ukubwa wa uhalifu, na makosa madogo yanapata adhabu nyepesi, wakati uhalifu mkubwa unaweza kuhukumiwa kifungo cha maisha au adhabu ya kifo.
#KitengeUpdates
Wiki iliyopita niliingia kitu cha mafuta nikaweka Diesel lita 35 kwa sh 100,000.
Leo nimeweka diesel ya sh 100,000 ikawa lita 26.
Wiki iliyopita lita ya diesel ilikua 2854 Leo wiki moja baadae ni sh 3806.
Fikiria vijana wa bodaboda, Bajaji na watu wengine kwenye sekta ya usafirishaji..
Hii hali haikubaliki mtu wa chini ataumizwa mno na huu ufisadi kama hali hii haitabadilika..
Tutaongea kuhusu hili na tujue nani hasa wanataka kuwatesa Watanzania kwa manufaa ya urafi wao.
WILLIAM LUKUVI AFARIKI DUNIA
Dodoma, Machi 25, 2026 .
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetangaza kifo cha aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu) na Mbunge wa Isimani, William Vangimembe Lukuvi, kilichotokea leo majira ya saa moja asubuhi katika Hospitali ya Benjamin Mkapa, jijini Dodoma.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka, marehemu alifariki dunia alipokuwa akipatiwa matibabu kufuatia ugonjwa wa mshtuko wa moyo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ametangaza kwa masikitiko makubwa kifo hicho na kutoa salamu za pole kwa Spika wa Bunge, familia ya marehemu, wananchi wa Jimbo la Isimani pamoja na Watanzania wote.
Rais Samia amesema taifa limepoteza kiongozi mwenye uzoefu mkubwa na mchango mkubwa katika uongozi na maendeleo ya nchi, akieleza kuwa Lukuvi alikuwa mtumishi wa umma aliyejitolea kwa dhati katika majukumu yake.
Marehemu Lukuvi amewahi kushika nyadhifa mbalimbali serikalini kwa nyakati tofauti, akibaki kuwa mmoja wa viongozi waliotumikia taifa kwa muda mrefu na kwa ufanisi.
Taarifa zaidi kuhusu taratibu za mazishi zinatarajiwa kutolewa na serikali baadaye.
https://t.co/fQI7qI5hsM
*DK. SAMIA MZIKI MNENE*
Na Mwandishi Wetu
Siku chache baada ya kufikisha siku 100 ikulu, katika kipindi cha pili cha awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, Tanzania inaendelea kushuhudia kasi mpya ya maendeleo katika sekta mbalimbali za kijamii na kiuchumi.
Fuatilia mfululizo huu wa makala za kazi inaendelea na Dk. Samia Suluhu Hassan katika kuleta Tabasamu la Taifa.
MIUNDOMBINU
Serikali imeongeza kasi ya ujenzi wa barabara, madaraja makubwa na reli ya kisasa, hatua inayorahisisha usafirishaji na kukuza biashara za ndani na nje ya nchi.
Maboresho ya bandari na viwanja vya ndege yameongeza ushindani wa taifa katika uchumi wa kikanda.
UMEME
Miradi mikubwa ya uzalishaji umeme imekamilishwa na mingine kuimarishwa, hali iliyoongeza upatikanaji wa nishati ya uhakika kwa viwanda, biashara na makazi ya wananchi. Umeme umefika katika maeneo mengi zaidi vijijini, ukichochea shughuli za uzalishaji.
MAJI
Ujenzi na upanuzi wa miradi ya maji safi na salama umeboresha huduma kwa wananchi wa mijini na vijijini.
Wananchi wengi sasa wanapata maji karibu na makazi yao, kupunguza adha ya kutembea umbali mrefu kuyatafuta.
AFYA
Kuanzishwa kwa Bima ya Afya kwa Wote kumeleta matumaini mapya kwa wananchi, huku hospitali zikiboreshwa kwa vifaa tiba na wataalamu zaidi.
Upatikanaji wa dawa na huduma za msingi umeimarika katika maeneo mengi.
ELIMU
Sera ya elimu bila malipo imeendelea kuimarishwa kuanzia msingi hadi sekondari.
