unaandaa document alafu unampa ChatGPT akiitoa unampa Gemini akiitoa unampa Claude akiitoa unampa AI humanizer kubabaake Akiitoa unaisave unatupia kwenye email una CC dunia kazi imenyooka vipi watu ni miluzi tu mpaka mtu mwenye utindio na uelewa mdogo anaielewa report😀🙌🏾
Fahamu Kwa Undani Ugonjwa Wa Tetanus (Pepopunda).
Chanzo cha tetanus, dalili zake, tiba na kinga ya tetanus.
Open Thread 🧵, Like & Repost 🔄 Kwa Ajili ya Wengine..!
KUZALIWA KWA MARYAM MAMA YAKE NABII ISSA (amani iwe juu yao) NA KULELEWA KWAKE.
• Hannah binti Faaquudh alikuwa mke wa Bwana 'Imraan.
Inasemekana kwamba hakujaaliwa kupata watoto. Kuna siku moja Bi. Hannah aliona ndege akimlisha kinda wake. Alipoona hivyo akatamani sana kupata mtoto akaomba Dua kwa Mwenyezi Mungu amjaalie kizazi. Mwenyezi Mungu akakubali Dua yake, akashika ujauzito.
Bi. Hannah akaweka nadhiri ya kumfanya mwanae awe ni mwenye kumtumikia Mwenyezi Mungu katika ibada, na kuihudumia Baytul Maqdis (Masjidil Aqswa). Alipotambua kuwa amebeba ujauzito ndiyo akaweka nadhiri hiyo.
📌 {Na kumbuka pindi aliposema mke wa ‘Imraan: Ewe Mola wangu, hakika mimi nimeweka nadhiri Kwako kilichomo katika tumbo langu kuwa ni wakfu kukutumikia, basi nikubalie. Hakika wewe ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua}.
- Surah: Al-'Imraan - Ayah: 35.
• Wala hakujua kama atajaaliwa mtoto wa kiume au wa kike. Alipojifungua mtoto wa kike aliona kwamba mwanamke sio kama mwanaume katika kumtumikia Mwenyezi Mungu Msikitini.
📌 {Basi alipomzaa akasema: Ewe Mola wangu, hakika mimi nimezaa mwanamke, na Mwenyezi Mungu anajua zaidi alichokizaa. Na mwanamme si sawa na mwanamke. Nami nimemwita Mayram, nami namkinga Kwako na kizazi chake kutokana na shaytwaani aliyewekwa mbali na kulaaniwa}.
- Surah: Al-'Imraan - Ayah: 36.
✍️ Maryam Maana yake ni “Mtumishi wa Mwenyezi Mungu” (Mwenye kumtumikia Mwenyezi Mungu kwa kufanya ibada).
• Kama Ayah ilivyomalizikia kwamba Bibi Hannah alimuomba Mwenyezi Mungu amkinge Maryam na kizazi chake kutokana na shaytwaan.
Mwenyezi Mungu akamkubalia Dua yake, na ushahidi wa kukubaliwa Dua yake upo kwenye Hadithi ifuatayo.
📌 Kutoka kwa Abu Hurayrah (Allah amridhie):
Mtume Muhammad (swalla llaahu 'alayhi wa sallam) amesema:
“Hakuna kizazi chochote kinachozaliwa ila shaytwaani anakigusa kinapozaliwa, na mtoto huanza kulia kwa sababu ya kuguswa huko, isipokuwa Maryam na mtoto wake (yaani Issa).”
- Bukhari na Muslim.
• Akapelekwa Maryam tokea utoto wake msikitini na akakulia huko na akamtoa kama ni zawadi ya Baytul-Maqdis.
Lakini ikatokea mivutano na kuanza kugombana, ni nani atakayemlea Maryam?! Kila mmoja alitaka kumlea Maryam. Basi ikabidi wapige kura ya kutupa kalamu zao kwenye mto. Yule ambaye kalamu yake itaelea katika mto ndiye atakayemlea Maryam. Walipozitupa kalamu zao, zote zilizama isipokuwa Kalamu ya Nabii Zakariya (amani iwe juu yake) ambaye alikuwa ni bwana wao, mwanachuoni wao na pia ni Nabii wao.
• Mwenyezi Mungu anampa kisa hiki Nabii Muhammad (rehma na amani ziwe juu yake) katika Wahyi (ufunuo), kisha anawazindua makafiri kwamba hizi ni habari za ghaibu ambazo hakuzijua Mtume (swalla llaahu 'alayhi wa sallam) kabla.
Qur'an si maneno ya Nabii kama wanavyodai makafiri.
📌 “Hizo ni habari za ghaibu tunakufunulia Wahyi (Ewe Muhammad). Na hukuwa pamoja nao walipotupa kalamu zao, ili nani kati yao amlee Maryam. Na hukuwa pamoja nao pindi walipogombana.”
