Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, @HecheJohn, ametembelea familia ya Mwenyekiti wa BAVICHA Mkoa wa Iringa, Ibrahimu Myovela, ambaye kwa mujibu wa familia na chama hicho hajulikani alipo tangu alipopotea mwezi Februari mwaka huu.
Akizungumza na wanafamilia wa Myovela, Heche amesema hakuna maneno yanayoweza kufuta maumivu wanayopitia kutokana na kutoweka kwa ndugu zao ambaye amekuwa akiishi maisha ya kawaida na kuwajibika kwa familia na jamii.
"Hata tukisema mambo ya pole hayaoshi kwa sababu umezaa mtoto, umemlea amekuwa mkubwa, ana watoto, ni muwajibikaji, ambaye anajua kwao. Amesoma shule ya msingi hajawahi kupotea, amesoma sekondari hajawahi kupotea, anaishi anatunza watoto wake na biashara zake, leo tu apotee njia asijue nyumbani kwake," alisema Heche.
Kiongozi huyo amesema tukio la kutoweka kwa Myovela ni miongoni mwa matukio yanayoibua maswali kuhusu hali ya usalama na haki za wananchi nchini.
Amesema CHADEMA imeendelea kuzungumzia suala la watu wanaodaiwa kutoweka kwa mazingira yasiyoeleweka na kwamba hali hiyo inapaswa kupewa uzito unaostahili na mamlaka husika.
"Sisi tumekuja kuwapa uhakika kwamba tukizungumza tuna uongozi unaocheza na amani ya nchi hii, tunamaanisha haya mnayoyapitia," amesema Heche.
Heche pia amekosoa maelezo yanayotolewa kuhusu sababu za kutoweka kwa baadhi ya watu, akisema baadhi ya hoja zinazotolewa hazitoi majibu ya kutosha kwa familia zinazotafuta wapendwa wao.
Ziara hiyo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa CHADEMA pamoja na wanafamilia wa Myovela na wenzake ambapo chama hicho kinaendelea kutoa pole na kuahidi kuendelea kufuatilia suala hilo hadi ukweli kuhusu alipo kiongozi huyo utakapojulikana.
Myovela ni Mwenyekiti wa BAVICHA Mkoa wa Iringa ambaye, kwa mujibu wa taarifa za familia na viongozi wa CHADEMA, hajulikani alipo tangu mwezi Februari mwaka huu.
Watu waliojitambulisha kuwa Jeshi la Polisi wamemchukua Katibu wa Chama Kanda ya Serengeti, Mhe. Jackson Mnyawami, nyumbani kwake usiku huu wakisema wanampeleka Kituo cha Polisi Shinyanga. Mmoja wao alijitambulisha kama Masudi. Tutaendelea kutoa taarifa.
CHADEMA Kanda ya Pwani inapenda kuwafahamisha wanachama na umma kuwa Mwenyekiti wa Kanda, Mh. @ExMayorUbungo ameitwa kufika Ofisi ya RCO Kinondoni, Dar es Salaam, tarehe 16 Juni 2025
Wanachama, viongozi na wapenzi wa haki mnaombwa kuwa pamoja naye katika kufuatilia suala hili. Muda wa kuwasili ni saa 3:00 asubuhi katika Ofisi za RCO Kinondoni
Matukio ya mauaji, vurugu na umwagaji damu yanapotokea katika jamii, athari zake haziishii kwa waliopoteza maisha pekee. Mara nyingi huacha majeraha makubwa ya kisaikolojia kwa walioshuhudia, walionusurika, familia za waathirika, na hata wale waliohusika moja kwa moja katika matukio hayo.
Wataalamu wa afya ya akili hali hii huiita PTSD (Kiwewe cha Kisaikolojia Baada ya Tukio la Kutisha). Mtu anaweza kuendelea kuishi kwa miaka mingi baada ya tukio, lakini kumbukumbu za siku hiyo zikawa zinaendelea kumwandama.
Dalili zake zinaweza kuwa ndoto za kutisha, hofu ya mara kwa mara, kushtuka kwa sauti ndogo, kukosa usingizi, kujitenga na watu, hasira zisizo za kawaida, au kuona picha za tukio zikijirudia akilini kana kwamba linatokea tena.
Wakati mwingine hata wale waliopewa jukumu la kutekeleza amri katika mazingira ya vurugu wanaweza kubeba majeraha ya ndani yasiyoonekana. Wanaweza kuonekana wenye nguvu nje, lakini ndani wakiteswa na hatia, maswali ya dhamiri, huzuni au kumbukumbu zinazowatesa usiku na mchana.
Historia duniani imeonyesha kwamba baada ya matukio makubwa ya umwagaji damu, baadhi ya walionusurika, mashahidi na hata baadhi ya wahusika wamehitaji msaada wa kisaikolojia, kijamii na kiroho ili kurejesha utulivu wa nafsi zao.
