#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 496
Upande wa mashtaka walieleza kuwa kauli ya mshtakiwa inatakuwa itazamwe katika muktadha mzima kuwa aliitishia serikali na kuwa mshtakiwa alikuwa na lengo la kuitisha serikali regardless kama serikali ilitishika au la!
Ushahidi wa upande wa utetezi mshtakiwa alisema maneno hayo lazima yapimwe katika muktadha wa kisiasa na lengo kwa kauli hiyo ilikuwa ni kueleza msimamo wa kisiasa wa Chadema na lengo lake halikuwa kuitishia Serikali, mtazamo huu ulingwa mkono na shahidi wa 2,3,4 na 5 kuwa kauli ya No reforms, No election ililenga kueleza ushawishi wa kisiasa.
Upande wa utetezi ulisema neno uasi lazima nilitazamwe katika muktadha wa kisiasa na kauli hiyo haikuwa na lengo la kuitishia Serikali au kuchochea vurugu.
Mshtakiwa alieleza kuwa upande wa mashtaka walipaswa kuthibitisha nia hiyo kuwa mshtakiwa alilenga kuitishia serikali na sio hisia tu. Mshtakiwa alieleza kuwa upande wa mashtaka walishindwa kuthibitisha
Kwa ushahidi uliotolewa kuna mambo ambayo hayabishaniwi, kwanza Chadema imekuwa inatetea mabadiliko ya kikatiba, na mfumo wa uchaguzi na msimamo wa No reforms, No election, kupitia mkutano huo wa 3/4/2025 mshtakiwa alitoa hayo maneno mbele ya viongozi wenzake, wanachama, watia nia na waandishi wa habari na mkutano huo ulirushwa live.
Upande wa utetezi wamemaintain kuwa kauli hiyo ni ya kisiasa ililenga umma to boycott uchaguzi na sio kuitishia serikali.
Tumeangalia kauli zilizotolewa na mshtakiwa na tumeona kuwa hakuna ushahidi wa moja kwa moja hatujaona kuwa mshtakiwa alilenga kuitishia Serikali, tumeangalia tafsiri ya shahidi wa 1,2 na 16 tumeona ni assumption haziwezi kuthibitisha kuwa mshtakiwa alilenga kuitishia Serikali.
Tumeona kwamba ushahidi uliotolewa na mashtaka una fall short kuthibitisha shitaka la uhaini hivyo katika kiini hiki cha pili tunaona ushahidi haujakidhi kuonyesha nia ya uhaini.
Kwa mujibu wa kifungu cha 39(2)(d) kuna vitu vitatu ikiwemo factuai issues, mahakama lazima iangalie ushahidi kujiridhisha na tatu ni ushahidi uoi umetolewa.
Mahakama inaona kwamba tafsiri ya maneno ya Lissu bila tangible evidence tumeongozwa na kanuni kwamba nia (mens rea) ni internal state of mind lazima liambatane na ushahidi wa kimazingira na vitendo vya kufanya uhaini.
Nia ovu siku zote inakuwa inferred kutoka kwa maneno na matendo ya mshtakiwa.
Part 497 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.
#FreeTunduLissu
As the word.awaits the final judgement in the treason trial against Tanzanian opposition leader @TunduALissu, Tanzanian activist Deus Valenine argues that it is in fact the Tanzanian Judiciary that is in the dock:
"Silence on binding precedent is not judicial restraint. It looks a great deal like capture".
https://t.co/uZsEJ821ZZ
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema, Tundu Lissu, ameingia ndani ya Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, tayari kwa kusikiliza hukumu ya kesi ya uhaini inayomkabili.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Leo November 6, 2026
Last time tuliishia part 493 so leo tunaendelea na -;
Part 494.
Karani amewasha kipaza sauti kutoa Tangazo kuwa watu wakae kwenye viti vyao na simu zao wahakikishe zinatolewa sauti na milio ya aina yote.
Waandishi wa Habari na wao wako wakutosha sijawahi kuwaona Mahakamani kwenye kesi yoyote wakiwa wa idadi hii ni wengi sana sana.
Hata waandishi ambao huwa hawajagi kabisa naona wamekuja, namuona yule Charles William wa Wasafi nae leo yupo kuna mtiti hapa unataka kutokea, wanataka kumnyayua Mzee Mpoki alienda kukaa viti vya Mawakili wa Serikali ๐๐๐
Wale watoto wa serikali ambao huwa wanakaa kwenye benchi la nyuma ya akina Katuga, leo wamekaa mawakili wa Mhe. wabishi hatari wamegoma kusimama.