- Surah: Al-'Imraan - Ayah: 44.
• Tukirudia kisa alipozaliwa Maryam.
Mwenyezi Mungu alikubali nadhiri ya mama yake, akamjaalia Maryam kuwa na tabia njema na kupata elimu ya dini yake kutoka kwa Nabii Zakariya (amani iwe juu yake), mpaka akawa mchamungu kwelikweli. Kutwa kucha alikuwa akifanya ibada.
• Ikawa kila mara Nabii Zakariya anapoingia katika Mihraabu (sehemu yake Maryam aliyokuwa akifanyia ibada) anamkuta ana vyakula. Ndipo alipomuuliza kama yanavyokuja maelezo katika Ayah ifuatayo:
📌 “Basi Mola wake akampokea (Maryam) kwa mapokeo mema, na akamkuza makuzi mazuri, na akamfanya Zakariya kuwa mlezi wake. Kila Zakariya alipoingia kwake katika chumba cha kufanyia ibada, alikuta kwake kuna vyakula. Akasema: Ewe Maryam! Umepata wapi hivi? Akasema: Hivi ni kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu anamruzuku amtakaye bila ya hesabu.”
- Surah: Al-'Imraan - Ayah: 37.
✍️ MWISHO.
أحبك حباً لو تحول إلى ماء لغرق العالم
#غرام
Nakupenda upendo ambao lau kama (upendo huo) ungebadilika na kuwa maji, basi Dunia yote ingezama.
#HubaZito
Hukmu ya Muziki kwenye Qur'an Na Sunnah.
Ewe Upendaye Nyimbo na Muziki, hivi haujafika wakati wa kuogopa adhabu kali za Allah?
📌 Muziki ni haramu kutokana na dalili dhahiri tulizopewa katika Qur'an na Hadith za Nabi wa Allah (rehma na amani ziwe juu yake).
Baadhi wa watu bado hawajatambua uharamu wa jambo hili, tunasikia wengi bado wanaimba taarabu na aina nyingine za nyimbo na muziki. Na mara kwa mara unapompa nasaha ndugu yako Muislamu kuacha maasi haya, jibu mara nyingi huwa: "Tena nyinyi mmezidi! Wapi dini inasema kuwa nyimbo haramu?!" Au wengine waliobobea katika maradhi haya hunena: "Mimi yote naweza kuacha lakini nyimbo utaniua!" Husema hivyo bila ya kujali amri ya makatazo ya Muumba wake ambaye ni Muweza wa kufutilia mbali masikio yake awe kiziwi na asiweze kusikia tena hizo nyimbo.
📌 Inafika hadi Muislam hawezi kulala hadi alazwe kwa muziki, hawezi kula ila muziki uwe unapigwa, hawezi kufanya kazi za nyumbani bila muziki kufunguliwa, hawezi kufanya kazi akiwa kazini… hawezi kusafiri… hawezi kufanya mazoezi bila kuwepo na muziki wa kumchochea na kumtia hamasa (kama wanavyoitakidi) ya lile analolifanya kwa wakati huo.
Kwa kila hali, muziki umekuwa ni sehemu kubwa ya maisha ya mwanadamu ambaye bado yupo kwenye maasi haya.
Hivyo tumeona kuna umuhimu mkubwa wa kuwakumbusha ndugu zetu waepukane na haramu hii ili wajiokoe na adhabu za Allah.
📌 Amesema Allah Mtukufu:
• {Na miongoni mwa watu yuko ambaye hununua maneno ya upuuzi ili apoteze (watu) njia ya Allah bila elimu, na huichukulia mzaha. Hao watapata adhabu yenye kudhalilisha}.
• {Na anaposomewa Ayah Zetu, hugeuka huku akitakabari kama kwamba hazisikii, kama kwamba kuna uziwi masikioni mwake, basi mbashirie adhabu iumizayo.
📚 [Luqmaan 6-7]
Ibn Mas'ud (Allah amridhie) amesema kuhusu Ayah hii "Naapa kwa Allah hii inamaanisha ni kuimba (muziki)."
📚[At-Twabariy 20:127]
Na Ibn 'Abbas (Allah amridhie) pia amesema kuhusu Ayah: ((Na miongoni mwa watu yuko ambaye hununua maneno ya upuuzi)) amesema: "Ni nyimbo na maneno yanayofanana (ya upuuzi)."
📚[Swahihi Adab al-Mufrad (603)]
📌 Na dalili za maharamisho na maonyo katika Sunnah ni zifuatazo:
1• Uharamu wa ngoma.
Kutoka kwa 'Abdullaah bin ‘Abbas: ((Hakika Allah Ameharamisha pombe na kamari na kuwbah na kila kilinacholewesha ni haramu)) [Swahihi Al-Jaami’i(7336)]
Na katika usimulizi mwingine: Sufyaan amesema: Nilimuliza 'Aliy ibn Budhaymah: "Nini Kuwbah?" Akasema: "Ngoma". [Swahihi Abi Dawud: (3696).