Majeraha ya mwili yanaweza kuonekana na kutibiwa kwa haraka, lakini majeraha ya akili na dhamiri mara nyingi huchukua muda mrefu zaidi kupona. Ndiyo maana uponyaji wa taifa baada ya matukio ya vurugu hauhusishi haki pekee, bali pia ukweli, maridhiano, na huduma za afya ya akili kwa wale walioathirika.
Mama Samia, pengine wanaokuzunguka wanakudanganya sana. Na msingi wa uongo huo kwao unaweza kuwa biashara kubwa sana. Wanaweza kuwa wanatumia intimidation kama strategy muhimu kwa maslahi yao. Lakini ukweli ni kwamba siasa za aina hii za kuongeza presha na taharuki hazileti faida ya muda mrefu kwa nchi, bali kwa watu wachache tu wanaonufaika na hali hiyo.
Kuhusu Mh Tundu Lissu, kumuweka mahabusu au kumdhibiti kisiasa hakutaondoa changamoto za kisiasa, bali kunaendelea kuongeza taharuki zaidi ndani na nje ya nchi. Hasara kubwa si yeye kufanya siasa akiwa nje, bali ni kuendelea kumuweka mahabusu.
Kwa mtazamo huu, hii sio faida , bali inaweza kuwa faida kwa watu wanaonufaika na mvutano huu. Ndiyo maana wakati mwingine huonekana kuna mkakati wa kupandisha presha ili maslahi fulani yaendelee kunufaika. Hofu nayo ni biashara , tena Tax free.
Kazi yetu sio rahisi hata kidogo, lakini ni lazima tuifanye. Tusipoifanya sisi, watoto na wajukuu wa Tanzania watakuja kukojolea makaburi yetu. Lazima tuikwepe hii aibu. Ni jambo la kumshukuru Mungu kuwa hata kama kuna uonevu , lakini umeitwa Polisi. Maana siku hizi, “bring back” imekuwa “forever lost.”
TAARIFA.
Katibu wa kanda ya Serengeti Mh- @jacksonmnyawam2 amechukuliwa na watu waliojitambilisha ni Polisi nje ya nyumbani kwake.
Watu hao wamesema walikuwa wanamuhitaji kituo Cha Polisi Shinyanga.
WITO WA JESHI LA POLISI KWA MWENYEKITI WA CHADEMA KANDA YA PWANI, MH. BONIFACE JACOB
CHADEMA Kanda ya Pwani inapenda kuujulisha umma kuwa Mwenyekiti wa Kanda ya Pwani, Mh. @ExMayorUbungo, amepokea wito wa Kufika ofisi za RCO, Mkoa wa Kipolisi Kinondoni siku ya Kesho Jumanne Juni 16,2025.
Kwa mujibu wa taarifa tulizopokea kutoka kwa Mwenyekiti wa Kanda akiwa safarini kuelekea Ifakara Morogoro kwa ajili ya kushiriki mialiko ya mikutano ya hadhara ya CHADEMA Kanda ya Kati (Mkoa wa Morogoro) ameeleza kuwa amepokea simu kutoka Jeshi la Polisi Kimara (W).
Katika mazungumzo hayo, amearifiwa kuwa Polisi Wilaya ya Kimara wamepokea maelekezo rasmi yanayomtaka kufika katika Ofisi za RCO, Mkoa wa Kipolisi Kinondoni ,Dar es Salaam siku ya kesho Jumanne, tarehe 16 Juni 2026.
Jeshi la Polisi limemtaka kuwa anapofika katika ofisi hizo, aongozane na Mawakili wake au watu wake wa karibu.
Kufuatia wito huo, ninatoa rai na kuwaomba Mawakili wetu, Viongozi wote wa Chama (CHADEMA), Wanachama na Wapenda Haki wote kuungana pamoja na Mwenyekiti wa Kanda kuelekea Polisi Siku ya Kesho Jumanne Juni 16 , 2026 Kuanzia Saa 3:00 Asubuhi katika Ofisi za RCO, Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Dar es Salaam.
Imetolewa na:
Ntele Benjamin @ntele_bh
Katibu, CHADEMA Kanda ya Pwani
Juni 15, 2026.
Free Mnyawami
Watu waliojitambulisha kuwa ni askari wa Jeshi la Polisi wamefika nyumbani kwa Katibu wa Kanda ya Serengeti, Mhe. Mnyawami, na kuondoka naye wakidai kuwa wanamhitaji katika Kituo cha Polisi Shinyanga.
Kwa mujibu wa taarifa za awali, mmoja wa watu hao alijitambulisha kwa jina la Masudy.