Ameingia Mheshimiwa Lissu akiwa na vibe na kusema TUTAFIKA! TUTAFIKA! TUTAFIKA!
Wameingia Mawakili wa Serikali.
MAJAJI walikwisha ingia hata kabla Mawakili wa Serikali hawajaingia.
Muda huu wanawasha zile mic zao ili tuendelee.
Jaji Ndunguru anasema karani tuendeleeee.
Jamhuri dhidi ya Lissu. Anasoma namba ya shauri karani.
Anasimama Katuga anajitambulisha niko na wenzangu Job Mrema, Cathbert mbiringe ba Winniwa Kasala
Tunaiwakilisha Jamhuri na Mshitakiwa yupo.
Shauri linakuja kwa ajili ya uamuzi na upande wa Jamhuri tuko tayari.
Mshitakiwa vipi wewe?
Mheshimiwa Lissu anasema niko tayari pia.
Majaji Wanateta pale kabla hawajaanza kuusoma huo uamuzi.
Jaji Ndunguru anasoma, naomba tusikilize Hukumu.
Katika shauri hili Mshitakiwa Tundu Lissu anashitakiwa kwa kosa la uhaini kinyume na kifungu cha 39(2)d kanuni ya Adhabu 2023.
Maelezo yanasema kwamba Tarehe 03/04/2025 Wilaya ya Kinondoni Dar es salaam mshitakiwa alitengeneza nia ya kuzuia uchaguzi wa 2025 kwa lengo la kuitishia Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Kudhihirisha nia hiyo kwa kitendo cha kutamka maneno ya wanasema kitu kimoja sahihi kwamba msimamo huu unaashiria uasi na tutahamasisha uasi na hiyo ndio namna ya kuleta mabadiliko na huu uchaguzi tutauvuruga.
Mshitakiwa alikana hati ya mashitaka na shauri likaanza kusikilizwa.
Kama ilivyo kawaida upande wa Mashitaka waliongozwa na Wakili Renatus Mkude na Ajuaye Zengeli na Nasoro Katuga na anawataja Mawakili wote wa Serikali.
Upande wa Mashitaka walileta mashahidi 17 na ambao kati yao 17 walikuwa ni mashahidi wanaolindwa.
Na mshitakiwa alijiwakilisha Mwenyewe na alileta Mashahidi wanne na yeye alikuwa watano na pia utetezi walitoa vielelezo anbavyo ni 16.
Baada ya upande wa mashitaka kutoa ushahidi na mshitakiwa alijitetea na walileta hoja za majumuisho walileta hoja hizo.
Mahakama hii iliongozwa na kanuni mbalimbali ni
1. Katika Mashauri ya Jinai mwenye jukumu la kuthibitisha ni Upande wa Mashitaka.
2. Kutiwa hatiani kwa mshitakiwa hakutazingatia udhaifu wa mshitakiwa.
3. Ushahidi utatazamwa kwa ujumla wake na sio vipande.
4. Mashaka yoyote hata kama yana uzito kiasi gani hayabadilishi burden ya kuthibitisha shitaka.
Mahakama hii imechunguza kwa umakini hati ya mashtaka, ushahidi na mawasilisho ya pande zote mbili na kuja viini vitatu vya kuthibitisha
Moja: Iwapo Mshtakiwa alikuwa chini ya utii wa JMT
Mbili: Iwapo Mshtakiwa alitengeneza nia ya kuzuia uchaguzi mkuu wa 2025 kwa lengo la kuitishia serikali.
Tatu: Iwapo mshtakiwa alidhihirisha nia hiyo kwa kutamka na kusambaza maneno hayo.
Mahakama imeona ni vyema ifafanue kwanza katika hoja ambazo zinaonekana kama mapingamizi wakati wa hoja za majumuisho ya mshtakiwa.
Kwa kuwa hati ya mashtaka ndio inayoanzisha shauri la jinai ni vyema tuamue kwanza kuhusu uhalali wa hati ya mashtaka. Mshtakiwa alisema hati ya mashtaka ina mapungufu katika maeneo matatu moja kuwa kwa mujibu wa kifungu cha 39(2)(d) kinazungumzia kuhamasisha kikundi cha watu, pili hati ya mashtaka haikutoa taarifa muhimu ambazo zilipelekea ashindwe kutoa utetezi kamili na tatu hakuna lengo lilioonyeshwa katika hati ya mashtaka.
