Katika demokrasia:
Mahakama ni kubwa kuliko Jaji Mkuu.
Bunge ni kubwa kuliko Spika.
Taifa ni kubwa kuliko Rais.
Katiba ni kubwa kuliko chama tawala.
Hii ni kwa sababu taasisi zinapaswa kudumu, wakati viongozi ni wa muda.
1. TAIFA NI KUBWA KULIKO RAIS
Rais ni kiongozi wa muda.
Taifa ni la kudumu.
Rais anaweza kukaa madarakani miaka 5, 10 au 20.
Lakini taifa linaendelea kuwepo kabla yake na baada yake.
Mfano:
United States imekuwa na marais wengi sana.
Wamekuja:
Ronald Reagan
Bill Clinton
Barack Obama
Donald Trump
Lakini Marekani imebaki kuwa Marekani.
Rais ni mtumishi wa taifa.
Taifa si mali ya Rais.
Ndiyo maana katika demokrasia, kumpinga Rais si sawa na kulichukia taifa.
Na kumuunga mkono Rais si sawa na kuwa mzalendo.
Uzalendo ni kuipenda nchi hata pale unapokosoa serikali.
2. SERIKALI SI TAIFA
Hili ndilo eneo ambalo watu wengi huchanganyikiwa.
Serikali ni chombo kinachosimamia nchi kwa kipindi fulani.
Taifa ni wananchi wote pamoja na historia, ardhi, taasisi na mustakabali wao.
Kwa mfano:
Leo serikali inaweza kubadilika.
Lakini:
Tanzania inabaki Tanzania.
Bendera inabaki ile ile.
Wananchi wanabaki wale wale.
Historia inabaki ile ile.
Kwa hiyo:
Kuikosoa serikali si kuisaliti nchi.
Na:
Kuisifu serikali si lazima iwe kuipenda nchi.
Swali muhimu ni:
“Je jambo hili linafaidisha taifa?”
si “Je jambo hili linaifurahisha serikali?”
3. CHAMA TAWALA SI SAWA NA NCHI
Hili ni somo muhimu sana kwa Afrika.
Katika demokrasia:
Chama tawala ni mshindi wa uchaguzi.
Hakimiliki taifa. Hakimiliki serikali milele.
Hakimiliki uzalendo.
Taifa ni mali ya:
waliokichagua chama tawala,
wasiokichagua chama tawala,
na hata wale ambao hawakupiga kura.
Ndiyo maana katika nchi zilizoendelea kisiasa:
Ukikosoa chama tawala huonekani adui wa taifa.
Unaonekana sehemu ya demokrasia.
Tatizo linaanza pale chama tawala kinapoanza kuonekana kama taifa lenyewe. Hapo demokrasia huanza kudhoofika.
4. KATIBA NI KUBWA KULIKO CHAMA TAWALA
Katiba ndiyo mkataba mkuu wa taifa.
Katiba ndiyo inayotoa mamlaka kwa:
Rais, Bunge Mahakama.
Sio Rais anayeipa Katiba nguvu.
Ni Katiba ndiyo inayompa Rais nguvu.
Sio chama tawala kinachounda taifa.
Ni Katiba ndiyo inayoweka sheria za namna taifa litakavyoendeshwa.
Katika demokrasia iliyokomaa:
Kama chama tawala kinataka jambo ambalo Katiba hairuhusu,
Katiba ndiyo hushinda.
Kwa sababu Katiba inawakilisha taifa lote.
Chama kinawakilisha wanachama wake.
5. BUNGE NI KUBWA KULIKO SPIKA
Spika ni kiongozi wa muda.
Lakini Bunge ni taasisi ya kudumu.
Leo kuna Spika mmoja.
Kesho atakuwepo mwingine.
Lakini Bunge linaendelea kuwepo.
Hii ndiyo sababu taasisi ni muhimu kuliko watu.
Mtu anaweza kuondoka.
Taasisi inapaswa kubaki imara.
6. MAHAKAMA NI KUBWA KULIKO JAJI MKUU
Jaji Mkuu ni mtumishi wa Mahakama.
Sio Mahakama mali ya Jaji Mkuu.
Kesho Jaji Mkuu akistaafu:
Mahakama inaendelea.
Hii ndiyo maana ya utawala wa sheria.
Sheria inapaswa kuwa kubwa kuliko watu wanaozisimamia.
TATIZO KUBWA AFRIKA
Katika nchi nyingi za Afrika watu hufikiri hivi:
Chama = Taifa
Serikali = Taifa
Rais = Taifa
Kukosoa Serikali = Kuisaliti nchi
Hiyo ndiyo sababu mjadala wa kisiasa huwa mgumu.
Kwa sababu watu wanafikiri wanalinda taifa wakati mara nyingi wanakuwa wanalinda serikali au chama.
Lakini katika demokrasia yenye afya:
Taifa ni kubwa kuliko serikali.
Serikali ni kubwa kuliko chama.
Katiba ni kubwa kuliko serikali.
Sheria ni kubwa kuliko viongozi.
Dhamira ni kubwa kuliko utii wa kipofu.
Kwa lugha rahisi sana
Ukiniuliza tofauti kati ya nchi, taifa na serikali ningesema:
Nchi ni ardhi, mipaka na mamlaka yake.
Taifa ni watu wake, historia yao, utamaduni wao, taasisi zao na mustakabali wao.