Mhe. Mnyawami amechukuliwa akiwa nje ya nyumba yake wakati akijiandaa kuingiza gari lake ndani.
Hadi sasa, sababu za kuchukuliwa kwake hazijafahamika rasmi. Tunaendelea kufuatilia suala hili kwa karibu na tutatoa taarifa zaidi kadri tutakavyopata taarifa za uhakika.
Mkutano Mkuu Maalum BAWACHA Wilaya ya Ukonga Mkoa wa Ilala
Kukagua UHAI wa BAWACHA na Chama kwa ujumla
Na Maandalizi Oparesheni #KATIBAMPYA#FREETUNDULISSU
inayotarajiwa kuanza wakati wowote Kanda ya Pwani
WANAWAKE
CHIMBUKO LA MAENDELEO
#NOJUSTICENOPEACE#STRONGERTOGETHER
🚨 Manchester United are set to save over £8/9m in compensation for Rúben Amorim and his staff.
Follows agreement done between Amorim and AC Milan, as revealed earlier today ❤️🖤
🎥➕ https://t.co/3PEgqIE4VY
‼️TAARIFA KWA UMMA‼️
Watu waliojitambulisha kuwa ni police wamefika nyumbani kwa Katibu wa Kanda ya Serengeti Mhe. @jacksonmnyawam2 wamemchukuwa na kuondoka nae wanasema walikuwa wanamhitaji kituo cha police Shinyanga mmoja wa Polisi hao amejitambulisha kwa jina la Masoud
Wamemchukuwa muda wa saa 21:08 akiwa nje ya geti lake wakati anataka kuingiza gari lake ndani nilikuwa naongea nae akiwa ananipa mrejesho wa uchaguzi wa Mkoa wa Shinyanga na ratiba ya chama ya kesho ya Mkoa wa Simiyu.
Lucas Ngoto @lucas_ngoto
Mwenyekiti wa Kanda Serengeti.
"Tunapenda kuwataarifu wanachama, wafuasi wake na Watanzania wote kuwa Chama kitaendelea na Operesheni Katiba Mpya - Free Tundu Lissu katika Kanda ya Kusini, Nyasa na Magharibi." Mhe. @BrendaRupia Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimetangaza rasmi kuingia barabarani kupitia mikutano ya hadhara nchini kote, kikidai kuwa sauti za wapinzani zinaendelea kufinywa na vyombo vya dola huku serikali ikisusa kutenga fedha za Katiba Mpya kwenye bajeti kuu ya nchi.
Akizungumza leo Juni 15, 2026 mbele ya Waandishi wa Habari, Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa CHADEMA, Brenda Rupia amesema ziara hizo zitaanza Ukanda wa Kusini, zikihusisha Kanda za Kusini, Nyasa na Magharibi kuanzia Juni 18 hadi Juni 26, 2026.
Rupia amekosoa bajeti ya serikali ya mwaka wa fedha 2026/2027 iliyotangazwa wiki iliyopita kwa kutotenga fungu lolote la mchakato wa Katiba, akionya kuwa ikifika mwaka 2028 utakuwa ni ucheleweshaji uliopitiliza.
"Bado sauti zetu hazijasikika, bado sauti zetu zinafinywa na vyombo vya dola na CCM wanajimilikisha vyombo hivyo. Bajeti haina kipengele cha Katiba, na serikali haina mpango huo kwa mwaka huu wakati sisi tulishasema ikifika 2028 itakuwa ni 'too late' kuanza mchakato," amesema Brenda Rupia kwenye makao makuu ya chama hicho, Edwin House yaliyopo Mikocheni.
Katika hatua nyingine, Rupia ameshtumu Jeshi la Polisi kwa kupora sare za chama hicho (kombati) na kofia kutoka kwa muuzaji mkuu, Ndugu Mjela, akidai kuwa kuna njama za kuwavalisha watu wao ili wafanye fujo na kuisingizia Chadema wakati wa operesheni hizo.
Ratiba ya mikutano hiyo itaanza Juni 18 huko Nachingwea, ikifuatiwa na Masasi (Juni 19), Songea Mjini (Juni 20), Njombe na Makambako (Juni 21), Mbarali (Juni 22), Mbeya Mjini (Juni 23), Tunduma (Juni 24), Mpanda (Juni 25) na kuhitimishwa Tabora Mjini mnamo Juni 26, 2026.
Leo, 15/06/2026 Mhe. @HecheJohn, akiwa Mkoani Iringa, ametembelea familia za Mwenyekiti wa Bavicha Mkoa wa Iringa Ibrahimu Myovera, Antony Fyumagwa na Ally Kalolo katika Kata ya Ruaha, ambao kwa mujibu wa familia walipotea baada ya kufika Kituo cha Polisi Iringa kuripoti.