Tahadhari yasije kukukuta mauti ukiwa katika kusikiliza au kuimba muziki, kwani mtu atafufuliwa na matendo yake ya mwisho.
Kutoka kwa Jaabir bin 'Abdillaah: "Nimemsikia Nabii (rehma na amani ziwe juu yake) ((Kila mja atafufuliwa katika hali aliyofia nayo))
📚[Muslim]
Je, ndugu Muislamu unayependa muziki, umetafakari vipi utakuwa mwisho wako? Je, haikuingii hofu katika moyo wako kuwa huenda mwisho wako ukawa ni kuimba nyimbo badala ya kusema "Laa ilaaha illa Llah" neno ambalo ukilitaja mwisho wa maisha yako wakati wa kufa utaingia Jannah?
📌 Muongozo na Nasaha ya Kujiepusha kusikiliza Nyimbo, Muziki na kucheza Ngomba:
Tusikilize Na Kusoma Qur'an.
Muziki na nyimbo humjaza mtu mapenzi makubwa moyoni, zimshughulishe zaidi hadi asiwe na muda wa Qur'an ambayo ndio ipasayo kukaririwa midomoni mwetu kwa sauti nzuri.
📌 Hata hivyo, upo wakati ambao mashairi yanaruhusiwa kuimbwa bila ya kuwepo kwa ala za muziki isipokuwa dufu tu kwa wanawake. Na hali hizo ni kama:
1. Wakati wa Jihadi na mapambano mengine katika Njia ya Allah aliyetukuka. Mtume wa Allah (rehma na amani ziwe juu yake) alikuwa akiimba wakati wa Vita vya Khandaq. (Muslim).
2. Wakati wa sherehe za Kiislamu kama Eid al-Fitwr na Eid Al-Adhwha.
3. Pia ruhusa imetolewa kwa wanawake na wasichana kuimba na kupiga dufu wakati wa harusi. (Baadhi ya wanazuoni wamejuzisha pia kupiga dufu kwa wanaume wakati wa harusi).
📌 Na Allah ni Mjuzi zaidi.
MWISHO.
IBADA YA SWALA (NAMNA YA KUSWALI).
🔴 Kwanza tufahamu nini maana ya Swala?
• Swala (صَلَاةٌ) kilugha ni: Dua / Maombi.
• Ama Swala kisheria ni: Kumuabudu Allah Mtukufu kwa maneno na vitendo maalum, vinavyoanzwa kwa kuleta Takbiira (Yaani kwa kusema "Allaahu Akbar), na vinavyohitimishwa kwa kutoa salaam (Kwa kusema "Assalaamu 'alaykum warahmatullaah").
✍️ Unapoleta Takbiira unakuwa tayari umeingia rasmi kwenye ibada ya swala, na unapotoa salaam tayari unakuwa umetoka nje ya swala (umemaliza kuswali).
1.📌 Ataianza ibada ya Swala kwa kusimama na kuelekea Qibla (Mwili wake wote uwe umeelekea Qibla bila kupinda).
2.📌 Kisha atatia nia moyoni.
3.📌 Kisha ataleta Takbiira ya kuhirimia swala, yaani atasema: "Allaahu Akbar", na huku akinyanyua mikono yake sambamba na Takbiira (Yaani wakati analeta Takbiira basi anyanyue mikono yake).
Anyanyue mikono usawa na mabega yake, au usawa na masikio yake.
4.📌 Kisha mkono wake wa kulia atauweka juu ya mkono wake wa kushoto. Mikono yote iwe juu ya kifua chake.
5.📌 Kisha atasoma Dua ya kufungua Swala (Dua ya ufunguzi wa Swala). Atasema:
( Subhaanaka Allaahumma wabihamdika, watabaarakasmuka, wata'aalaa jadduka, walaa ilaaha ghairuka ).
✍️ TAFSIRI YA DUA HII.
( Utukufu ni wako ewe Allah, na sifa njema zote ni zako, na limetukuka jina lako, na umekuwa juu utukufu wako, na hakuna mwabudiwa wa haki isipokuwa wewe ).
6.📌 Kisha atasema: A'uudhu billaahi mina shaytwaani Rrajiim.
7.📌 Kisha atasoma Suratul Faatiha, kwa kuanza kusoma "Bismi llaahi Rrahmaani Rrahiim".
Akimaliza kusoma Suratul Faatiha atasema "Aamiin" Kisha atasoma Surah nyingine yoyote kwenye Rakaa mbili za kwanza za Swala ya Dhuhri, 'Aswri, Maghribi, Ishaa na Fajri. Ama rakaa ya tatu na ya nne kwenye Swala ya Dhuhri na 'Aswri, na rakaa ya tatu kwenye Swala ya Maghribi, na rakaa ya tatu na ya nne kwenye Swala ya Ishaa atasoma Suratul Faatiha tu (hasomi Surah nyingine).
