Leo nchi yetu inaadhimisha siku adhimu kuwakumbuka mashujaa wetu. Hii ni miamba na majabali ya kihistoria ambayo kwa kujitoa kwao kwa hali na mali kumetufanya sisi kuwa huru, kuishi huru, kuwa na Taifa letu, nyumbani kwetu, na kuwa hapa tulipo kama nchi.
Tunajenga mnara mrefu zaidi barani Afrika katika Jiji la Dodoma kama sehemu ya kuendelea kuwaenzi mashujaa wetu. Mnara huu ni alama nyingine ya uhuru wetu, shukrani yetu na kujitambua kwetu wapi tumetoka, wapi tupo na wapi tunakwenda. Nawaelekeza Ofisi ya Waziri Mkuu, Wizara ya Fedha na wote wanaohusika na ujenzi huu wa kihistoria kuhakikisha unakamilika kwa wakati na kwa viwango.
Siku hii pia ni siku ya tafakari. Tafakari ya kuendelea kuyaishi waliyoyaamini na kuyasimamia mashujaa wetu kwa kutunza amani, umoja, utulivu, mshikamano na kufanya kazi kwa bidii kwa Taifa letu.
Katika siku hii muhimu, tuendelee pia kukumbuka na kuzingatia kuwa Tanzania ni moja, itabaki kuwa moja na kamwe haitagawanyika. Tusikubali na hatutaruhusu mtu yeyote au kikundi chochote kutugawa kwa kisingizio chochote kile.
Mwenyezi Mungu Ibariki Afrika.
Mwenyezi Mungu Ibariki Tanzania.
Shirika la Reli Tanzania (TRC) linaendelea na majaribio ya mifumo ya vifaa vya uendeshaji wa Reli ya Kisasa (SGR) vinavyotengenezwa na Kampuni ya Hyundai Rotem katika Mji wa Changwon, nchini Korea ya Kusini.
Kampuni ya Hyundai Rotem ilipewa tenda ya kutengeneza vichwa 17 vya treni vya umeme pamoja na seti 10 za treni za Kisasa za EMU maarufu kama ‘Treni zilizochongoka’.
Timu ya Wataalamu kutoka TRC inayoundwa na Wahandisi mitambo, Wahandisi umeme, Mafundi na Madereva wa Treni imeweka kambi katika kiwanda cha Hyundai Rotem kwa ajili ya ukaguzi wa mifumo mbalimbali ikiwemo umeme, mfumo wa breki na vipimo katika utengenezaji wa vichwa vya treni vya umeme.
Kiongozi wa Timu hiyo ya Wataalamu ambaye pia ni Meneja wa mradi wa ununuzi wa vifaa vya uendeshaji vinavyotengenezwa na Kampuni ya Hyundai Rotem, Mhandisi Kelvin Kimario ameeleza kuwa zoezi la ukaguzi wa kiwandani ni muhimu ili kujiridhisha kuwa vifaa vilivyotengenezwa vimefuata masharti ya mkataba na viwango vya reli iliyojengwa.
“Bila kufanya ukaguzi wa kiwandani, kifaa kinaweza kusafirishwa na baanda ya kufika nchini unagundua hakifanyi kazi iliyokusudiwa, au vipimo vyake haviendani na miundombinu kama vile madaraja na mahandaki tuliyojenga, na matokeo yake kuisababishia Serikali hasara au kuhatarisha usalama wa miundombinu na Watumiaji”
#MillardAyoUPDATES
Kwa mashabiki wote wa Yanga tunaotumia mtandao wa Twitter kwa nguvu zetu na umoja wetu leo tunaweza kubadili profile picture na kuweka LOGO ya club kuonyesha mshikamano kuelekea kilele cha siku ya Mwananchi.
#WikiYaMwananchi#HiiImeenda