Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko akipokea zawadi ya maua kutoka kwa Mwenyekiti wa India Pulses and Grains Association (IPGA), Bimar Kothar wakati wa Mkutano wa mazao jamii ya mikunde uliofanyika Februari 13, 2025 jijini New Delhi nchini India
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi akizungumza na Balozi wa Uganda nchini Tanzania, Mhe. Kanali (mst) Fred Mwesigye, aliyefika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, jijini Dar Es Salaam, kwa ajili ya mazungumzo, Jumatano tarehe 12 Februari 2025.
📍Bungeni,Dodoma
📷HOTUBA YA KUAHIRISHA MKUTANO WA 18 WA BUNGE LA 12
“Tuzo ya Global Goalkeeper Award aliyopewa Rais Dkt. Samia ni kielelezo cha utashi wake katika kuharakisha kufikia malengo Endelevu,”
-Waziri Mkuu Kassim Majaliwa 📷:O/Waziri Mkuu📹
#sisinitanzania #maendeleo #tanzaniampya #sisinitanzaniampya #tanzaniayetu #tanzanianamaendeleo #tanzania #samiasuluhu #ssh #sisinitanzaniamakini
Halmashauri ya jiji la Tanga dawati la msaada wakisheria,jana limefanikiwa kujitambulisha na kutoa elimu katika kata za majengo na chumbageni ambazo ni kata za mwisho kati ya kata 27 ambazo dawati limezunguka katika kata hizi zote
MAAFISA MAENDELEO DAWATI LA MSAADA WA KISHERIA JIJI LA ARUSHA WATOA MAFUNZO DHIDI YA UKATILI WA KIJINSIA KATIKA SHULE YA MSINGI MSASANI B.
Maafisa Maendeleo kutoka Dawati la Msaada wa Kisheria katika Halmashauri ya Jiji la Arusha wametembelea Shule ya Msingi Msasani B na kutoa mafunzo maalum kwa wanafunzi kuhusu ukatili wa kijinsia na njia bora za kujilinda dhidi ya vitendo hivyo.
Katika mafunzo hayo, wanafunzi walielimishwa kuhusu aina mbalimbali za ukatili wa kijinsia, athari zake kwa wahanga na jamii kwa ujumla, pamoja na hatua za kuchukua ili kujikinga na kuripoti matukio ya ukatili. Mafunzo hayo yalilenga kuongeza uelewa wa watoto kuhusu haki zao na kuwajengea ujasiri wa kupinga ukatili wa aina yoyote katika mazingira yao ya kila siku.
Maafisa hao walisisitiza umuhimu wa kushirikiana na wazazi, walimu, na viongozi wa jamii katika kupambana na ukatili wa kijinsia, huku wakihamasisha wanafunzi kuwa mabalozi wa mabadiliko kwa wenzao.
Hatua hii ni sehemu ya jitihada za serikali na wadau wa haki za binadamu katika kuhakikisha watoto wanalelewa katika mazingira salama na yenye ulinzi dhidi ya unyanyasaji wa kijinsia.
#MSLAC #KatibanaSheria #SSH #CCM #KaziIendelee #NchiyanguKwanza #SisiniTanzania #matokeochanya
Jengo la Kitega Uchumi Tanga – Maendeleo kwa Ustawi wa Jiji
Jengo hili la kisasa limejengwa kwa gharama ya bilioni 8.8 kutoka Serikali Kuu. Lipo Kata ya Maweni, Mtaa wa Kange, karibu na Stendi Kuu. Litakuwa na Maafisa Biashara kwa ajili ya kuimarisha uchumi wa Tanga.
#SSH#CCM #KaziIendelee #Nchiyangukwanza #SisiniTanzania #matokeochanya @samia_suluhu_hassan @ikulu_mawasiliano @dr_philip_isdor_mpango
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bole, Addis Ababa nchini Ethiopia tarehe 14 Februari, 2025 kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa kawaida wa 38 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU). Pamoja na mambo mengine pia Mhe. Rais Dkt. Samia atashiriki mkutano wa Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika
Wanafunzi wa shule ya sekondari Kwembago, kata ya Magamba. Wilaya ya Lushoto wafikiwa na MSLAC na wadau wengine wa Sheria. Wamepewa elimu ya Ukatili wa kijinsia na madhara ya rushwa wawapo ndani na nje ya Shule.
@SuluhuSamia#SisiNdioWajenziWaTanzaniaYetu#KaziIendelee #Nchiyangukwanza
#matokeochanya #sisinitanzania #SSH
Mkoa wa Mbeya Umekusanya Shilingi Bilioni 2.3 za maduhuli ya Sekta ya Madini kwa kipindi cha cha miezi saba kuanzia mwezi wa saba (Julai, 2024 mpaka Januari, 2025).
Maduhuli hayo ni sawa na asilimia 63 ya lengo la mwaka la kukusanya Shilingi Bilioni 3.7 ifikapo mwezi Juni mwaka 2025
Pakua Samia App kupitia Play Store au App Store.
#samiaapp
#kaziiendelee
#tumejipatanamama
ELIMU YA MSAADA WA KISHERIA YAWEZESHA WANAFUNZI NA WALIMU SHULE YA MSINGI ORKIRUNG'RUNG
Simanjiro, Tanzania – Wanafunzi na walimu wa Shule ya Msingi Orkirung'rung, iliyopo katika Kijiji cha Orkirung'rung, Kata ya Endonyongijape, Wilaya ya Simanjiro, wamepatiwa elimu muhimu kuhusu haki za mtoto na madhara ya ukatili wa kijinsia.
