"Daima kuna wanaokubali, wanaopinga na kuna wanaokaa kimya. Wanaokaa kimya inawezekana wana hoja nzuri ila hawana ujasiri wa kusema, wa kupaza sauti au wa kulumbana. Wape nafasi ya kuwasikiliza, inawezekana ndio wenye majawabu." ~Togolani Mavura.
"Sisi wazazi wa watoto wa kike, ombi letu kwa wazazi wa watoto wa kiume ni kuwalea watoto wenu wajue kujali, kusamehe, na kuwa na imani kwa wanawake. Sisi tukiwaandaa wanetu wa kike kuwa wake na mama wema haisaidii sana ikiwa ninyi hamuwaandai wenu kuwa waume na baba bora."