Mabadiliko ya mitaala yamelenga kuwajengea wanafunzi ujuzi wa kisasa, ubunifu na stadi za maisha zinazoendana na mahitaji ya soko la ajira.
KILIMO
Sekta ya kilimo imepewa kipaumbele kupitia ruzuku za pembejeo, mikopo nafuu na juhudi za kufungua masoko ya uhakika kwa mazao ya wakulima, hatua inayoongeza tija na kipato chao.
MADINI
Mageuzi katika sekta ya madini yameongeza uwazi na mapato ya taifa, huku wachimbaji wadogo wakipewa msaada wa kitaalamu na masoko bora.
Uongezaji thamani ndani ya nchi umeanza kuimarika.
UTALII
Kupitia kampeni za kimataifa na maboresho ya miundombinu, sekta ya utalii imeendelea kukua, kuongeza mapato ya fedha za kigeni na ajira kwa vijana.
AJIRA
Fursa za ajira zimeongezeka kupitia miradi ya maendeleo, ukuaji wa sekta binafsi na uwekezaji mpya unaoendelea kuvutiwa nchini.
SAPOTI KWA WAJASIRIAMALI
Serikali imeendelea kuweka mazingira rafiki ya biashara kwa kurahisisha usajili na upatikanaji wa mikopo kwa vijana na wanawake, hatua inayochochea ukuaji wa biashara ndogo na za kati.
UHUSIANO WA KIMATAIFA
Diplomasia ya uchumi imeimarisha mahusiano ya Tanzania na mataifa mbalimbali, kufungua milango ya uwekezaji, mikataba ya maendeleo na ushirikiano wa kibiashara.
MAONI YA WANANCHI
Wananchi wengi wanaeleza kuiona kasi ya maendeleo katika maeneo yao, wakisema maboresho ya miundombinu, afya, elimu na ajira yanaonekana kwa vitendo na kuongeza matumaini ya maisha bora zaidi.
Kaa tayari kupata uchambuzi wa sekta kwa sekta, mkoa kwa mkoa na taasisi kwa taasisi katika mfululizo wa makala maalum za Kazi inaendelea na Dk. Samia Suluhu Hassan katika kuleta Tabasamu kwa Taifa.
Makala hizo zitaletwa kwenu kupitia magazeti ya JAMVI MEDIA GROUP na vyombo vingine katika njia za mtandao, magazeti, redio na Tv.

uteuzi huu unaonesha chama kimewachagua viongozi waliokwisha pimwa, kuaminiwa na kukubalika,hatua inayofuata ni uthibitisho wa kikatiba. Tz Bara waliopitishwa ni Paul Christian Makonda, Livingstone Joseph Lusinde na Asia Halamga, Zanzibar ikiwakilishwa na Khamis Omar na Tauhida.
DK. SAMIA MWENDO MDUNDO
Anachanja Mbuga Kanda ya Ziwa, Bukombe Yatingisha kwa 'MASHINE' Biteko
Na Mwandishi Wetu – Geita
Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameendelea kuchanja mbuga katika mikutano yake ya kampeni inayoendelea nchini kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi huu. Katika mwendelezo wa ziara zake Kanda ya Ziwa, Dkt. Samia amepokelewa kwa shangwe na maelfu ya wananchi waliomiminika kumshuhudia na kusikiliza sera za maendeleo anazoendelea kuzisemea kwa nguvu.
Akizungumza jana katika mikutano mikubwa wa kampeni iliofanyika Ushirombo, Runzewe - Bukombe, na ule wa awali uliofanyika Mbogwe mkoani Geita, Dkt. Samia aliwapigia wananchi saluti kwa umoja wao na kuwashukuru kwa kumwamini yeye pamoja na serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika kutekeleza miradi ya maendeleo inayoleta matokeo halisi kwa wananchi.
Katika mkutano hiyo iliofurika wananchi, Rais Samia alimsifia Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko, akimwelezea kama “MASHINE” iliyothibitisha uwezo wake kwa vitendo.
