"Ikiwa kila mtu anamuomba Mungu ombi lake kwa wakati wake, basi majibu ya Mungu kwetu hayawezi kuwa ya aina moja wakati mmoja. Vuta subira." ~Togolani Mavura.
Ee Mungu mwenye upendo na rehema,
Asante kwa kuniamsha salama siku hii mpya,
na kwa kunipa nafasi ya kuuona mwezi huu mpya.
Naomba baraka zako ziwe juu yangu,
Uniongoze katika kila ninalofanya,
Unilinde na mabaya yote,
Na unijalie afya, amani, na mafanikio.
Nisaidie kuwa na moyo wa shukrani,
na kuenenda kwa haki na upendo.
Katika jina lako takatifu, naomba. Amina.