VIDEO:
Wadau mbalimbali kwa sasa wanaweza kuwekeza katika ujenzi wa vituo vya mafuta katika maeneo ya vijijini, baada ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kupunguza gharama za uwekezaji na masharti ya uombaji wa leseni, hatua inayolenga kuondoa uuzaji holela wa nishati hiyo katika maeneo hayo.
Hayo yamesemwa na Meneja wa EWURA Kanda ya Ziwa, Mhandisi Nyirabu Musira, wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye Maonesho ya Tisa ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea katika Viwanja vya Dk. Samia Suluhu Hassan, mkoani Geita.
Musira amesema EWURA imetambua umuhimu wa upatikanaji wa nishati ya mafuta kwa wananchi wa vijijini, hivyo imechukua hatua za kupunguza masharti pamoja na gharama za uombaji wa leseni ili kuwavutia wawekezaji kuanzisha vituo vya mafuta katika maeneo hayo.
Amesema hatua hiyo inalenga kuhakikisha wananchi wa maeneo ya vijijini wanapata huduma ya mafuta kwa njia rasmi na salama, huku ikisaidia kupunguza utegemezi na uuzaji holela wa mafuta ambao unaweza kuhatarisha usalama wa wananchi na mazingira.
Kwa upande wake, Afisa wa Mahusiano kutoka EWURA, Thobietha Makafu, amesema mamlaka hiyo imejipanga kutoa elimu ya kutosha kwa wananchi kuhusu udhibiti wa huduma za maji na nishati, pamoja na kuwafahamisha wadau kuhusu taratibu na matakwa ya kisheria katika utoaji wa huduma hizo.
Makafu amesema elimu hiyo itasaidia wananchi na wawekezaji kuelewa wajibu wao, huku ikichangia upatikanaji wa huduma bora na salama za maji na nishati nchini.
VIDEO:
Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padre Dkt. Charles Kitima, amebainisha kuwa kuvurugwa na kuondolewa kwa dhana ya ushindani wa haki wa kisiasa ndicho chanzo kikuu kilichoharibu mfumo wa uchaguzi na misingi ya demokrasia nchini.
Kauli hiyo imetolewa leo, Septemba 15, 2026, mkoani Dar es Salaam wakati Padre Kitima akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Demokrasia Duniani yaliyoratibiwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC).
Akirejea msingi wa kihistoria wa taifa, Padre Kitima ameeleza kuwa Mwalimu Julius Nyerere aliweka msingi thabiti baada ya uhuru kwamba uhalali wa kiongozi kuongoza lazima utokane na ushindani wa haki na wa wazi kutoka kwa wananchi, kulingana na misingi ya Katiba inayoeleza kuwa uongozi ni dhamana na wananchi ndio wenye mamlaka ya utawala
"Mwaka 1962 Nyerere alisema siwezi kuwa rais wa nchi bila kuchaguliwa na wananchi baada ya kuwa tumepata uhuru tarehe 9 Disemba 1961, akasema lazima nichaguliwe nipate kile kitu kinaitwa legitimacy... ule uhalali wa kuongoza upatikane kwa ushindani ulio halali unaotoka kwa wapiga kura wananchi wenyewe. Kwa sababu tunaamini na Nyerere alijaribu kujitahidi sana kuaminisha Watanzania kwamba uongozi ni dhamana", ameeleza Padre Kitima.
Akifafanua kuhusu sababu zilizofanya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 kuwa na idadi kubwa ya wagombea urais waliofikia 17 ukilinganisha na chaguzi za nyuma, Padre Kitima amefafanua kuwa hali hiyo haikutokana na kukua kwa demokrasia, bali ilitokana na mbinu za makusudi za kuondoa ushindani halisi wa kisiasa ulioanza kubomolewa tangu mwaka 2019 na 2020.
Ameongeza kuwa michakato hiyo ya kisiasa ilianza kuvurugwa kuanzia ndani ya vyama vya siasa kabla hata ya kufika kwenye uchaguzi mkuu.
#UPDATES Kupitia mtandao wa X Mbunge na Waziri wa zamani wa Ardhi, Prof. Anna Tibaijuka amesema uamuzi wa Rais wa Marekani Donald Trump kusitisha misaada kwa mashirika ya afya duniani kama GLOBAL FUND na PEPFAR iwapo yatatekelezwa ni kiama.
"Upatikanaji wa madawa ya kuongeza kinga za mwili ARVs utaathirika. Ninashauri Wizara ya Afya kuufahamisha umma wa waTanzania je ni hatua gani za haraka zinachukuliwa kutathmini jambo hili na kuchukua hatua stahiki?."
"Ikibidi African Union waitishe kikao maalum kuangalia swala hili na kuweka mkakati wa pamoja. Waathirika wa gonjwa hili la UKIMWI ni waAfrika na ugonjwa haujulikani ulitoka wapi?. Tujitetee."
"Aidha juhudi za kuthibiti maambukizi ya virus vya ukimwi ziwekewe nguvu mpya. Upatikanaji wa ARVs utakuwa mgumu. Na kununua ARVs kibiashara ni jambo litakalohitaji bajeti kubwa na uwezo wa taifa kwa ujumla ni mdogo. Na jambo limekuwa la ghafla. Waathirika wengi hawana uwezo kununua madawa hayo wenyewe maisha yao yote. Afya zao zikidhoofika itatumika gharama kubwa kuwauguza hivo kusababisha umaskini na vifo. Pia bila ARVs maambukizi yatashika kasi mpya. Tuwe macho" amesema Tibaijuka. #EastAfricaTV
Captain Ibrahim Traoré ndiye headliner wa Energy Summit. Media na waandishi wote watakuwa na macho kwake—mwanaume huyu wa shoka kutoka Burkina Faso! Ninasubiri kuona kama atafanya kama Ghana, alipoingia full geared na wanajeshi wake, akivunja protocols za kimataifa. 🔥