@Wakazi Kama nitakuwa sahihi niliamini show ya heshima kama ile ingechukuwa hata mwezi mzima ili kuwa na quality nzuri.ukiangalia concert ya miaka 50 ya hip hop iliyofanyika marekani kila kitu kilikuwa bora na hakuna mkongwe yeyote aliyebaki.Naamini TID alizungumza ukweli sahihi.
HUU NI UONGO FLAVA
It’s sad to see, Wasanii wanatumika kisiasa hadi kuruhusu Muziki wao kushushwa thamani ili Serikali Haramu ijihalalishe.
NINI KINASHEREKEWA? LINI KIMETIMIZA MIAKA 30?
Neno Bongoflava lina miaka takriban 32, which means na Muziki wenyewe ni older than 30. Sasa hiyo 30 imetoka wapi? Na lini tulikubaliana kuwa kila muziki wa Tanzania ni Bongoflava? Maana show ilijaa Rappers? nachojua ni kwa ujumla tunaitaga “Muziki wa Kizazi Kipya” na Bongoflava huwa ina refer Muziki wa Waimbajii. Ni kama Watu wame-force narrative!
UNAADHIMISHAJE MIAKA 30 YA KITU BILA KUHUSISHA WAASISI?
Yaani Show yao ilijaa watu ambao ni wa miaka 15-25 iliyopita na sio 30; kama kweli unataka kuenzi Muziki wetu, unapaswa uanze 34 - 30 years ago. Saleh Jabir, Mr II Sugu, Hard Blasters, Kwanza Unit, Mawingu Band, Unique Sistaz, GWM, Deplowmatz, etc Inabidi ushirikishe Taji Liundi, Mike Mhagama, Radio One, TVZ, ITV… Kiufupi mmepuyanga na kuudogosha muziki!
Ilikuwa golden opportunity ya kuwa na proper documentary, full representation ya Waasisi na ikiwezekana kuwaenzi Jukwaani, ila nyie mmejiwaza wenyewe tu na kutaka kuIhalalisha Serikali Haramu.
“BRIDGING THE GAP” & WHERE ARE THE FLAG BEARERS?
Ukiongelea kitu cha miaka 30, haimaanishi uwe na watu waliofanya Zamani tu. Show imekuwa ndogo sababu current flag-bearers wanao uwakilisha muziki hawakuwepo. Pengine wasingeimba nyimbo zao, bali kuimba za Wakongwe. Imagine Diamond na Ali Kiba wanaimba “Anakudanganya” wa B Love M, Zaiid anaimba “Kukuru Kakara Zako” wa Sos B, Young Lunya na OMG wanaimba “Kula Kona” ya Manzeshe Crew, au “Cheza Mbali na Kasheshe” wa GWM, Temayai waimbe “Run Tings” wa Kwanza Unit, Abby Chams na P Mawenge wanaimba “Sikiliza” wa Unique Sistaz ft Hashim Dogo.
POOR PERFORMANCES
Watu walioenda kuimba ilipaswa wafanye mazoezi ya live. Yaani Unaandaa show unawaza kuwaweka Hotelini tu na sio kuwapa budget ya Rehearsal ya japo mwezi. Where are your priorities?
Audience ilikuwa ya watu wa Gen X na Millennials, na ni watu ambao wana-appreciate live music na quality performances. Wamefata Nostalgia, basi mngewapa zawadi ya quality show badala “Show Mazoea”!
KUTOKIDHI HADHI
Huwezi kuwa na Lineup ya “Kifiesta fiesta” alafu ukaipeleka Mlimani City; mngefanya Viwanja vya Posta au Leaders! Pia demographic inayovutiwa na Miaka 30 sio watoto wa miaka 25! So kuipeleka M-City na kujua kuwa audience ni majority of 35 - 55 yrs, basi ingekuwa a VIP and VVIP event. Kuna watu wana Gout mmewasimamisha masaa pale!
Tatizo Waandaaji ni wa Mchongo; Fid Q ambae show zake huwa zina mapungufu, na Madee ambae hajawahi hata andaa uzinduzi wa Video Launch. Na nyuma ya pazia yupo Mtoa Maboko namba moja, Paul Makonda na Babu Talent.
HITIMISHO
Watu wanataka burudani, mmewapa burudani mbaya, na kibaya zaidi mkataka kuchomeka siasa! Na Wasanii Njaa na Chawa nao wanaendelea kujiuza kirahisi tu kwa watu ambao hawawasaidii chochote!
Platform pekee inayoenzi Bongoflava ni BONGO FLAVA HONORS ya Deiwaka Ent (Sugu), huu upuuzi mwingine ulikuwa ni SAMIA KINGS & QUEENS 2.0 wakitaka kuturubuni ila TUMESHTUKA.
The Leader
Watu ambao hawana haraka na watoto huenda ndio watu wenye utimamu na wanaofikiria zaidi kuliko wenye watoto.
Mtoto ni kitu serious ila sisi tunazaa kwa mazoea, unakuta hata lishe yake inamgonga halafu alete mtoto. Udumavu hautoisha.
Michezo.