“Nataka niwaambie, mmeniletea MASHINE. Mmeniletea kijana ambaye nilimuamini kumfanya awe Naibu Waziri Mkuu, kijana ambaye anatusaidia sana kazi zetu. Na kwa sababu ya hiyo, nanyi mkamuheshimu — hakuna mwingine aliyejitokeza,” alisema Dkt. Samia huku akishangiliwa kwa nguvu na wananchi wa Bukombe.
Kanda ya Ziwa yaendelea kung’aa kwa miradi mikubwa
Ziara ya Dkt. Samia Kanda ya Ziwa imekuwa sio tu ya kisiasa, bali ni onyesho la matokeo ya kazi kubwa iliyotekelezwa na serikali yake katika kipindi cha miaka minne iliyopita. Kanda hii imekuwa kinara wa miradi mikubwa ya kimkakati katika sekta za miundombinu, maji, nishati, kilimo na madini.
Miongoni mwa miradi hiyo ni Daraja la Busisi lenye urefu wa zaidi ya kilomita 3.2 linalounganisha mikoa ya Mwanza na Geita, mradi ambao ukikamilika utarahisisha usafiri na usafirishaji wa bidhaa kutoka maeneo ya uzalishaji hadi masoko, hususan sekta ya uvuvi, kilimo na madini.
Vilevile, serikali imetekeleza kwa kasi miradi ya maji vijijini na mijini kupitia mamlaka mbalimbali za maji na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA), ambapo maelfu ya wananchi wa maeneo ya Geita, Chato, Misungwi, Sengerema na Bukombe sasa wanapata huduma ya maji safi na salama karibu na makazi yao — hatua iliyopunguza adha kubwa kwa wanawake na watoto.
Katika sekta ya kilimo, Rais Samia ameongeza bajeti ya pembejeo kwa wakulima wa pamba, mpunga, na mahindi, huku ruzuku ya mbolea na mbegu bora ikiimarisha uzalishaji na kipato cha wakulima. Serikali imewezesha pia upanuzi wa skimu za umwagiliaji katika maeneo ya Magu, Nyang’hwale, na Shinyanga, hatua inayosaidia kilimo cha uhakika hata katika vipindi vya ukame.
Sekta ya madini nayo imepiga hatua kubwa. Kanda ya Ziwa sasa imekuwa injini ya uchumi wa madini nchini, huku shughuli za uchimbaji zikisukumwa na sera rafiki kwa wachimbaji wadogo, na ujenzi wa vituo vya ukusanyaji na uchenjuaji madini ukiendelea kwa kasi katika Geita, Chunya na Kahama.
Bukombe, wilaya inayong’ara leo kwenye kampeni, imepata pia neema ya miradi mipya ya kimkakati ikiwemo ujenzi wa Uwanja wa mpira wa Ushirombo, unaotarajiwa kufungua fursa za kiuchumi, utalii na biashara kwa mkoa mzima wa Geita kwa timu mbalimbali kuutumia utakapokamilika.
Hamasa ya ushindi yazidi kupanda
Wachambuzi wa siasa wanasema kampeni za Dkt. Samia Kanda ya Ziwa zimekuwa zenye mwamko mkubwa kuliko kipindi chochote, zikionekana kama sherehe za kutathmini matunda ya uongozi wake. Maelfu ya wananchi wamejitokeza katika kila eneo, wakiwa na mabango na ujumbe wa kumpongeza kwa utekelezaji wa miradi inayogusa maisha yao moja kwa moja.
Kwa wengi, Kanda ya Ziwa imekuwa kielelezo cha “maendeleo yanayoonekana” chini ya uongozi wa Dkt. Samia — maendeleo yanayojengwa juu ya dira ya umoja, utulivu na kazi.
#Samia2025 #MwendoMdundo #Bukombe #MASHINE #KandaYaZiwa #CCM #KaziInaendelea #TanzaniaMpya

NI ZAMU YA VYOMBO VYA HABARI..?