Part 495 itaendele kwenye post inayofuata
Naomba Repost yako.
Dear Kenyans, I must inform you that while the world waits for Tundu Lissu's fate tomorrow, he confirmed that he is leaning on a Kenyan fighter. Koigi wa Wamwere's I Refuse to Die is the book keeping his spirit unbroken in prison. Some struggles refuse to stay inside one country
Binafsi naamini Tundu Lissu anatabasamu moyoni huku akijisemea yale maneno ya Yesu:
Msinililie mimi; jililieni ninyi na watoto wenu.
Tundu ni champion wa civil disobedience.
Kama walivyo watangulizi wake: Yesu, Mahatma Gandhi, Martin Luther, Nelson Mandela, Henry Thoreau, etc., amechagua kukataa kutii kwa sababu anaamini ndio njia sahihi ya kupambania haki.
Anajua wazi hatari iliyopo mbele yake lakini bado anafanya alivyofanya kwa sababu anaamini ndio jambo sahihi.
Wanaamini kwenye yale maneno ya Gandhi aliposema:
"They may torture my body, break my bones, even kill me. Then they will have my dead body, not my obedience."
Imani ya Tundu Lissu ni kuyaishi yale ambayo Mitch Leigh aliyeweka kwenye midomo ya Don Quixote wa Man of La Mancha:
To dream the impossible dream,โจTo fight the unbeatable foe,โจTo bear with unbearable sorrow,โจTo run where the brave dare not go.
To right the unrightable wrong,โจTo love pure and chaste from afar,โจTo try when your arms are too weary,โจTo reach the unreachable star.
This is my quest,โจTo follow that star --โจNo matter how hopeless,โจNo matter how far.
To fight for the rightโจWithout question or pause,โจTo be willing to march into hellโจFor a heavenly cause.
And I know if I only be trueโจTo this glorious questโจThat my heart will lie peaceful and calmโจWhen I'm laid to my rest.
And the world will be better for thisโจThat one man scorned and covered with scarsโจStill strove with his last ounce of courage.โจTo fight the unbeatable foe.โจTo reach the unreachable star.
Kwa hiyo, badala ya sisi kulia na kumwonea huruma, tunapaswa kujiangalia ndani yetu na kutafakari namna tunavyoshiriki kuhalalisha ushenzi anaopambana nao.
Uchungu wa ukweli ni kukataa kuendelea kutumika kukawaidisha na kurudufisha hali.
Uchungu wa kweli ni kuhakikisha mbegu aliyoipanda Lissu inamea na kuzaa matunda.
Kwa maneno yale yale ya Yesu: ANAKUFA ILI WENGI WAPATE KUPONA.
Tutafika.
2๏ธโฃ3๏ธโฃ4๏ธโฃ caps.
1๏ธโฃ4๏ธโฃ6๏ธโฃ goals.
3๏ธโฃ major international honours.
Only 1๏ธโฃ @Cristiano ๏ฟฝ2๏ธโฃ3๏ธโฃ4๏ธโฃ caps.
1๏ธโฃ4๏ธโฃ6๏ธโฃ goals.
3๏ธโฃ major international honours.
Only 1๏ธโฃ @Cristiano ๏ฟฝ2๏ธโฃ3๏ธโฃ4๏ธโฃ caps.
1๏ธโฃ4๏ธโฃ6๏ธโฃ goals.
3๏ธโฃ major international honours.
Only 1๏ธโฃ @Cristiano ๏ฟฝ2๏ธโฃ3๏ธโฃ4๏ธโฃ caps.
1๏ธโฃ4๏ธโฃ6๏ธโฃ goals.
3๏ธโฃ major international honours.
Only 1๏ธโฃ @Cristiano ๏ฟฝ2๏ธโฃ3๏ธโฃ4๏ธโฃ caps.
1๏ธโฃ4๏ธโฃ6๏ธโฃ goals.
3๏ธโฃ major international honours.
Only 1๏ธโฃ @Cristiano ๏ฟฝ2๏ธโฃ3๏ธโฃ4๏ธโฃ caps.
1๏ธโฃ4๏ธโฃ6๏ธโฃ goals.
3๏ธโฃ major international honours.
Only 1๏ธโฃ @Cristiano ๏ฟฝ2๏ธโฃ3๏ธโฃ4๏ธโฃ caps.
1๏ธโฃ4๏ธโฃ6๏ธโฃ goals.
3๏ธโฃ major international honours.
Only 1๏ธโฃ @Cristiano ๐