8.📌 Kisha atarukuu huku akisema: "Allaahu Akbar". Na atashika magoti yake huku akiviachanisha vidole vyake vya mikono, na macho yake yaangalie sehemu ya kusujudu. Na atasema: Subhaana Rabbiyal 'adhwiim (mara tatu).
9.📌 Kisha atainuka kutoka kwenye rukuu huku akisema: Sami'a llaahu liman hamidah, na atasimama sawasawa (yaani atasimama akiwa amenyooka vizuri), kisha atasema: Rabbanaa walakal hamdu.
10.📌 Kisha ataenda kusujudu huku akisema: Allaahu Akbar." Na atasujudu kwa viungo vyake saba, navyo ni:
- Paji la uso na pua.
- Viganja viwili vya mikono.
- Magoti mawili.
- Ncha za miguu miwili (Yaani vidole vya miguu).
✍️ Viungo hivi ni lazima viguse chini pindi mtu anapokuwa amesujudu.
11.📌 Wakati akiwa amesujudu atasema: Subhaana Rabbiyal a'alaa (mara tatu).
Wakati akiwa amesujudu anatakiwa kuigusanisha miguu yake. Kisha atainuka huku akisema: "Allaahu Akbar", na atakaa kitako. Kisha atasoma Dua kati ya sijda mbili (Yaani akiwa amekaa kitako kabla ya kusujudu mara ya pili basi alete dua). Atasema: Rabbighfir lii.
12.📌 Kisha atasujudu sijda ya pili kwa namna ileile ya sijda ya kwanza.
13.📌 Kisha atanyanyuka juu (kwa ajili ya kuswali rakaa ya pili) huku akisema: Allaahu Akbar.
Kisha atasoma Suratul Faatiha na Surah nyingine yoyote. Baada ya kisomo cha rakaa ya pili atarukuu na atasujudu kama alivyofanya kwenye rakaa ya kwanza. (Yaani zile dua/adhkaari ambazo alisoma kwenye rakaa ya kwanza basi atasoma pia kwenye rakaa zingine zilizobaki).
🔴 TASHAHUDI YA KWANZA (ATAHIYAATU NDOGO).
✍️ Tashahudi ya kwanza ataisoma akiwa amekaa kitako baada ya kuswali rakaa mbili za mwanzo za Swala ya Dhuhri, 'Aswri, Maghribi na 'Ishaa. Atasema:
Attahiyyaatu lillaahi waswalawaatu watwayyibaatu assalaamu 'alayka ayyuha Nnabiyyu warahmatullaahi wabarakaatuhu, assalaamu 'alaynaa wa 'alaa 'ibaadi llaahi swaalihiin. Ash-hadu allaa ilaaha illa llaah, wa ash-hadu anna Muhammadan 'abduhu warasuuluhu.
🔴 TASHAHUDI YA MWISHO (ATAHIYAATU KUBWA).
✍️ Tashahudi ya mwisho ataisoma baada ya kumaliza kuswali rakaa ya mwisho ya kila Swala.
• Atasema: ⬇️
Nikisema Nakupenda Nitasafiri umbali nikuone, Nitapoteza vyote nisikukose.. ..Ungeficha Sura Mwili bado ningezimia Ubongo wako tuu...Sijui ni Umbo Sura au Nywele ni kama vile una Magic...
#HubaZito 😎
simkumbuki .. Nitamkumbuka vipi wakati siwezi kumsahau?
📌 Ewe unaedhani kwamba mimi simkumbuki .. Mwenyezi Mungu anajua kwamba siwezi kumsahau.
📌 Akiwa mbali nami kwenye roho yangu ndiyo makazi yake .. Anayeishi ndani ya roho, moyo utawezaje kumsahau?.
#HubaZito
"Napenda siku zetu ziendelee kuwa na furaha kama leo, na upendo wetu uongezeke kama vile unavyoongeza mwanga katika maisha yangu. Jioni njema, mpenzi wangu wa thamani."
#hubazito
Uliza Chochote Kwangu; Niombe Chochote Unachohitaji Na Niamrishe Chochote Unachohitaji Kama Si Katika Maasi Ntakutimizia Kwa Upendo Wangu Wote Kwani Mimi Naishi Maisha Yangu Yote Kwa Ajili Yako Wewe
#hubazito
ما كنت أؤمن بالعيون وسحرها
حتى دهتني في الهوى عيناكِ.❤️
#غرام
Mwanzo nilikuwa siamini kama macho yana maajabu .. Mpaka pale nilipokamatika kwa macho yako.
#HubaZito