Serikali ni timu ya muda iliyopewa jukumu la kuendesha taifa kwa kipindi fulani.
Ndiyo maana unaweza kubadilisha serikali bila kubadilisha taifa.
Lakini ukiharibu taifa, hata serikali nzuri haiwezi kulirudisha kwa urahisi.
Kwa hiyo kiongozi wa kweli hapaswi kuuliza:
“Je hili linaisaidia serikali?”
Bali: “Je hili linaimarisha taifa, taasisi zake, na vizazi vijavyo?
𝐒𝐢𝐤𝐮 𝐲𝐚 𝐖𝐚𝐭𝐨𝐭𝐨 𝐃𝐮𝐧𝐢𝐚𝐧𝐢.
Tanzania ina jumla ya Watoto 𝟑𝟎,𝟐𝟓𝟕,𝟏𝟗𝟔 (yaani watu walio na umri chini ya miaka 18). Kutokana na umri wao mdogo, jamii imepewa jukumu la kutimiza haki zao na kuwawezesha watoto nao kutimiza wajibu wao.
Nimepokea Taarifa za kukamatwa kwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bwana @TunduALissu pamoja na viongozi wengine wa Chama hicho kwa masikitiko makubwa. Nawasihi Jeshi la Polisi @tanpol wamwachie huru Lissu mara moja na bila masharti yeyote ili aendelee na shughuli zake za kisiasa kwa mujibu wa Katiba na Sheria za Nchi yetu. Wengi tunaamini kuwa enzi za kukamata viongozi wa kisiasa zimepitwa na wakati na Ndio maana Vyama vinafanya mikutano ya Hadhara bila hatari yeyote kwa Wananchi wala Serikali yenyewe. Jeshi la Polisi litafute namna bora ya kuzungumza na wanasiasa pale ambapo kuna kutoelewana na Waachene na hii tabia ya kukamata kamata Watu na kuwazuia kufanya shughuli zao. Jeshi la Polisi liwaachie mara moja Tundu, Catherine, Mama Kiwanga na wote wengine waliokamatwa Leo huko Arusha
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dokta Samia Suluhu Hassan ameshawasili jijiji Arusha kushiriki maadhimisho ya siku ya kupinga matumizi ya dawa za kulevya duniani inayoadhimishwa kitaifa jijini Arusha leo tarehe 25 Juni 2023.
Akiwa njiani kuelekea Arusha Rais Dokta Samia alisimama eneo la Tengeru na kuzungumza na wananchi wakiojitokea kumpokea. Akizungumza na wananchi hao alisema;
"Kama mnavyo jua kuwa kesho tunajambo muhimu Arusha kuhusu dawa za kulevya,siku hii siyo kwa ajili ya kusherehekea hapana bali ni kwa ajili ya kuangalia hali halisi nchini kwetu na kuondoa yake yote ambayo yamepelekea watu wetu kuingia katika mambo hayo"
#KigogoMediaUpdates
We have tried everything! We have tried everything! We gave it our all! We dreamed of it like crazy 😩! yes We deserved it like Kings but alas the man proposes God disposes, We will come back even stronger Inshallah by the grace of God. Big thank you to all ☘️🔰🙏
Hongereni sana Yanga kwa hitimisho la mchezo wa Fainali ya Kombe la Shirikisho (CAF Confederation Cup). Historia mliyoandika katika safari yenu ya michuano hii ni kubwa na ya heshima kwa Taifa letu. Nawatakia kheri katika mipango yenu ya siku zijazo.
Mwana Utajiri Wake Umeanguka Kwa TSH. Trilioni 16.1 Ndani Ya Muda Huu Ambao Insta Na FB Hazifanyi Kazi!!
Tunamsindikiza Sana Mwana Kwenye Utajiri Aiseee….Kama Nime Catch Hivi
@mshambuliaji@mzeewakaliua Then kosa kubwa ni serikali kuweka nguvu kuhimiza watu kupata vitambulisho hivyo ilihali wanajua bado havitoshi kujustify uraia. Waanze Kwa kuipa value National Id ili waloyonayo wawe ni raia pekee na si wasio raia
@mshambuliaji@mzeewakaliua then pamoja na viambatanisho vyote tunavyotoa ili kupata kitambulisho icho cha taifa (viambatanisho ambavyo vyote ni muhimu katika kujustify urai) halafu mwisho wa siku kuna wasio raia wanapata kitambulisho na baadae serikali inatoa matamko kuwa National Id sio kielelezo tosha...
@mshambuliaji@mzeewakaliua Daah hapo kwenye National ID, kama serikali yetu itakuwa inasema sio kielelezo tosha cha uraia then kuna sehemu wamekosea wanapaswa kuboresha. Kama procedure za kukipata inatutaka tutoe vyeti vya kuzaliwa, utambulisho wa serikali za mtaa, historia za mahali tumezaliwa, tumesoma..
"Kuweni watulivu" na bado mnaendelea kukata hela za watu. Ili muonekane serious kwenye huo utulivu mnaouhitaji, sitisheni hayo makato kwanza mpaka mtakapopata muafaka kama kweli nyie ni wasikivu kama mnavyojinadi.
Kuna ka script kaliandikwa kusapoti tozo. Ma influencers wakatambaa nako weee... Leo kametoka ka script kengine ka "serikali yenu ni sikivu" ma influencer hao hao wanatambaa nako tena.
😂😂😂