Waandishi wa habari nguli na maarufu wa radio na TV maarufu hapa Jijini Dar es Salaam wamefungiwa na Bodi ya ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) kutangaza au kufanya kazi ya uandishi wa Habari kwa kile kinachoitwa "kushindwa kujisajili katika bodi ya ithibati"
Mpaka naandika habari hii Wahusika na mwaajiri wao wamefanya siri kwa mujibu wa maelekezo waliyopewa na serikali kuwa "wasifanye kazi ya uandishi wa habari na wasiseme lolote kuhusu kuzuiwa kwao"
Kwa mujibu wa kifungu cha 19 cha sheria ya huduma za habari sura ya 229 kina weka masharti kuwa
"waandishi watakaoshindwa kujisajili hawataruhusiwa kufanya kazi za kihabari"
Waandishi hawa wamewekewa kikwazo hiki baada ya kuwa mwiba katika vipindi vyao na mahojiano yao kwa wakati huu nchi inapoelekea katika uchaguzi Mkuu
Uchunguzi unaonyesha Masoud Kipanya ameingia katika kifungo hiko baada ya kuchora mchoro wa katuni uliowakasirisha watawala uliolenga kutaka media zisitumike kama Toilet Paper
Mwenyekiti wa Jukwa la Wahariri Tanzania Balile aliongea na kuonyesha hadharani kukasirishwa na mchoro huo huku akiahidi Masoud Kipanya achunguzwe na mamlaka za nchi.
Masoud Kipanya na Ciza Wameshindwa kujisajili kwa sababu ya kukosa sifa ya kusomea taaluma ya uandishi wa Habari kinyume na sheria kama inavyoelekezwa katika kifungu cha 24 cha sheria ya huduma za habari sura ya 229.
Rungu la namna hii pia linaonekana kumkumba mwanahabari na Mkurugenzi wa Jambo TV, John Marwa ambaye amekuwa mwiba katika mahojiano mbalimbali na kuendesha vipindi vilivyo wakwaza watawala.
Duniani kote watu wenye uzoefu na kazi ya uandishi wa habari kwa zaidi ya miaka 10 kama Masoud Kipanya, SIZA, na John Marwa walipaswa automatically kuwa na sifa za kusajiliwa na bodi ya ithibati ya Waandishi wa Habari kwa kigezo cha uzoefu na muda waliofayia kazi tasnia ya habari.
Hawa ni baadhi ya Waandishi wa Habari wakubwa Duniani ambao hawakusomea taaluma ya uandishi wa Habari Anderson Cooper (CNN na ABC News) Stephen A. Smith (ESPN) na Trevor McDonald (ITN na ITV)
N.B
Kwa upande wa mmoja mtangazaji maaurufu wa radio na Tv kutoka ofisi hiyo hiyo, kwake maarufu kama imekuwa tofauti kidogo. Pamoja na kukidhia sifa zote za Sheria ya Huduma ya Habari na Kujisajili katika Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari
Wenye Mamlaka wamepiga simu kwa mwajiri wake na kumtaka aondolewe katika majukumu yake kwa kile walichokiita "mkosoaji sana"
Boniface Jacob
The voice of the Silenced Majority.
DJ Fete,
Kupitia maumivu ya kusimamishwa kazi kwa sababu ya msimamo wako, najua si rahisi lakini naamini ndani yako kuna kitu kikubwa, msimamo wa kweli, ujasiri na heshima kwa dhamira yako. Walio kusimamisha wana mamlaka ya leo, lakini Mungu ndiye anayeshika kesho.Usiogope. Mara nyingi mlango unapofungwa kwa nguvu, ni ishara kuwa Mungu anafungua mlango mkubwa zaidi , mlango wa heshima, wa uhuru, na wa mafanikio yasiyotegemea mnyororo wa hofu. Endelea kuwa mwaminifu kwa kweli, msimamo, na utu wako maana kesho ni bora kwako kuliko jana.Mbele yako kuna mlango usiofungwa na mkono wa mwanadamu. Much ❤️
Nimemsikiliza Gwajima.
Nahisi ana stress, ameongea bila kuweka nukta.
Anauliza waandishi wa habari kama kuna swali huku akijua kuwa anaji stream mwenyewe peke yake.
Nadhani ni miongoni mwa watu wanaostahili kupuuzwa kama wanavyopuuzwa wajinga wengine.