Kamati yaTAMISEMI tukijadili changamoto ya kuharibika miundombinu ya Barabara inayotokana na Mvua kubwa zinazoendelea. Serikali imelipa suala hili Uzito mkubwa na kazi imeshaanza kwa baadhi ya maeneo. Pole sote tunaoathirika na adha hii kubwa. Kazkaz @ortamisemitz
KUHUSU MUSWADA WA JANA, Ingekuwa ni hatari kubwa kama Askari wa Kificho asingeshitakiwa kwa Makosa ya Jinai aliyotenda wakati akitekeleza majukumu hayo. Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe Spika, Wabunge wenzangu tumeupiga mwingi HEKO, wakienda nje ya Maadili na Kanuni WASHITAKIWE.
Tundu Lissu ni Makamu Mkiti wa CHADEMA, alikuwa Mnadhimu wangu bungeni. Ni Kaka na rafiki yangu, alijeruhiwa vibaya na nilimsindikiza airport Dodoma usiku ule akienda Nairobi kwa matibabu. Nisipoenda kumpokea hata shetani atanishangaa. #TunduLissuHomeComing
Kugombea kupitia upinzani ni maisha ya roho mkononi kila wakati. Kufutiwa uraia, kubambikiwa kesi, kufilisiwa, kutekwa, kujeruhiwa, kuuawa, na kuteswa kisaikolojia. Ni utitiri wa visa na hofu. Unashika fomu ya kugombea mkono mmoja na mkono wa pili unaandika wosia.