Elimu hii ya msaada wa kisheria ilitolewa kwa lengo la kuwajengea uelewa na kuwawezesha wanafunzi na walimu kutambua haki zao, kujikinga na ukatili wa kijinsia, na kujifunza namna ya kuripoti matukio ya ukiukwaji wa haki za watoto.
Katika kampeni hiyo, Afisa wa Dawati la Msaada wa Kisheria aliambatana na watetezi wa haki za binadamu kutoka jamii ya wafugaji, ambao walishiriki kikamilifu katika kutoa mafunzo hayo. Ushiriki wa wanajamii katika kutoa elimu hii umeongeza ushawishi wa ujumbe wa kulinda haki za watoto na kupinga ukatili wa kijinsia katika jamii ya wafugaji.
Wananchi wa eneo hilo wamepokea mafunzo hayo kwa shukrani kubwa, wakisema kuwa elimu hii itasaidia kupunguza visa vya ukatili wa kijinsia na unyanyasaji wa watoto. Walimu wa Shule ya Msingi Orkirung'rung pia wameonyesha utayari wa kuhakikisha kwamba elimu hiyo inaendelezwa kwa wanafunzi na jamii kwa ujumla.
Mafunzo haya ni sehemu ya jitihada za kuimarisha uelewa wa haki za binadamu, hususan miongoni mwa watoto na vijana, ili kujenga jamii inayothamini na kulinda haki za kila mmoja.
@ikulu_mawasiliano @ikulu_habari @samia_suluhu_hassan @kassim_m_majaliwa
@DBiteko@sisiniTanzania
@airtanzania_atcl @arusha_nationalpark #sisinitanzania #maendeleo #tanzaniampya #sisinitanzaniampya #tanzaniayetu #tanzanianamaendeleo #tanzania #samiasuluhu #ssh #sisinitanzaniamakini #sisinitanzania #tanzaniabora #millardayo #updates #news #habari #habarimpya #News
Mkutano wa Hadhara Kijijini Roondoo Watoa Elimu ya Msaada wa Kisheria kwa Wananchi
Katika jitihada za kuimarisha uelewa wa wananchi kuhusu haki zao za kisheria, mkutano wa hadhara umefanyika katika Kijiji cha Roondoo, Kata ya Romu, ambapo wananchi walipata fursa ya kupokea elimu kuhusu huduma ya msaada wa kisheria.
Wananchi walionyesha furaha na shukrani kwa elimu waliyopewa, wakisisitiza umuhimu wa elimu hiyo kuwa endelevu ili kuendelea kuwasaidia katika kutatua changamoto mbalimbali za kisheria zinazowakabili.
Mkutano huu ni sehemu ya juhudi zinazoendelea za kuhakikisha wananchi wanapata uelewa mpana wa haki zao na namna ya kuzitetea kupitia taratibu za kisheria.
#MSLAC #KatibanaSheria #SSH #CCM #KaziIendelee #NchiyanguKwanza #SisiniTanzania #matokeochanya
Kituo cha Afya Tongoni – Halmashauri ya Jiji la Tanga
Kituo hiki kinahudumia wananchi wa Kata ya Tongoni, Pogwe, Kirare, na Marungu. Sasa kimeimarishwa kwa kuongeza jengo la upasuaji, wodi ya mama na mtoto, pamoja na sehemu ya kufulia nguo ili kuboresha huduma za afya kwa jamii.
#SSH #CCM #KaziIendelee #Nchiyangukwanza #SisiniTanzania #matokeochanya @samia_suluhu_hassan @ikulu_mawasiliano @dr_philip_isdor_mpango
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Jamhuri ya Uganda nchini Tanzania Mhe. Kanali Mstaafu Fred Mwesigye, mazungumzo yaliyofanyika Ikulu Chamwino mkoani Dodoma leo tarehe 13 Februari 2025.
Katika mazungumzo hayo, Makamu wa Rais amesema Tanzania na Uganda zimekua na uhusiano sio tu wa kihistoria bali wa kindugu. Amesema Tanzania inafuraha kuendelea kushirikiana na Uganda kwenye masuala mbalimbali katika Jumuiya za Kimataifa kama vile Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika na Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Makamu wa Rais amesema Tanzania na Uganda ni muhimu kuendelea kushirikiana kiuchumi ikiwemo kuongeza kiwango cha ufanyaji biashara pamoja na kuendelea kufanya kazi pamoja katika utafiti wa kilimo, kubadilishana maarifa kuhusu kilimo cha kisasa na mazao yanayohimili ukame pamoja na udhibiti wa magonjwa yanayovuka mipaka.
Halikadhalika Makamu wa Rais amesema Tanzania imeendelea na jitihada za kuboresha miundombinu na nishati ili kuimarisha biashara na uwekezaji ikiwemo ujenzi wa bwawa la kufua umeme la Mwalimu Nyerere, ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) kuboresha bandari ya Dar es Salaam pamoja na kuimarisha mifumo ya kidigitali ya utoaji na usafirishaji mizigo ili kurahisisha usafirishaji wa bidhaa mbalimbali.
Kwa upande wake Balozi wa Jamhuri ya Uganda nchini Tanzania Mhe. Kanali Mstaafu Fred Mwesigye ameishukuru Tanzania na viongozi wake kwa kuendeleza maono ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambaye alijitolea kusaidia nchi za Afrika ikiwemo Uganda kujikomboa na kupata uhuru.
Ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kukubali kupitisha mafuta yaliyogunduliwa nchini Uganda kupitia bomba la mafuta linalotoka Hoima hadi Chongoleani mkoani Tanga. Amesema ujenzi wa bomba hilo la mafuta umekuwa msaada wa kiuchumi na kijamii katika maeneo linalopita kabla hata ya mafuta hayo kuanza kupitishwa.